Umri gani ni sahihi kumtenganisha mtoto na chumba cha wazazi?

Hahahaha umenikumbusha mdada mmoja alimwambia mwanae akalale mtoto akajibu ahaaa mnataka nikalale muanze uchafu wenu eeh, ss mtt wa miaka 5 kajuaje km huo ni uchafu au lah, akianza tu kuongea ahamishwe lah sivyo majanga.
 
Hahahaha umenikumbusha mdada mmoja alimwambia mwanae akalale mtoto akajibu ahaaa mnataka nikalale muanze uchafu wenu eeh, ss mtt wa miaka 5 kajuaje km huo ni uchafu au lah, akianza tu kuongea ahamishwe lah sivyo majanga.

duuh! i cant imagine alijisikiaje huyo dada
 
...si kwa wanandoa peke yao.
Bali changamoto hii hutukumba hata sie tulio single parent.

Mwanangu aliniambia kbs kuwa mkimlaza chumba cha peke yake atalia usiku kucha, na pia sipendi alale na dada wa kazi wala kaka wa kazi.
Inabidi nimchukue nilale nae.
Ukiongea na simu...atataka akuulize maswali kwa yale yote uliyoongea.
Ukifungua laptop atataka achungulie na maswali juu.
Nikitoka out usiku...halali mpaka nirudi, huku maswali yakinisubiri.
Ndio maana tunaamua kupeleka watoto wetu Boarding Schools...si kwa kupenda bali kwa kadhia na usumbufu kama huo.

Ila kwa walioko ndoani, i mean pair, nadhani umri mzuri wa kumtengea mtoto chumba chake ni kuanzia miezi 9 mpaka mwaka na nusu...ili awe amekomaa kiakili kidogo.
 
View attachment 117547View attachment 117548
KUTOKA NYUMBA YA JIRANI!! Baba anacheki TV, mtoto wake miaka 3 miezi 4 (cha kiume) alikua anarukaruka kwenye sofa wakati mama yake anafanya usafi ghafla mtoto akalala kwa mgongo kaanza kukata kiuno akaanza kumuita mama yake aje amkalie!! Mama kaanza kumtandika fagio za kutosha, Baba kashindwa kuvumilia ikabidi aangue kicheko nae kalimwa fagio akajiondokea.
Ni umri gani mtoto asiendelee kulala na wazazi??? au tuige mfano wa kule kijijini Baba na Mama kuwa na vyumba tofauti wakishapata watoto??
duuuh yaleo kali!kwakweli huu uzao wa kikwete unapevuka haraka sana,kwa upande wangu naona miaka miwili inatosha kwa mtoto kulala na wazazi,kuna mfanya kazi mwenzangu huwa bado analalaga nawanae wawili (pacha)wanamiaka mitatu,sasa sikumoja wakati anakula tunda akijua kwamba watoto washalala ghafla yule wakiume akaanza kumpiga baba ake makalio huku akilia kwanguvu akimuambia baba muache mama,baba muache mama!kitu ambacho sio kizuri
 
Jamieni enzi hizi hakuna mtoto ukita mtoto asikopi n.a. Kwanza kuiga munapo gegedana basi akifika miezi miwili tu muhamishe chumbani kwake k
 
Dawa ni kumtengenezea cage tu! wtoto wa siku hzi wamezaliwa wanasema mtu mzima huchelewi kuumbuka
 
Pindi anapoacha kunyonya usiku...maana wamama wengi (mimi mmoja wapo) ni wavivu kuamka kwenda chumba kingine kunyoyesha mtoto.
 
KUTOKA MAARIFA YA JAMII - TUSAIDIANE.
clip_image002_thumb%25255B2%25255D.jpg




Wazazi wengi kupenda kulala na watoto wao katika Chumba kimoja bila kujali umri wa mtoto huyo kuwa unamfaa kuendelea kulala humo tangu azaliwe au la¡-

Hili jambo linatokea sana katika familia zetu za kiswahili hasa kwa wale ambao hawana kipato kikubwa cha kuweza kuandaa chumba maalum kwa ajili ya mtoto huamua kuweka kitanda kidogo ndani ya chumba cha baba na mama na kumtunza mtoto huyo humo hadi pale wazazi hao watakapoona inafaa kumuacha kulala peke yake au na Dada, Kaka zake.

Hapo Ndipo kwenye Shida kwani kuna wengine tunawaona mtoto ameshaanza darasa la kwanza lakini bado analala chumba cha Baba na mama ukitazama umri wa mtoto huyo ni Kuanzia Miaka 7 na Kuendelea ambaye kwa watoto wa siku hizi tayari ameshatambua zuri na baya..

Nakama tujuavyo chumbani kuna mengi hufanyika ambayo Mtoto hapaswi kuona katika kipindi hicho cha umri huo.

Kwenu Wadau...
 
Inategemea na uwezo wa familia ila ni vizuri mtoto akatoka chumbani kwa wazazi akifikisha miaka miwili.
Kama uwezo hauruhusu mnalala nae tu ila ratiba inabidi ibadilike sasa,No kujiachia tena!!!!
 
kwahyo na ww unaunga mkono suala la kulala naye?? Hapo ni kujipanga mapema kabla hujapata mtoto. Jitahidi akifikisha miaka miwili aanze kulala peke yake. Ili asije kukung'ang'ania sku moja

Well said mkuu, mtoto ukitaka upende malezi yake akiwa na kama miezi sita hivi (anakula chakula chochote na keshajua usiku ni kulala tu) unafanya kumzoesha kulala vyumba tofauti tofauti na watu tofauti ili kuzea hiyo hali. Kikubwa uwe makini na usalama wa mtoto, awe na kitanda kinachohama kwa usalama zaidi ili alale kitanda chake chumba chochote.

Tatizo Waafrika wengi huwa tuna desturi kuwa ukifanya maandalizi ya ujauzito na maandalizi ya mtoto anayekuja wanachukulia kuwa ni uchuro!! Ukinunua vitu vya maandalizi wanaishia "kukuuliza akifa je?" na hali hii inafanya tusiwe na tabia ya kufanya planning ya ujauzito wa mtoto/watoto wanaotarajiwa kutafutwa na kuzaliwa!! Hatimae utakuta hali inafika kuwa mbaya kwa familia, watoto watatu hadi wanne tena wa jinsia tofauti wanashea chumba kimoja na wazazi.

Lakini mambo huwa ni rahisi pale mnapoanza kuishi pamoja mkajadili kwanza kabla ya kubeba mimba juu ya huduma za huo ujauzito na hata mtoto ajae kuwa atakula nini, atalala wapi, atavaa nini na atacheza mazingira yepi!!
 
Mkuu inategemea na maisha yako,kama unaishi uswazi umepanga chumba kimoja ukisema umtenge labda alale kwa jirani,ila kama mambo safi akifikisha mwezi mmoja tu anakua na kitanda chake kidogo ila kinakua jiran na kitanda chenu ili mama akiamka usiku ni kunyonyesha na kumrudisha kwenye kitanda chake ili asizoee kulala na wazazi.
 
Back
Top Bottom