Hivi ninavyofungua huu uzi kuna kijana jirani yangu yamemkuta. Yeye ni mmoja wa wale wanaoitwa 'watoto wa nje' (neno hili silipendi kabisa,kwangu mtoto ni mtoto tu). Mzee wake amefariki hakuacha wosia. Sasa mke wa marehemu na wanae wa kuzaa wamegangamala wanasema mtoto wa 'nje' kisheria hana haki ya kurithi chochote.It is too sad maana hata baba yake alikuwa anampenda sana kijana huyu na bado hajamaliza shule.Kwa wale watu wazima chonde chonde jamani tuandike will ili mali yetu tuigawe kulingana na utashi wetu. Na kwa vijana wakumbusheni wazazi wenu kuandika will wala msiogope kuwambia,ni kwa faida ya wanandugu wote na kupunguza mizozo isiyo na lazima.
Wezetu wa mbele huko (wazungu)ni kitu cha muhimu sana lkn huku kwetu wazee wakiambiwa wanaona km wanchuriwa kufa au watoto wana tamaa ya mali, ila kiukweli ni muhimu sana kuandika wosia.
Hivi ninavyofungua huu uzi kuna kijana jirani yangu yamemkuta. Yeye ni mmoja wa wale wanaoitwa 'watoto wa nje' (neno hili silipendi kabisa,kwangu mtoto ni mtoto tu). Mzee wake amefariki hakuacha wosia. Sasa mke wa marehemu na wanae wa kuzaa wamegangamala wanasema mtoto wa 'nje' kisheria hana haki ya kurithi chochote.It is too sad maana hata baba yake alikuwa anampenda sana kijana huyu na bado hajamaliza shule.Kwa wale watu wazima chonde chonde jamani tuandike will ili mali yetu tuigawe kulingana na utashi wetu. Na kwa vijana wakumbusheni wazazi wenu kuandika will wala msiogope kuwambia,ni kwa faida ya wanandugu wote na kupunguza mizozo isiyo na lazima.
Onana na wanasheria waeleze unavyotaka usia wako uwe then watakupa utaratibu.taratibu za kuandika wosia zikoje hususani kwa walio mikoani
eeehh,ukimkumbusha atasema unataka kumuua,so tumia busara ya ziada katika zoezi hilo@bishanga umeongea kiutu uzima! acha nimkumbushe babu yangu!
Ukimfuata mtz umwambie aandike wosia atasema wamchuria.
Ona sasa yanayomkuta mtoto wa watu....
Hivi ninavyofungua huu uzi kuna kijana jirani yangu yamemkuta. Yeye ni mmoja wa wale wanaoitwa 'watoto wa nje' (neno hili silipendi kabisa,kwangu mtoto ni mtoto tu). Mzee wake amefariki hakuacha wosia. Sasa mke wa marehemu na wanae wa kuzaa wamegangamala wanasema mtoto wa 'nje' kisheria hana haki ya kurithi chochote.It is too sad maana hata baba yake alikuwa anampenda sana kijana huyu na bado hajamaliza shule.Kwa wale watu wazima chonde chonde jamani tuandike will ili mali yetu tuigawe kulingana na utashi wetu. Na kwa vijana wakumbusheni wazazi wenu kuandika will wala msiogope kuwambia,ni kwa faida ya wanandugu wote na kupunguza mizozo isiyo na lazima.
Kwa sheria ilivyo sasa watoto wa nje wanapoteza haki ya kurithi hasa kama baba hakuwatambulisha/ama kuwaweka wazi kuwa ni wanawe....na kwa kusema ukweli mimi naona hii ni fair tu. Kama una mtoto wa nje ni vema ukamchukuwa na kukaa nae/au kuhakikisha anatambulika formally kuwa ni mwanao/mtegemezi wako.
Kutegemea na dini ya muhusika, wosia peke yake unaweza usiwe na nguvu.....kama kuna vitu unataka 'kumrithisha' mtu ambaye kisheria hana haki ya kukurithi ni vema ukamgawia sehemu yake akaanza kuimiliki kabla wewe hujafa.
Mkuu SMU una maana will ambayo imeandikwa vizuri ikawa na ushahidi wa saini kwa mujibu wa sheria (nasikia ni watu wawili) mtu akifariki bado inaweza kuwa contested? Kivipi?
Mimi nasema hivi wanaume mnashindwa kuandika wosia mnadai mnachuriwa hili gumu, Jamani mie nawaomba wababa wale wenye mali zingine zile za pembeni ambazo mke hajui tafadhali muache mchezo huo. Binamu zangu wamekuwa maskini kwelikweli sababu tu ya usiri wa baba, watu wengine wanafaidi inasikitisha sana.
nami pia kuna watu ninaowafahamu, ukweli ni kwamba sio mali tu bali inasaidia hata mambo ya mazishi (tumeona maiti zinagombewa kidini), sehemu ya kuzikwa nk. Lakini kwa suala hili mkuu mkuu linatukumbusha pia kuwa integrity ya mtu ni muhimu, sio kitu kizuri kuwa na watoto wengi wa nje kwa maana ni kielelezo cha kutokuwa mwaminifu kwa familia. Ni changamoto!
hili ni kweli kabisa. Inatakiwa hii elimu itolewe sana!
ni jambo zuri sana, hata mimi kuna kanyumba nakafuatilia huko mbeya kwa kuwa baba yenu kampa mtoto wake aliyezaa na mama mwingine, ndo niko kwenye process na kuonana na mwanasheria wangu.
Kwa mfano katika uislamu kuna utaratibu maalumu wa kurithi/kurithisha (very detailed, kwa mtizamo wangu). Na pia will ambayo muhusika anatoa mali yake yote kwa watoto wa nje (au watu ambao kisheria sio warithi) halafu wale wa ndani wakose chochote....naamini inaweza kuwa contested.....hasa kama kwa mfano watoto bado ni tegemezi. Kwa mfano hebu chukua mtu kaandika will ambayo anaitoa nyumba anayoishi yeye na familia yake kwa mtu ambaye sio mwanafamilia na kitendo hichi kufanya watoto na mama kukosa pahala pa kujihifadhi, unadhani hiyo will hata kama imesainiwa itakubalika (tuangalie kimantiki tu!)?