Umri katika kuoana

King Easy

Member
Aug 11, 2013
46
59
***MY OUTLOOK's***
********
*07th January,2017*

UMRI KATIKA KUOANA

*Ni kawaida kuona akina dada wengi wakiolewa na wanaume wenye umri mkubwa kuliko wao na pia kwa upane mwingine, tumekuwa tukishuhudia vijana wa Kiume wakioa wanawake wenye umri mkubwa kuliko wao hadi kuwa gumzo kwa jamii ambazo hazijazoea kuona hayo.Kwani masuala ya kuoana mara nyingi yamejikita ktk Mila na Desturi ambazo sasa zinapata challenge kubwa mno.

*Katika hali ya ukweli, Umri ni namba tu na hauna nafasi katika kukusaidia kuwa na ndoa imara (Ila Sio Chini ya Miaka 18). Wapo wanandoa wenye Umri sawa na Ndoa badi zimekalia Mabechi ya ICU ya Ndoa, pia kuna wengine umri upo sawa na wanaaendelea kujienjoy utadhani wapo Paradiso.

*Hebu Angalia lile Rika Ulilozaliwa Nalo Pale mtaani Kwenu Kama Mlikua 10 weka ratio ya 5 Wanawake na 5 Wanaume then Jiulize Wangapi Wametangulia Mbele za Haki?, Wangapi Wameozalishwa/Wameolewa/Wameoa? Wangapi Wamechumbiwa thn angalia Wangapi Mpo Single na Mnatamfuta Wachumba Wenye Umri Sawa nawe. Je Utampata Wa Umri Unaomhitaji?. Penda Unapopendwa Waswahili Husema, hawajasema Penda Kulinga na Umri.

*Ndoa inategemea kukomaa kwa Akili kwa Wahusika na Upendo wa Kweli uliopo kati yao, Awe Amekuzidi au Umemzidi au Mpo Sawa Misingi ya ndoa hajajijenga katika tofauti ya umri bali TRUE LOVE AND SATISFACTION EMOTIONALLY. Wanasema love is blind ni kweli mapenzi hayaangalii umri bali mioyo miwili iliyopendana na kuwa mmoja.

*Binafsi napendekeza kwamba umri mzuri kuoana unapatikana kwa formula ifuatayo:

Umri wa kuoana = ½ ya Umri wako + 7 (Minimum)
Umri wa kuoana = 2 x Umri wako - 7 (Maximum).

*Pia jinsi mtu anavyozidi kuongezeka umri zaidi ya miaka 50 kama unaoana naye na wewe upo chini ya miaka 25 fahamu kabisa kwamba suala la sex na kuzaa watoto uwe makini na umejiweka sawa na mmeongea mkamalizana kabla ya kuingia kwenye ndoa na mtu mwenye umri huo.

*Nisisitize kwa Kimombo “Age doesn’t matter, what matters is the real love till death do you apart”

NB: YOUR MARRIAGE ORRELTIONSHIP IS SO IMPORTANT. PLEASE TAKE GOOD CARE OF YOURSELF AND BE KIND TO YOUR PARTNER ALSO TRY KEEP YOUR SENSE OF HUMOR.
 
Back
Top Bottom