UN - Tusidanganyane, kama Taifa Tulipwaya

Kuna haja ya kuambiana ukweli. Kama taifa UN hatukufurukuta.

Siyo siri, madhumuni ya mkutano ule ilikuwa ni kwa mataifa kuweka wazi sera zao za nje zenye kuelezea maingiliano baina ya nchi na nchi.

Mkutano ule haukuwa wakutafutia wawekezaji, kutangazia utalii wala kuhusiana na mambo ya ndani ya nchi.




Badala yake tukatumia muda kujielekeza kwenye mambo ya kijinsia. Kwani tulivisahau vyuma vilivyo tikisa dunia hii wakiwamo akina Angel Merkel, Thatcher, Indira Gandhi, Golda Meir, nk?

Usawa wa kijinsia katika mataifa nje ya Africa si agenda za kupeleka UN labda AU. Huko waungwana walikwisha toka zamani. Mama Clinton alikuwa achukue urais wa dunia na wala si kwa kudra za Mola.

Taarifa za Corona tulizosoma ni za WHO ambayo ni agency tanzu ya UN yenyewe.

Kwamba tuna ushauri kuhusu chanjo ya Corona ambayo aghalabu tungetaka hata copyright kwenye chanjo isiwepo wakati tunapewa bure?

Hatuna neno lolote kuhusu nyungu, maombi, mikaratusi, michai chai, malimao au hata na matango pori mengine?

Hatuna neno lolote kuhusiana na vita vya kiuchumi hasa hasa mabeberu dhidi ya Tanzania?

Hatuna neno kumhusu beberu yeyote na upigaji wake kwenye chanjo, barakoa, PPE au kuhusu Corona kwa ujumla?!

Kwani dunia haikupata kutusikia na misimamo yetu na shujaa wetu wanayeshuku Corona haikumnusuru?

Kwani zile takwimu za ugonjwa wa Corona ambazo dunia imekuwa ikituasa kuzitoa tumewahi kuzitoa?

Tupitieni hotuba za wengine kulinganisha na ya kwetu.

Ama kwa hakika hatukufua dafu!

Ukweli mtupu.....tulipwaya sana! Lini tutajifunza nini kinatakiwa kuongelewe na kwa wakati gani na wapi?????

Inachosha Sana.
 
Back
Top Bottom