Umoja wa Mataifa watoa ripoti ya Congo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umoja wa Mataifa watoa ripoti ya Congo

Discussion in 'International Forum' started by jamadari, Oct 3, 2010.

 1. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [​IMG]Wakimbizi kutoka Rwanda wakipita Zaire


  Umoja wa Mataifa unatarajia kuchapisha ripoti yenye utata juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika miaka ya 90.
  Lugha iliyotumika kwenye nakala ya mwisho inaaminiwa kupunguzwa makali baada ya ile iliyotolewa awali bila kutarajiwa kuibua hasira kutoka nchi za Uganda na Rwanda.
  Nchi zote mbili zilishutumiwa kwa kuhusika na uhalifu wa kivita dhidi ya Wahutu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa ghasia hizo.
  Walitishia kuondoa majeshi yao ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.
  Ripoti hiyo inayohusu mgogoro kati ya mwaka 1993 na 2003 inaaminiwa kuwa na maelezo ya uhalifu ambayo hayakuwahi kuandikwa hapo awali.
  Imezungumzia matukio takriban 600 ikiwemo madai ya mauaji ya raia, utesaji, na uharibifu wa miundo mbinu iliyosababisha vifo vya raia.
  Rwanda ilihamaki sana juu ya madai kuwa jeshi lake linaloongozwa na Watutsi huenda lilihusika na mauaji ya kimbari huko Congo, wakati huo ikijulikana kama Zaire mpaka mwaka 1997, dhidi ya Wahutu kutoka Rwanda.
  Waandishi wanasema madai ya mauaji ya kimbari dhidi ya serikali ya Rwanda ya sasa, inayoongozwa na Rais Paul Kagame, ni suala tete, kwani anajiwakilisha kama mtu aliyeweza kuyamaliza mauaji hayo ya Watutsi wenzake na Wahutu wenye msimamo wa kati mwaka 1994.
  Baadhi ya wapiganaji wanaohusishwa na mauaji hayo walikimbilia Zaire.
  Lakini ripoti ya Umoja wa Mataifa inawashutumu kwa kuwaua maelfu ya raia wa Kihutu, waliokimbia na wapiganaji hao.


  chanzo: BBC Swahili - Habari - Umoja wa Mataifa watoa ripoti ya Congo
  mimi huwa najiuliza kisha huwa sipati jibu, kwanini Tanzania haisaidii kuweka amani kwa majirani zake hususana Jamhuri ya watu wa Congo? huwa najiuliza kila siku huwa sipati jibu kamili au Tanzania inangojea mpakaiamrishwe na Marekani ndio Tanzania yaweza kwenda Jamhuri ya watu wa Congo kuweka amani?
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ripoti inasema Kagame kwenye miaka ya kati ya 1990 aliongoza jeshi hilo lililofanya mauaji ya Wahutu hao Zaire.
   
Loading...