Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,169
- 48,451
Kwanza nianze na tafsiri ya neno "Lock down" ambalo limekuwa ni shina la mijadala hapa JF na Tanzania kwa ujumla hasa kwenye medani ya siasa.
"Lock down" ni amri maalum kwa wakati maalum inayotolewa na wenye mamlaka kwa eneo husika kuzuia watu kufanya jambo fulani kwa kuwatenga ama kuwazuia kabisa watu hao kushirikiana kwa lengo la kufanya tathimini ya ukubwa wa tatizo,kuzuia kuenea kwa tatizo, kukusanya rasirimali za kupambana na tatizo, na kupata muda wa kufanya tafakuri jinsi ya kuendenda kwa ajili ya siku zijazo baada ya tatizo kupita.
Kwa ivo "lock down" si tendo la kiwendawazimu bali ni mfumo maalum wa kitaalamu wa kupambana na majanga mbali mbali kwa njia za kisayansi. "Lock down" kwa kuwa ni jambo la kisayansi haifanywi kwa kukurupuka.
Tangu kuingia kwa Janga la Korona hapa Tanzania, kama jamii tumegawanyika kwenye makundi mawili. Kuna kundi la wale waliotaka itangazwe "Lock down" kuinusuru nchi na kuenea kwa COVID-19 na kuna kundi linalopinga kuanzishwa kwa "lock down". Makundi yote mawili yana hoja zao!!
Kundi linalopinga kuwepo kwa "Lock down" linadhani kwamba "lock down" maana yake ni kufunga ama kuzuia kufanyika kwa kila kitu kwenye nchi yetu kwa kukurupuka. Hoja yao kubwa ni kwamba Uchumi wa nchi yetu utaporomoka kwa kasi ya ajabu sana.
Lakini hata kwenye zile nchi za Ulaya na Marekani ambako "Lock down" imefanyika, siyo kwamba kila kitu kilizuiliwa kwa muda wote kwa watu wote, mambo muhimu yaliendelea kwa mpangilio na utaratibu maalum uliosimamiwa na serikali.
Ni kweli kwamba kazi za Uzalishaji zilisimamishwa kwa kiwango kikubwa, lakini kazi nyingi za kiofisi zilifanyika tokea nyumbani. Kwa ivo hata hapa Tanzania hakuna mtu anayesema kwamba watu waache kufanya kazi, bali tunasema kazi zile muhimu tu ndizo zifanyike tena kwa utaratibu maalum.
Hapa kwetu ambako miji sehemu yake kubwa sana haijapangwa (hili siyo kosa la COVID-19) watu wanaishi shaghalabaghala sana kiasi kwamba kuitunza ile kanuni ya kukaa mbali mbali (social distancing) inashindikana, ni lazima kuwe na sheria ya "Lock down" ili kulazimisha watu wasio na kazi za muhimu sana kuonekana mitaani.
Wakati tunaambiwa kwamba maisha ya watanzania yameboreka kwa kipindi cha miaka 4 iliyopita, bado tena tunaambiwa watanzania wote wasipotoka kwenda kazini hawawezi kulisha familia zao kwa siku husika. Hivi ni kweli kwamba kila mtanzania anatakiwa atoke kwenda kutafuta ndiyo alishe familia yake? KWA NINI?
"Lock down" itasidia kuzuia kuenea kwa kasi kwa maambukizi ya COVID-19, kutupa muda wa kujipanga, kufanya tathimini ya hasara inayotokea kwenye uchumi wetu kutokana na COVID-19, na kubwa kuliko yote ni kujipanga na kupambana na athari za uchumi wa dunia unaoporomoshwa na janga la ugonjwa huu.