Umoja wa Mataifa wamsifu Rais Magufuli

BabuK

JF-Expert Member
Jul 30, 2008
1,845
329
alvaro-rodriguez_210_120.jpg

SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limeeleza kuridhishwa kwake na utendaji wa Rais John Magufuli katika mapambano ya rushwa, kuongeza uwajibikaji na ukusanyaji wa mapato.

Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro Rodriguez, alisema hayo jana katika semina ya wabunge kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikipambana na rushwa na kusimamia kwa karibu ukusanyaji mapato, hali aliyosema itasaidia maendeleo kwa kuwa hakuna nchi iliyoendelea bila kuchapakazi.

Rodriguez alisema mbali na kuona maendeleo katika baadhi ya mikoa na mitaa, ameona jitihada hizo za Serikali na amefurahishwa na kuridhika nazo.

Mwakilishi huyo pia alisema Serikali ya Tanzania na Ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN), zimekuwa zikifanya kazi pamoja katika harakati za usambazaji wa malengo ya dunia kwa Watanzania.

Alisisitiza umuhimu wa malengo hayo kueleweka kwa wabunge, ili katika jukumu lao la kuisimamia Serikali, wawe mabalozi wa utekelezaji wa malengo hayo katika ufuatiliaji kwenye ngazi zote za utawala.

Awali akifungua semina hiyo, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson aliwataka wabunge kuoanisha malengo hayo na malengo ya Dira ya Taifa ya 2025 pamoja na malengo ya Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano wa 2016/2017 mpaka 2020/2021 ambao ulishafikishwa bungeni.

Dk Tulia aliwataka wabunge kila mmoja kuyaelewa vizuri malengo hayo ili kila mmoja ashikilie mahali atakapofuatilia Serikalini wakati wa utekelezaji wake.

Miongoni mwa malengo hayo ni pamoja na kutokomeza umasikini wa kila aina, kufuta njaa kwa kuhakikisha kuna kuwa na uhakika wa chakula bora kwakuboresha kilimo endelevu, kuhakikisha watu wote wanakuwa na afya bora nakupata huduma za afya na kupunguza utofauti wa kipato.

Akitoa mada katika semina hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Paul Kessy, alisema Tanzania imeshiriki kwa kiasi kikubwa katika maandalizi ya malengo hayo na hivyo mchango wake kuwa sehemu ya maudhui ya malengo hayo endelevu kwa maslahi mapana ya taifa na watu wake.

Kwa mujibu wa Kessy, sehemu ya mchango wa Tanzania katika kuunda malengo hayo, ilikuwa ni kutaka malengo hayo yahakikishe kuwa baadhi ya masuala ambayo hayakukamilika katika utekelezaji wa Malengo ya Milenia yanazingatiwa katika malengo endelevu.

Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na kupunguza umasikini, upatikanaji wa ajira na kukuza uwezo wa nchi masikini hasa katika maendeleo ya teknolojia.

Chanzo: HabariLeo
 
Mimi nafikiri hii habari ingekuwa na heading inayoakisi hiyo semina ya hoja 17 za maendeleo endelevu ya dunia.
Lengo la semina halikuwa kumsifia mfalme.
Ila kwakuwa mfalme wetu ni mtakatifu na anastahili sifa na utukufu na kwakuwa mwandishi anaongozwa na njaa na mbinu aliyobakiza ni kujikomba, basi sawa.
Ila ushauri wangu, mwandishi kataa njaa, iamini taaluma yako.
 
Wakati jpm akisifiwa na mwakilishi wa undp nchini kwa kupambana na rushwa na kuongeza uwajibikaji ni aibu kwa mbowe eti akiongozana na wale wakimbizi wa ccm lowassa na sumaye kuazimia kuzunguka nchi nzima kumpinga.

chadema na ukawa baada ya kuwakaribisha waliokua wanaonekana mafisadi na ccm sasa wanaimba mapambio kuwasifu hao makapi na wamekua wanapinga juhudi za kupambana na ufisadi na kuleta uwajibikaji kwa kisingizio cha kutetea demokrasia.

huwezi kuruhusu makosa kama uwepo wa wafanyakazi hewa wanafunzi hewa vyeti hewa etc eti kwa kua uongozi ulikua wapi makosa yakitendeka. wanataka mafisadi na ufisadi kuachwa wafaidi matunda ya ufisadi au makosa ya uongozi wa nyuma. kama watu walipora ardhi ya wananchi basi waachwe.

kama mtu alitumia madaraka kuiba basi aachwe afaidi dhuluma. ni rahisi kuona hiyo falsafa kwa kuangalia makapi ya ccm na wafuasi wao waliohamia cdm na jinsi walivyoenda na kupokewa cdm na ukawa.
 
Ww ni mtu mkatili kabisa tena sio mtanzania mzalendo au kwasababu sio watoto wako kwahiyo magufuli hao sio wananchi wake
 
Jesca alifika vipi chuo kikuu kama hakukuwa na mazingira ya rushwa?
 
SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limeeleza kuridhishwa kwake na utendaji wa Rais John Magufuli katika mapambano ya rushwa, kuongeza uwajibikaji na ukusanyaji wa mapato.

Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro Rodriguez, alisema hayo jana katika semina ya wabunge kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikipambana na rushwa na kusimamia kwa karibu ukusanyaji mapato, hali aliyosema itasaidia maendeleo kwa kuwa hakuna nchi iliyoendelea bila kuchapakazi.

Rodriguez alisema mbali na kuona maendeleo katika baadhi ya mikoa na mitaa, ameona jitihada hizo za Serikali na amefurahishwa na kuridhika nazo.

Mwakilishi huyo pia alisema Serikali ya Tanzania na Ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN), zimekuwa zikifanya kazi pamoja katika harakati za usambazaji wa malengo ya dunia kwa Watanzania.

Alisisitiza umuhimu wa malengo hayo kueleweka kwa wabunge, ili katika jukumu lao la kuisimamia Serikali, wawe mabalozi wa utekelezaji wa malengo hayo katika ufuatiliaji kwenye ngazi zote za utawala.

Awali akifungua semina hiyo, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson aliwataka wabunge kuoanisha malengo hayo na malengo ya Dira ya Taifa ya 2025 pamoja na malengo ya Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano wa 2016/2017 mpaka 2020/2021 ambao ulishafikishwa bungeni.

Dk Tulia aliwataka wabunge kila mmoja kuyaelewa vizuri malengo hayo ili kila mmoja ashikilie mahali atakapofuatilia Serikalini wakati wa utekelezaji wake.

Miongoni mwa malengo hayo ni pamoja na kutokomeza umasikini wa kila aina, kufuta njaa kwa kuhakikisha kuna kuwa na uhakika wa chakula bora kwakuboresha kilimo endelevu, kuhakikisha watu wote wanakuwa na afya bora nakupata huduma za afya na kupunguza utofauti wa kipato.

Akitoa mada katika semina hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Paul Kessy, alisema Tanzania imeshiriki kwa kiasi kikubwa katika maandalizi ya malengo hayo na hivyo mchango wake kuwa sehemu ya maudhui ya malengo hayo endelevu kwa maslahi mapana ya taifa na watu wake.

Kwa mujibu wa Kessy, sehemu ya mchango wa Tanzania katika kuunda malengo hayo, ilikuwa ni kutaka malengo hayo yahakikishe kuwa baadhi ya masuala ambayo hayakukamilika katika utekelezaji wa Malengo ya Milenia yanazingatiwa katika malengo endelevu.

Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na kupunguza umasikini, upatikanaji wa ajira na kukuza uwezo wa nchi masikini hasa katika maendeleo ya teknolojia.

Habari Leo
 
Haya sasa mnapenda kusifiwa na wazungu ila walipokata misaada ya MCC mliwatukana humu. Ama kweli mtu mweusi mwache alivyo tu
 
Back
Top Bottom