Strategic relationship inatakiwa ianze mapema unapoingia miaka 30, Ila vijana wengi huwa hatuelewi namna ya kuset mikakati katika mahusiano, na hata kama tukikumbushwa huwa hatuzingatii na tunakuwa tunaendelekeza shape, sura na hali ya fedha.
Wenza wazuri wa kufanya maisha hawapatikani kwenye 40s, kwenye umri huwa unatakiwa uwe tayari una bond nzuri na mwenzako. Mtafuta mwenza kimkakati wakati upo collage ama University mnapokuja mtaani unaimarisha familia kwa kuweka pamoja mawazo yenu na kuongeza watoto.
Utakapokutana kwenye 40 mzee tunakuwa tushachafuliwa na hali mbaya mbaya nyingi, kukata tamaa na machukizo ya kisirani cha maisha. Wengi wetu tunakuwa tumeumizwa sana akili za kimapenzi zishadumaa hatuwezi kuamini na uchaguzi wetu unakua wa kujinufaisha sana.
Mwanamke anakaa kwa mwanaume kisa anastirrika, ila moyoni hana mahaba na mwenzawake. Mapenzi anayatengeneza ukiwa nawe ila ana mwenza akilini mwake anamtawala muda wote na ndio maana kesi za kutokufikishana kileleni ziko nyingi umri huo.Hisia zimekata kwa visirani tulivyopitia awali.
Hali mtaani sio shwari, changamoto za kiuchumi ni nyingi ambazo husababisha matatizo mingi ya kijamii hasa kimahusiano.
KIJANA WA 20s FANYA CHAGUO LAKO MAPEMA UKIWA UNANGUVU NA MAARIFA. KUWA MKWELI NA UPAMBANE NA USALITI MAPENZI YANAHARIBU MAARIFA YA MAISHA.