Tukuza hospitality
JF-Expert Member
- Jul 30, 2022
- 325
- 704
Na Constantine J. S. Mauki March 2025
Utangulizi
Asilimia 60 ya mwili wa binadamu ni maji. Ila kwa mtoto mchanga asilimia 80 ya mwili wake ni maji. Kiwango hiki cha maji hupungua kadri ukuaji wa mtoto unavyoendelea; na hatimaye hufikia asilimia 60, ambayo ndio wastani kwa watu wazima.
Manasvi Jain (17 Jan, 2024), anasema, kunywa maji inachukuliwa kama ni kazi rahisi, ambayo haihitaji maarifa makubwa. Anaendelea kwa kuuliza, unajua unapokunywa maji, yana athari chanya ya Moja kwa Moja katika mwili wako? Kwa hiyo ni muhimu kuyanywa kwa usahihi.
Faida za Maji Mwilini
1. Husaidia mmeng'enyo wa chakula, hivyo kuepusha Matatizo ya choo kigumu.
2. Kusafisha mwili. Husaidia kuondoa sumu mwilini kupitia haja kubwa, mkojo na jasho.
3. Husaidia kudhibiti uzito usiofaa.
4. Huepusha kichwa kuuma.
5. Huupa mwili nguvu.
6. Huipa ngozi Hali ya unyevunyevu.
7. Huboresha afya ya ngozi.
8. Husaidia kuepusha saratani ya utumbo na ya kibofu cha mkojo.
9. Huwezesha Figo kufanya kazi vizuri.
10. Husaidia kujenga misuli na kuzalisha seli mpya.
11. Huchochea ukuaji wa nywele zenye afya Bora.
12. Huzuia kujijenga kwa mawe kwenye Figo.
13. Hudhibiti kiungulia.
14. Huimarisha Kinga ya mwili.
Utaratibu wa Kunywa Maji
1. Kunywa maji ya moto au vuguvugu. Maji vuguvugu husafisha na kuondoa sumu mwilini kwa ufanisi zaidi kuliko maji baridi au ya kawaida.
2. Kaa wakati unapokunywa maji. Kunywa maji ukiwa umesimama inavuruga uwiano wa vimiminika mwilini, jambo ambalo linaweza kusababisha Matatizo ya kiafya kama maumivu ya viungo (pingili za mwili), shida ya mmeng'enyo wa chakula, na ufyonzaji wa madini mwilini.
3. Kunywa Maji taratibu. Kunywa maji taratibu (kidogo kidogo) huruhusu mwili kuchakata virutubisho na madini vizuri. Pia Husaidia Figo kuchakata vimiminika vyote.
4. Anza siku siku yako na glasi ya maji vuguvugu. Kunywa maji vuguvugu asubuhi husaidia kuondoa sumu zilizojilimbikiza mwilini usiku mzima na kusafisha mfumo wako wa kumeng'enya chakula. Pia huboresha metaboli, hivyo kusaidia kudhibiti uzito.
5. Epuka Kunywa maji wakati wa Milo. Unywaji wa maji wakati unakula, inaweza kupunguza nguvu ya tindikali zinazosaidia umeng'enyaji wa chakula, hivyo kuathiri mfumo wa umeng'enyaji wa chakula. Unaweza Kunywa maji mengi saa Moja kabla au baada ya kula chakula.
6. Kiasi Cha Maji ya Kunywa kwa siku. Kwa wastani, mtu mzima anapaswa Kunywa maji Lita 2 kwa siku. Mtu mwenye uzito wa kilo 25 anatakiwa Kunywa maji Lita 1 kwa siku, mwenye kilo 50, maji Lita 2 kwa siku.
Kwa ujumla, mambo yafuatayo yanaweza kufanya kiasi Cha Maji ya Kunywa kubadilika:
i. Uzito. Kiasi Cha Maji ya Kunywa kinaongezeka kulingana na uzito wako; mfano: mtu mwenye uzito kati ya kilo 60 na 75 atakunywa maji kati ya lt 2.5 na 3.0......
ii. Shughuli unazofanya. Kama unafanya kazi au mazoezi yanayokufanya utoke jasho jingi, mwili utahitaji maji zaidi.
iii. Hali ya hewa. Kipindi cha baridi, mwili haupotezi maji mengi, lakini kipindi cha joto, mwili hupoteza maji mengi kupitia ngozi.
iv. Hali yako ya Afya. Hali ya Afya Hufanya mwili kuhitaji kiasi kidogo au kikubwa cha Maji.
Hitimisho
Maji ni muhimu SANA katika mwili wa binadamu, hivyo, ni muhimu mtu mmoja mmoja, Jamii, asasi mbalimbali na serikali kuhakikisha kuwa swala la upatikanaji wa maji linazingatiwa katika miradi yote ya maendeleo.