Kinuju
JF-Expert Member
- Mar 20, 2021
- 2,390
- 5,310
Waziri wa Tamisemi mh Ummy Mwalimu amesema wizara ya Tamisemi inamtesa na kumnyima usingizi kwa mambo mawili.
La kwanza ni wimbi la watumishi kuhama kutoka vijijini kwenda kwenye majiji na manispaa.
Watumishi wengi sasa hawataki kufanya kazi vijijini hali hii imepelekea wananchi wa vijijini kukosa huduma.
La pili ni uzalishwaji wa madeni ya wazabuni bila utaratibu na madiwani kukaa kimya hadi madeni hayo yanakuwa makubwa na kuwa mzigo mkubwa kwa serikali.
=========
Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu leo Ijumaa Oktoba 28, 2021 ametaja mambo makubwa mawili ambayo amesema yanamkera akiwa kwenye nafasi yake ndani ya Wizara hiyo, akisema hawezi kuyavulimia yaendelee.
Miongoni mwa mambo hayo ni uhamisho wa watumishi walio chini ya ofisi ya Tamisemi ambao wanaomba kuhama kutoka halmashauri za vijijini na kukimbilia kwenye majiji na manispaa ambao amesitisha hadi atakapotangaza tena.
Amesema uhamisho kwa watumishi wanaoomba kuhama kutoka halmashauri za majiji kwenda wilayani au maeneo mengine ya vijijini, agizo hilo haliwahusu bali wao wanaweza kuhamishwa.
Waziri Ummy amemuagiza Katibu Mkuu Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe kuwa “Kuanzia leo ni marufuku na sitaki kusikia kuhusu uhamisho wa mtu kutoka vijijini kwenda mjini hasa katika majiji na manispaa, ila kama wanatoka huko kwenda halmashauri za vijiji waharakashiwe uhamisho wao ili waende.
Waziri Ummy ametaja jambo la pili linalomchukiza kuwa ni madeni ya wazabuni ambayo huzalishwa bila mpangilio.
“Utakuta halmashauri inatoa tenda ya kujenga kitu fulani na wakati huo huo inashindwa kumlipa mzabuni na kufanya deni liendelee kukua, hivi mkurugenzi na baraza la madiwani hamlioni hilo, yani inanikera hasa,” amesema Ummy.
Amebainisha kuwa mambo hayo yanamkera na kumnyima usingizi ndani ya Tamisemi lakini anaendelea kupambana nayo siku hadi siku akiamini wenzake watamuelewa.
Katka taarifa yake Waziri amezungumzia changamoto ya ucheleweshaji wa taarifa za Tamisemi kwamba kunatokana na mfumo lakini kwa baadhi ya maeneo inachangiwa na uzembe wa baadhi ya watumishi.
Ametoa agizo kwa vikao vya mabaraza ya madiwani kutoketi badala yake watakuwa wanangoja taarifa ya Tamisemi ndipo watakutana kwa ajili ya kujadili pamoja na mambo mengine taarifa za Wizara na kujilinganisha na wenzao wengine.
Mwananchi