Umri wa kustaafu kwa hiari

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
9,449
16,953
Salaam aleykhum waungwana.

Juzi baada ya CAG kustaafu baada ya kipindi chake cha miaka mitano kuisha, niliona watu wengine wakisema CAG ana miaka 58 hajafikia umri hata wa kustaafu kwa hiari, kwani kustaafu kwa hiari ni miaka 62 na kwa mbinde ni miaka 65.

Hebu mlio Dar es Salaam mtujuze maana najua huko Dar ndio kuna ma profesa wa sheria, viongozi wa serkali, wasomi na wastaafu watarajiwa wengi.
 
Kwa hiari miaka 55 na zaidi
Sawa bro. Mimi niko na 57 kwa hiyo naweza kustaafu kwa hiari na kupewa bulungutu lote nivunje mifupa kama bado meno iko au ikishapita 55 ndio mpaka 60, hapa katikati 56 mpaka 59 haturuhusiwi?
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa
 
Sawa bro. Mimi niko na 57 kwa hiyo naweza kustaafu kwa hiari na kupewa bulungutu lote nivunje mifupa kama bado meno iko au ikishapita 55 ndio mpaka 60, hapa katikati 56 mpaka 59 haturuhusiwi?
Unarubusiwa ila lazima utoe taarifa ya miezi 6
 
Thanks all of you good people for your response. Mbarikiwe na muongezwe hekima
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom