Mkuu nimefuatilia uzi wako. Nimeona unasema unaogopa kurudi mtaani bila mwanamke ambaye una malengo naye. Kwa ushauri wangu sio lazima umpate mwanamke chuoni. Ukiwa chuoni unakuwa na mtazamo finyu juu ya mahusiano, pia mapenzi ya chuo hayana uhalisia na maisha wengi wanadanganyana kwa kuwa hawajui nini kitatokea baada ya kumaliza chuo. Wasichana wengi wanapokuwa chuo hudhani kuwa wao ni malkia, wanazurura na huyu na yule ki ufupi hawana msimamo. Hivyo kama unadhani ni lazima utoke na mchumba chuoni unakosea. Maliza chuo, tafuta michongo ya kueleweka, wanawake wapo wengi mtaani, using'ang'anie chuoni. Usiige, mapenzi ya dhati yanahitaji subira na uvumilivu. Usikomae ukipata degree basi upate na mchumba simultaneously utaumia