UN yaitaka Serikali ya Tanzania kuwalinda waandamanaji katika maandamano yaliyopangwa tarehe 9/12 na kuendelea

UN yaitaka Serikali ya Tanzania kuwalinda waandamanaji katika maandamano yaliyopangwa tarehe 9/12 na kuendelea

Uzima Tele

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2023
Posts
1,532
Reaction score
3,535
20251207_184959.jpg

#BREAKING: UN CALLS FOR LIFTING OF PROTEST BAN IN TANZANIA AHEAD OF DECEMBER 9
The Tanzanian government has been urged to uphold fundamental freedoms ahead of planned Independence Day protests on 9 December.

Spokesperson Seif Magango of the UN High Commissioner for Human Rights reminded authorities of their obligation to protect the rights to freedom of expression, peaceful assembly, and association.

He called on security forces to plan and implement operations in ways that allow citizens to fully exercise these rights.

The appeal comes amid reports that hundreds of people were killed and more than 2,000 detained following post‑election protests on 29 October, after which authorities escalated a crackdown on opponents culminating in a blanket nationwide ban on demonstrations announced on 3 December.

Under international law, Magango noted, firearms must never be used to disperse protests and can only be deployed as a last resort to counter imminent threats of death or serious injury.

The UN reiterated that commanders of security forces carry a responsibility to ensure respect for these principles ahead of any demonstrations, underscoring that Tanzania’s Independence Day should be marked by freedom, not repression.
 
Habari Mchepuko:
UMOJA WA MATAIFA (UN) WAITAKA SERIKALI YA TANZANIA KUONDOA MARA MOJA AMRI YA KUPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YALIYOPANGWA KUFANYIKA TAREHE 9/12/2025 NA KUENDELEA

Tanzania imetakiwa na UMOJA WA MATAIFA kulinda haki ya msingi ya uhuru wa watu kuelekea katika maandamano yaliyopangwa kufanyika siku ya uhuru wa Tanganyika Desemba, 9

Msemaji wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Seif Magango amezikumbusha mamlaka za serikali ya Tanzania kusimamia kikamilifu haki na uhuru wa watu kujieleza, kukusanyika na kujumuika

Amezitaka mamlaka za ulinzi na usalama za Tanzania kuhakikisha zinaweka mpango thabiti wa kuhakikisha wanasimamia na kuwalinda waandamanaji wanapitekeleza haki yao hii muhimu

Taarifa hii inakuja baada ya ripoti kuonesha kuwa mamia ya watu waliouwawa na vyombo vya ulinzi na usalama na wengine zaidi ya 2,000 kushikiliwa katika magereza mbalimbali nchini humo kwa sababu ya maandamano yaliyofanyika siku ya uchaguzi 29/10 na siku zilizofuata yaliyosababisha fujo na mapigano makubwa baada ya mamlaka kuyapiga marufuku kinyume cha sheria na haki

Seif Mugango anasema, chini ya sheria za kimataifa, ni marufuku na inakatazwa kabisa kwa vyombo vya usalama kutumia risasi za moto kusambaza au kuwapinga waandamanaji isipokuwa tu pale ambapo kweli Kuna tishio la uhai

UMOJA WA MATAIFA unawataka Makamanda wote wa vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania kuhakikisha kuwa wanabeba wajibu wao muhimu wa kuheshimu kanuni na misingi hii ya kiusalama wakati wote wananchi wanapoelekea kwenye maandamano ya amani ya tarehe 9/12 ikizingatiwa kuwa, siku hiyo ni siku ya uhuru wa Tanganyika, sio siku ya mapambano na mapigano

MY TAKE:
1. Sijui tutaona na kusikia tena ile Kauli ya "WHO ARE YOU?????"🤔🤔🤔
2. Personally, nilitegemea statement hii itolewe na custodian wa ulinzi wa haki, usalama na uhuru wa watu hapa nchini kwetu Rais Bi. Samia Suluhu Hassan.
3. Mtu aweza kujiuliza tu kuwa, ina maana mpaka kutoa statement zenye akili na ustaarabu kama hii mpaka tufundishwe na UN wewe Samia????
 
Ma TRA KO yao.
Sudan sasa wanaishi kama mbu UN imewasaidia nini?
Kongo watu wanaishi kwenye ufukara licha ya kuwa na madini mengi UN imewasaidia nini?
Vipi Libya UN imewasaidia nini?
Naongezea Gaza wameuliwa na wanaendelea kuuwawa UN wamefanya nini?UN iache mara moja kujipa umuhimu kwenye suala linalohusu Tanzania.Hawana Moral Authority ya kutoa wito wala tamko.
 
Ma TRA KO yao.
Sudan sasa wanaishi kama mbu UN imewasaidia nini?
Kongo watu wanaishi kwenye ufukara licha ya kuwa na madini mengi UN imewasaidia nini?
Vipi Libya UN imewasaidia nini?
Wote unao wataja walinyanyua bunduki,UN wanawaonya Tanzania kunyanyua bunduki yatatokea kama ya nchi ulizo zitaja.
Maandamano yapo kila nchi, Malawi kulikuwa na maandamano hadi yakazalisha katiba mpya ila hakukuwa na vifo, bunduki hazikuinuliwa,Zambia kulikuwa na maandamano vilevile ila bunduki hazikuinuliwa...
 
Bunduki hazikuinuliwa kwa sababu yalikuwa maandamano sio uporaji uchomaji wa miundo mbinu na husda dhidi ya watanzania waliojiwekea vitega uchumi vyao baada ya kufanya kazi bila kusahau kuvamia na kuchoma vituo vya Polisi.Bunduki ziliinuliwa kwa sababu kulikuwa na kila sababu ya kufanya hivyo.
 
Hawa UN nao ni mbwa wasio na meno wala kucha.

Hapa bwana wao marekani angekuwa ana mahesabu napo sasa hivi chura kiziwi yupo guantanamo.
Kwa kuwa basha wao hana mpango napo, wababweka bweka tu bila msaada.
 
Rudi kasome comment ya niliye kuwa namjibu. Hajaongelea MO29,ila ametaja nchi zilizo athirika kwa vita ya ndani.
Kwanini mnakimbilia sana kutaja uharibifu wa mali ila hamuongelei kwanini wamefikia hatua ya kuandamana?
MTU MASKINI HUONGELEA UHARIBIFU WA MALI,HATHAMINI NAFSI ZILIZOPOTEA
 
Habari Mchepuko:
UMOJA WA MATAIFA (UN) WAITAKA SERIKALI YA TANZANIA KUINDOA MARA MOJA AMRI YA KUPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YALIYOPANGWA KUFANYIKA TAREHE 9/12/2025 NA KUENDELEA

Tanzania imetakiwa na UMOJA WA MATAIFA kulinda haki ya msingi ya uhuru wa watu kuelekea katika maandamano yaliyopangwa kufanyika siku ya uhuru wa Tanganyika Desemba, 9

Msemaji wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Seif Magango amezikumbusha mamlaka za serikali ya Tanzania kusimamia kikamilifu haki na uhuru wa watu kujieleza, kukusanyika na kujumuika

Amezitaka mamlaka za ulinzi na usalama za Tanzania kuhakikisha zinaweka mpango thabiti wa kuhakikisha wanasimamia na kuwalinda waandamanaji wanapitekeleza haki yao hii muhimu

Taarifa hii inakuja baada ya ripoti kuonesha kuwa mamia ya watu waliouwawa na vyombo vya ulinzi na usalama na wengine zaidi ya 2,000 kushikiliwa katika magereza mbalimbali nchini humo kwa sababu ya maandamano yaliyofanyika siku ya uchaguzi 29/10 na siku zilizofuata yaliyosababisha fujo na mapigano makubwa baada ya mamlaka kuyapiga marufuku kinyume cha sheria na haki

Seif Mugango anasema, chini ya sheria za kimataifa, ni marufuku na inakatazwa kabisa kwa vyombo vya usalama kutumia risasi za moto kusambaza au kuwapinga waandamanaji isipokuwa tu pale ambapo kweli Kuna tishio la uhai

UMOJA WA MATAIFA unawataka Makamanda wote wa vyombo vya ulinzi na usalama Tanza kuhakikisha kuwa wanabeba wajibu wa muhimu wa kuheshimu kanuni na misingi hii ya kiusalama wananchi wanapoelekea kwenye maandamano ya amani ya tarehe 9/12 ikingatiwa kuwa, siku hiyo ni siku ya uhuru wa Tanganyika, sio siku ya mapambano na mapigano
 
Bunduki hazikuinuliwa kwa sababu yalikuwa maandamano sio uporaji uchomaji wa miundo mbinu na husda dhidi ya watanzania waliojiwekea vitega uchumi vyao baada ya kufanya kazi bila kusahau kuvamia na kuchoma vituo vya Polisi.Bunduki ziliinuliwa kwa sababu kulikuwa na kila sababu ya kufanya hivyo.
Wote walioandamana walifanya uharibigu huo?
Kwanini watu wamefikia hatua hio ya kuandamana ?
 
Hawa UN nao ni mbwa wasio na meno wala kucha.

Hapa bwana wao marekani angekuwa ana mahesabu napo sasa hivi chura kiziwi yupo guantanamo.
Kwa kuwa basha wao hana mpango napo, wababweka bweka tu bila msaada.
It's not so fast just like that

It's done step by step

Do not worry!......Itakuwa hivyo, wewe hata usiwe na wasiwasi wala mashaka

We know and they know exactly the consequences of their evil actions

Life is paid by life

Maisha ya mtu hulipwa kwa maisha ya mtu mwingine vivyo hivyo

Naona kama hujaelewa vizuri:

Nasema: Auae kwa upanga, naye vivyo hivyo atauwawa kwa upanga!
 
Back
Top Bottom