beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Umoja wa Ulaya(EU) umekataa ombi la [HASHTAG]#EAC[/HASHTAG] la kuiondolea vikwazo Burundi, yasema vikwazo vitaendelea hadi hali ya kisiasa itakapobadilika nchini humo.
Juzi katika mkutano wa kukabidhiana uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC uliofanyika jijini Dar es Salaam, Rais Museveni wa Uganda na Rais Magufuli waliutaka Umoja wa Ulaya ufute vikwazo ulivyoiwekea Burundi.
Mgogoro mkubwa wa kisiasa umeikumba Burundi tangu Rais Pierre Nkurunziza alipoamua kugombea tena urais kwa mara ya tatu mfululizo huku wapinzani wakisema kuwa huo ulikuwa ni ukiukwaji wa wazi wa makubaliano ya Arusha, Tanzania, yaliyomaliza vita vya ndani nchini Burundi.