Umwinyi(mamwinyi) warejea kupitia Tour guiding nchini Uganda

Umwinyi(mamwinyi) warejea kupitia Tour guiding nchini Uganda

McCarthy

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2017
Posts
506
Reaction score
554
Ni kwamba katika enzi za ukoloni suala la kuwaona watu wenye asili ya Afrika wakiwa wamembeba Mwarabu, au Mzungu lilikuwa ni suala lisilohaba hasa maeneo ya pwani. Vitendo hivyo vilifanywa hasa na watu wenye wadhifa wa Mwinyi(na waliitwa Mamwinyi), wakiwalazimisha manyampara, manamba na/au watumwa(Waafrika) kuwabeba.

Hata hivyo tabia hii ilipingwa vikali na wapigania uhuru na wanamapinduzi wa Kiafrika.

Katika hali ya kushangaza, hali hii imeanza kurejea tena barani Afrika kwa mtindo mwingine. Inafanyika huko Uganda ambapo waongozaji wa watalii (hasa watalii wa kizungu) huwabeba watalii katika kile kiitwacho "tour guiding". Hatari sana.

IMG-20180220-WA0018.jpg
 
Siamini kama watalii ndo wanataka hivyo labda ni ubunifu wa magaidi kuongeza kipato!
 
This looks like is a movie.. all for money? Aseeeh
 
Mbona hao Waganda wemevaa kama wametoka Jela, au siku hizi wanatumia wafungwa?

Definetely that must stop.
 
AISEE NIKIONA HII PICHA NAKUMBUKA VILE VITABU VYA HISTORIA VYA SHULE YA MSINGI WAKATI SISI WAHENGA TUNASOMA
 
Sio mbaya kwakua wanafanya kazi hiyo kwa hiari na wanalipwa pesa (kazi ni kazi ili mradi mkono uende kinywani).
Tofauti na enzi za utumwa kwakua walitumikishwa bila ridhaa na hawakulipwa chochote,,
Naunga mkono hoja,,
Vyuma vimekaza jamani msinipopoe kwa mawe..!!
 
Waganda sijui kwa nini ..wana vituko vya ajabu ajabu sana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom