Naomba kuuliza kuhusu umuhimu wa nambari 3 katika tamaduni za Kitanzania, aidha kihesabu au katika imani za watu (belief/religious systems)kwa mfano kwenye matambiko, nk. Kwa nini nadodosa hili? Naomba nitoe mifano.
Kwenye lugha ya Kiswahili tuna nafsi tatu: mimi, wewe, yeye; sisi, nyinyi, wao. Tulifikaje kwenye matumizi ya hizi nafsi zinazojumuishwa kwa nambari 3? Zaidi ya hapo, waandishi mashughuli kama washairi marehemu Shaaban Robert na Mathias Mnyampala waliandika aidha kwa makusudi au bila kujuwa kuhusu umuhimu wa nambari 3. Shaaban Robert aliandika kuelezea umuhimu wa ngazi tatu katika maisha ya mwanadamu: kuzaliwa, ndoa, na kifo (a triplet). Mathias Mnyampala aliandika hadithi nzuri kuhusu kisa cha mrina asali na wenzake wawili (also a triplet). Kulikoni washairi maarufu walilenga hii nambari 3?
Aidha, tamaduni nyingine duniani pia zimeipa hii nambari tatu umuhimu wa pekee. Marumi waliabudu miungu wakuu watatu vinyo hinyo majirani wao Magiriki. Mpaka hivi leo Wakristo wanaamini Utatu Mtakatifu (God the Father, the Son, and the Holy Spirit). Kuzaliwa kwa Yesu kuliashiliwa na nyota iliyowaongoza wafalme watatu (the three magi) hadi Yerusalemi. Na karne za mwanzo za enzi za Ukristo ziliashiria huo utatu mtakatifu hususan katika matumizi ya alama ya jich ndani ya “triangle.” The eye in the triangle representing God’s all-seeing eye.
Wajapani wanaamini kuwa Taoism ina mandhari tatu, mbingu, ardhi na bahari, na kila moja ina mtawala maalum. Wajerumani wana Imani katika utamaduni wao kuwa makabila matatu muhimu ya Kijerumani yalitokana na uzawa wa Mannus yaani Wodan, Thorr, na Donar. Linganisha hadithi hii na hadithi ya Wayahudi kwenye Mwanzo (Genesis) sura ya 9 aya ya 19).
Ni kutokana na maelezo hayo hapo juu ndo maana nauliza kama kuna anaelewa umuhimu wa namba 3 katika jamii zetu. Nahisi kuwa Watanzania pia tuliipa hii nambari 3 umuhimu wa pekee na ningependa kujuwa Zaidi. Kwa kutamatisha, ilikuwaje mama zetu waliamua kupika kwa kutumia mafiga matatu na siyo manne?
Naomba kuuliza.
NB: HUU MJADALA NIMEUTOA KWENYE MTANDAO MMOJA, NIKAONA UNAFAA KUJADILIWA HAPA. KWAHIYO MIMI SIO MWANDISHI.