Umri sahihi wa kuoa na kuolewa ni upi?

Akili Pesa

JF-Expert Member
Jun 18, 2014
616
854
Wakuu habari za muda?

Nina jambo kidogo tushirikishane maana tunatakiwa kuelezana vizur hili naamini linaweza kuamsha au kusaidia baadhi ya watu kujua ni umri upi ni sahihi kuoa na kuolewa kwa kijana, hasa tukizingatia mila za Kibantu/Kiafrika.

Maana binafsi nahsi wapo wanaooa na kuolewa bila kuzingatia umri wakati anafanya maamuzi yake hapa wengine wanawahi, yaani wanakuwa "very young" lakini wengine wanachelewa sana kufanya maamuzi, yaani wanakuwa "wakubwa plus"

Tujuzane kwa MWANAUME umri upi ni sahihi kwa kuoa? Na kwa MWANAMKE umri upi ni sahihi kwa kuolewa?

Nimeshuhudia ndoa moja hivi ya aina yake ikivunjika kwa kipindi kifupi sana ambapo mwanaume ni 38 na mwanamke ni 22, hapo nikaanza kujiuliza nani kati ya MUME NA MKE Amefanya maamuzi yasiyo sahihi. Je, ni mwanaume amechelewa au ni mwanamke amewahi?

Majibu yako yatasaidia wengi sana.

Ahsante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mambo huwa hayana formula, unaweza minya minya nyanya ukajikuta umenunua biringanya.

Hakuna umri sahihi kama ukitumia kigezo cha umri.

Maana kuna walio oana wote wakiwa under 20 na wakadumu na wengine wakaoana wakiwa na 30+ na ndoa hazikudumu.

#MWAJUMAKAOLEWA

Bagwell
 
Haya masuala ya NDOA ni mazito sana, huwezi kuyaelewa.

Wengine wanaoana, wanadumu kwenye NDOA yao mpaka kufikia Miaka kumi na mitano (15) au kumi na sita (16), na unakuta wamebahatika kupata WATOTO kwa mfano Wanne (4), au Watano (5), kisha NDOA inavunjika
 
Nadhani hakuna muda maalumu as kila mtu vile anajisikia nafsi yake inatakaje. Lakini kama unataka kupata watoto(coz wapo wasiotaka kuzaa), ni heri kuwa nao mapema.

Kwa life expectancy ya mtanzania wa kawaida, kwa uzito na ugumu wa life la sasa, kusomesha nk ni heri uzae(oa/olewa) mapema. Hiyo mapema naamini 25-35 uwe umemaliza kutafuta warithi wako.
 
Haya masuala ya NDOA ni mazito sana, huwezi kuyaelewa.

Wengine wanaoana, wanadumu kwenye NDOA yao mpaka kufikia Miaka kumi na mitano (15) au kumi na sita (16), na unakuta wamebahatika kupata WATOTO kwa mfano Wanne (4), au Watano (5), kisha NDOA inavunjika
Mkuu umenena vyema ni kweli kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pale nafsi kwa hiyari yake inapojihisi kuhitaji kuwa na majukumu ya kifamilia basi ujue umri wako wa kuoa/kuolewa umefika!
 
Kuna mambo hubadilika kutokana na muda na mitkasi za maisha (vipaumbele)...

Miaka ya nyuma watu walikuwa wanaoa nankuolewa wakiwa nanumri mdogo kwa vile walikuwa na mlolongo mfupi wa vipaumbele...

Pia kwa mathalani kwa mila za kiafrika, ilikuwa tu ukifika umri wa balehe unapelekwa jando au unyagoni tayari kwa maandilizi ya ndoa...

Lakini miaka imepita na mambo mapya yamekuja na yataendelea kuja (culture is dynamic)...

Malengo na vipaumbele vimebadilika kwa kiasi kikubwa, ndio maana kuna sheria hadi za ndoa. Umri sahihi wa mtu kuoa au kuolewa kisheria n.k (18yrs)...

Wanadamu wenyewe wamekuwa wakijiwekea malengo fulani ya msingi kabla ya kuamua kuingia ulimwengu wa kulala bila "kyupi"...

Hivyo ukitaka kujua umri sahihi, basi jibu litaegemea juu ya sheria ya mahali ulipo na asilimia ya ukamilifu wa malengo binafsi ya mtu aliyojiwekea kabla ya hatua ya ndoa...
 
Umeuliza umri sahihi wa kuoa tu na wala hukugusia jsmbo la Ndoa kudumu ama kutodumu.mimi nadhani umeuliza umri sahihi wa ndoa ambao utamfanya mwanandoa aweze kuhimili maisha ya ndoa.

Mimi naona kuwa umri sahihi wa ndoa ni kubaleghe/kuvunja ungo pamojs na Mindset ya mwanandoa.

Kijana wa kike ama wa kiume anapokuwa na mindset imara sana ya namna ya kuishi na watu mbalimbali na hasa mwenza wake na akawa na experience juu ya hilo basi nadhani hapo ni sahihi kuingia kwenye ndoa maadamu amepevuka kimwili bila kuangslia umri wake.

Kuna familia niliziona mtoto wa miaka 18 ukimuangalia mindset yake kama mtu mzima hawwzi utoto kabisa,anajiona mtu mzima kabisa kijana wa miaka 18.

Mfano tu mzazi alianza kumzoesha kijana wake kupanga matumizi ya nyumbani tokea umri wa miaka 10 akakua na jambo hilo,mtoto alikuwa anapewa pesa atunze na akawa anakua na jambo hilo,mtoto akawa anazoeshwa kuwa na jasiri na kufanya biashara mtoto akakua katika jambo hilo,mtoto anazoeshwa kuwa na maneno mazuri juu ya wajinga na kuwa na subira mtoto anafuzu hilo.

Mtoto anapewa madini ya kiutu uzima anaelewa na ubongo wake unatanuka.

Mtoto kufikia kubaleghe ansanza kupewa elimu juu ya wanawake na namna ya kuwaepuka kabisa anakua na jambo hilo.

Huyu mtoto hatokuwa sawa na mtoto wa fulani ambaye mindset yake inajengwa kuwa yeye ni mtoto tu.


Umri sahihi wa kuingia kwenye ndoa ni ule ambao umekupa uzoefu wa kuvumilia na kufahamu mambo ya kiutu uzima.

Kuna watu wanafikia miaka 30 lakini bado hawana uzoefu wala subira wala hawana ufahamu juu ya mambo makubwa ya ndoa.

Na hiyo ni kutokana na jamii kupuuza kuona kuwa ndoa ni kitu kisichohitaji kusomewa na kufundishika wakati ndoa ni jambo kama kulima na kufanya biashara,kama huna idea na nondoo mbili tatu juu ya jambo hilo utafeli.

Hivyo hakuna umri sahihi wa kuoa kama ambavyo hakuna umri sahihi wa kufungua biashara just a matter of knowledge tu juu ya jambo lako unalolitaka.

Hakuna umri sajihi wa kuoa kama ambavyo hakuna umri sahihi wa kuwa mkulima hapo ni jambo la utayari na elimu juu ya ukulima.

Kitakachokufanya udumu kwenye jambo ambalo halina kigezo cha umri kulifanya basi ni suala zima la utayari na utafiti wa kina pamoja na elimu juu ya jambo hilo ksma vile ndoa na biashara na kilimo.

Akili Pesa,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaingia kwenye ndoa bila maono ndio matokeo yake siku nikioa nitajua ama sijui pamoja na yote lazima ni OE
 
Umri sahihi wa mwanaume kuoa ni pale anapokuwa amepata a life partner ambaye anajua anataweza kumvumilia kwa yote na tayari anaweza kubeba majukumu yake Kama mme, baba na kiongozi wa familia. Vile vile, umri sahihi wa mwanamke kuolewa ni pale anapokuwa kampata mtu sahihi kwake anayejua watavumiliana katika hali zote huku yeye akiwa tayari kubeba majukumu yake Kama mke na mama wa familia pasipo muda wote, na sio tu kuolewa akifikisha umri Kati ya 23-27.
 
Haya mambo huwa hayana formula, unaweza minya minya nyanya ukajikuta umenunua biringanya.

Hakuna umri sahihi kama ukitumia kigezo cha umri.

Maana kuna walio oana wote wakiwa under 20 na wakadumu na wengine wakaoana wakiwa na 30+ na ndoa hazikudumu.

#MWAJUMAKAOLEWA

Bagwell
🤔
 
Kibailogia,tunapobalehe tu,tunakuwa tayari kuoa au kuolewa ila kufanya binadamu tuwe wastaarabu serikali zikaweka muda,mfano miaka 18 ili tukamilishe baadhi ya masuala kama ukomavu,elimu n.k. Hivyo baada ya hapo unaweza kuoa( kwa mwanamme) ilimradi uwe na uwezo wa kutoa ziada ya mambo muhimu ktk maisha kama chakula,malazi,tiba,ulinzi n.k kwa mwenzi wako na watoto Mungu akijalia
 
Back
Top Bottom