Wana Jamvi,
Kuna hii tabia ya madereva wa pikipiki almaarufu kama Bodaboda ambao hutumika au hufanyakazi pale mmoja wao anapopata tatizo. Japo sina tatizo na umoja wao huo kutokana na matukio ya kikatili wanayofanyiwa na waporaji wa pikipiki zao lakini kwa bahati mbaya sasa umoja huu hufanya vurugu, hupiga huumiza na pengine kuua kwa kisingizio kuwa mmoja wao amegongwa, hata kama aliyegongwa alifanya makosa yeye.
Nimeshashuhudia pale Sinza Mori mmoja wao aligongwa na wakapiagiana simu, wakafika vijana wengi sana na pikipiki zao wakaanzisha vurugu, kule tegeta imesharipotiwa pia ambapo walifanya vurugu na kusababisha gari kuchomwa moto, Ubungo vivyo hivyo na juzi niliwakuta pale maeneo ya manzese-bgi brother. Yawezekana kuna matukio mengi zaidi ya haya pia
Angalizo langu; vijana hawa wapatiwe elimu sahihi ya udereva vinginevyo watakuja kusababisha tatizo kubwa zaidi la umwagaji damu kwa watu ambao hawana tatizo.
Na nyinyi wenye magari kwa nini muwagonge waendesha pikipiki? Kisa hajui sheria tu? Adhabu yake agongwe/ auwawe? Ninyi wenye magari na munaozijua sheria za barabarani basi ongezeni uangalifu mnapokuwa kwenye vyombo vyenu vya moto mkijua kwamba mwendesha pikipiki yeye mwenyewe ni bodi. Ukimgonga unamuua au unampa kilema cha maisha akipona. Kukosea kwao sheria siyo kibali cha ninyi kuwakanyaga. Bado mwaweza kuepusha shari kama mtakuwa waangalifu. Nje ya hapo mtawaua wengi.
Arusha hii pia ilitokea.moroco jana wamechoma BMW
Kuna siku jamaa wa bodaboda alijibamiza kwenye gari yangu na pikipiki yake ikaanguka na kuvunjika side mirrors. Niliposhuka kuangalia iwapo ameharibu gari yangu (bahati nzuri alijibamiza kwenye ngao), nikajikuta nimezungukwa na pikipiki kibao huku wakijaribu kunitisha. Nikawaambia wamuulize mwenzao iwapo nimemgonga au amejibamiza mwenyewe. Waliponisogelea zaidi kwa shari nilichomoa 'mguu wa kuku' kiunoni, wakatawanyika, nami nikawasha gari yangu na kuondoka. Kama alivyodokeza mkuu mwingine hapo juu, mara nyingi hawajali kama wao ndio wenye makosa au la. Sasa hivi hizi bodaboda ni chanzo kimojawapo cha ajali za barabarani. Vijana wengi wanajifunza kuendesha asubuhi na jioni wanabeba abiria. Wengi wao hawajui kabisa sheria za barabaranii.

Yaaaanii nashindwa hata kuelezea sijui tufanye nini, naona bora usafiri wa bodaboda upigwe marufuku mara moja maana hili limeshakuwa tatizo! afadhali hata jamaa wa bajaj