Umuhimu wa Bahari Duniani

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,258
Bahari ni eneo kubwa penye maji ya chumvi. Katika Kiswahili cha kila siku neno hili hutumiwa pia kwa kutaja magimba madogo zaidi ya maji kama ziwa.

Kwa maana ya kijiografia bahari hasa ni bahari kuu ya dunia yaani maeneo makubwa ya maji ya chumvi ambayo ni kama gimba moja. Bahari kuu ya dunia inafunika asilimia 71 za uso wa dunia.
Tena neno "bahari" linatumika pia kwa maeneo ambayo ni bahari za pembeni za bahari tatu kubwa kama vile Mediteranea, Baltiki.

Bahari ni muhimu sana kwa ajili ya maisha na hali ya hewa duniani. Bahari zinashika asilimia 96.5 za maji yote ya dunia. Maji ya bahari yana takriban asilimia 3.5 za chumvi ndani yake. Kiwango hiki hutofautiana kidogo katika sehemu mbalimbali kutokana na uvukuzaji mkubwa penye joto kwa matumizi ya kibindadamu hata kwa matumizi ya mimea na wanyama wa nchi kavu haifai. Lakini bahari pia ni chanzo cha mvua kwa sababu mawingu hutokea hasa juu ya bahari. Katika mwendo wa uvukizaji chumvi inabaki na mvuke unapaa bila chumvi ndani yake kuwa mawingu na kurudi katika mwendo wa usimbishaji. Usimbishaji unaleta maji yanayojaza mito na maziwa hata akiba za maji chini ya ardhi.
Tangu zamani bahari ni njia kuu za mawasiliano ya kimataifa. Hadi leo asilimia 92 ya mizigo yote hubebwa kwa meli baharini kati ya bandari

  1. Mvumo wa Mawimbi ya Bahari ni Kinanda cha Ubongo kikikuondolea msongo wa mawazo na kuburudisha akili
  2. Jua la Bahari ni dawa muhimu sana kwa ngozi yako nchi nyingi sana watu wake hutumia muda mwingi kujianika baharini
  3. Kutazama maji ni tiba asilia na mbadala na haiswihi mtu kwenda airport kwa masaa matatu ukiancha bahari ya msaa mawili ambapo ungefaidika sana, ni muhimu pia hapa kufahamu kwamba unaposafri na boti ni vyema ukapenda kukaa nje ukipigwa na upepo na kutazama maji badala ya kuhemea pumzi ya mzungu ndani
  4. Miale ya jua inayokupia pia ni vitamini D bora kabisa
  5. mchanga wa bahari pia ni dawa
  6. maji ya bahari ni dawa kadhalika
  7. Upepo wa Bahari ni pafu mbadala kwa binadamu
  8. na zaidi sana kitoweo cha samaki toka baharini ni dawa muhimu sana katika kukukza upeo wako
Mshana JR na Mzizimkavu watakuja na nondo zaidi
 
Dirty Mind!!

Nlijua unaongelea bahari ile nyingine yaan uko chumban ni mwenzako halafu unakutana na Bahari ile sasa khaaa!!
wacha ni editi iende jukwaa la mabo ya kikubwa
 
Ukiachana na ishu za ushirikina baharini na mambo mengi ya ajabu mengi uliyoongea ni kweli kabisa labda tu kwa kuongezea ni kwamba
-kama unasafiri na meli boat mtumbwi jahazi nk ikitokea ukapata kichefuchefu au kujisikia kutapika lala chali Ukiangalia juu
-bahari pekee ndio ambayo mpaka leo kuna viumbe mimea na vitu vya ajabu vinavumbuliwa
 
IMA JUNGU KUU HALIKOSI UKOKO
 
Viumbe wa kushangaza baharini
1454322662696.jpg
1454322668355.jpg
1454322673398.jpg
1454322682845.jpg
 
Chini ya bahari kuna idadi kubwa ya Viumbe kuliko huku juu, kuna milima, mabonde ya kutisha, pango na miti mirefu, pia bahari mpaka Leo hatujui wapi Yale maji yakitoka yanakwenda na yakirudi hujui wapi yatoka. Hii ni miujiza mikubwa. Bahari INA maua mazuri kuliko huku juu na viumbe wa kutisha hatari. Huenda siku nyingine ukakutana na ngombe chini ya bahari.

Kuna chunusi unaweza ukazama kwenye maji ya kwenye kifua tuu na usionekane tena hata kama ulikua unajua kuogelea. Nimambo mengi huwezi kuyamaliza.

Mshàna Jr lile tatizo language halijesha naomba unisaidie.
 
Wanasayansi wa zama hizi wamegundua kuwa mahali ambapo bahari mbili tofauti hukutana, kuna kizuizi baina yake. Kizuizi hiki huzigawa bahari mbili hizo kiasi kwamba kila bahari huwa na joto lake, kiwango cha chumvi na msongamano.[21] Kwa mfano, maji ya bahari ya Mediterranean ni yenye uvuguvugu, yana chumvi na msongamano mdogo yakilinganishwa na maji ya bahari ya Atlantiki. Pindi maji ya Mediterranean yaingiapo Atlantiki katika kizingiti cha Gibraltar, huingia mamia kadhaa ya kilomita ndani ya Atlantiki katika kina cha kadiri ya mita 1000 yakiwa pamoja na sifa zake za uvuguvugu, kiwango uchumvi na uchache wa msongamano. Maji ya Mediterranean huimarika katika kina hiki [22] (angalia mchoro namba 13)
Chini ya bahari kuna idadi kubwa ya Viumbe kuliko huku juu, kuna milima, mabonde ya kutisha, pango na miti mirefu, pia bahari mpaka Leo hatujui wapi Yale maji yakitoka yanakwenda na yakirudi hujui wapi yatoka. Hii ni miujiza mikubwa. Bahari INA maua mazuri kuliko huku juu na viumbe wa kutisha hatari. Huenda siku nyingine ukakutana na ngombe chini ya bahari.

Kuna chunusi unaweza ukazama kwenye maji ya kwenye kifua tuu na usionekane tena hata kama ulikua unajua kuogelea. Nimambo mengi huwezi kuyamaliza.

Mshàna Jr lile tatizo language halijesha naomba unisaidie.
AMA KWELI ELIMU NI BAHARI
 
maji ya Bahari ni dawa kila maradhi wewe kama upo Dares-Salaam fanya kila mwezi uwe unakwenda kuogelea baharini hata mikosi mikosi ya mwilini mwako itakuondokea ukioga maji ya bahari yana siri kubwa sana hata waganga wa kienyeji wanayatumia maji ya bahari.
 
Chini ya bahari kuna idadi kubwa ya Viumbe kuliko huku juu, kuna milima, mabonde ya kutisha, pango na miti mirefu, pia bahari mpaka Leo hatujui wapi Yale maji yakitoka yanakwenda na yakirudi hujui wapi yatoka. Hii ni miujiza mikubwa. Bahari INA maua mazuri kuliko huku juu na viumbe wa kutisha hatari. Huenda siku nyingine ukakutana na ngombe chini ya bahari.

Kuna chunusi unaweza ukazama kwenye maji ya kwenye kifua tuu na usionekane tena hata kama ulikua unajua kuogelea. Nimambo mengi huwezi kuyamaliza.

Mshàna Jr lile tatizo language halijesha naomba unisaidie.
Tukutane dar weekend hii tutawasiliana pm
 
ASILIMIA 66 YA WAKAZI WOTE DUNIANI WANAISHI KWENYE AU KARIBU NA KINGO ZA BAHARI
 
Mshana Jr saidia hili kuuna wanaosema mtu akifia baharini au majini anaenda peponi mojamoja kwa moja. Ni imani ya dini moja Nina kapuni kwa sababu za imani za watu
 
Back
Top Bottom