Kupiga kura ni haki ya kikatiba inayomwezesha kila Mtanzania kushiriki katika maamuzi ya nchi kwa njia ya amani, kupitia kura wananchi huamua ni nani awaongoze katika nafasi za kisiasa kama Rais, Wabunge na Madiwani na hii ni njia halali ya kushiriki katika ujenzi wa taifa na kuhakikisha kuwa sauti ya wananchi inasikika.
Ni wajibu wa kiraia kwa kila mwenye sifa ya kupiga kura kuhakikisha anatumia haki hiyo, kutojitokeza kupiga kura ni kuruhusu watu wengine kufanya maamuzi kwa niaba yako, jambo linaloweza kusababisha kuchaguliwa kwa viongozi wasiowatumikia wananchi ipasavyo.
Wananchi wanapojitokeza kwa wingi kupiga kura, wana nafasi ya kuchagua viongozi waadilifu na wenye uwezo wa kuleta maendeleo, Kupitia kura matatizo ya huduma duni za jamii kama elimu, afya na maji yanaweza kushughulikiwa kwa kuchagua viongozi wanaojali maendeleo ya wananchi.
Aidha, kupiga kura huimarisha misingi ya demokrasia na utawala bora, inawafanya viongozi walioko madarakani kuwajibika kwa wananchi wakijua kuwa wanaweza kuondolewa kwa kura iwapo hawatatimiza ahadi zao.
Kila Mtanzania anapaswa kutambua kuwa kura yake ni sauti yake na anatakiwa kuwajibika ifikapo Oktoba Ili taifa lipige hatua, kila mwananchi mwenye sifa anapaswa kujitokeza kwa hiari na kwa wingi kushiriki katika uchaguzi kwa kupiga kura kwa amani na utulivu.
#OktobaNawajibika
#OktobaTunatiki
#KuraYanguSautiYangu