Ummy Mwalimu ataja yanayomtesa Wizara ya TAMISEMI

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Waziri wa Tamisemi mh Ummy Mwalimu amesema wizara ya Tamisemi inamtesa na kumnyima usingizi kwa mambo mawili.

La kwanza ni wimbi la watumishi kuhama kutoka vijijini kwenda kwenye majiji na manispaa.

Watumishi wengi sasa hawataki kufanya kazi vijijini hali hii imepelekea wananchi wa vijijini kukosa huduma.

La pili ni uzalishwaji wa madeni ya wazabuni bila utaratibu na madiwani kukaa kimya hadi madeni hayo yanakuwa makubwa na kuwa mzigo mkubwa kwa serikali.
=========

Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu leo Ijumaa Oktoba 28, 2021 ametaja mambo makubwa mawili ambayo amesema yanamkera akiwa kwenye nafasi yake ndani ya Wizara hiyo, akisema hawezi kuyavulimia yaendelee.

Miongoni mwa mambo hayo ni uhamisho wa watumishi walio chini ya ofisi ya Tamisemi ambao wanaomba kuhama kutoka halmashauri za vijijini na kukimbilia kwenye majiji na manispaa ambao amesitisha hadi atakapotangaza tena.

Amesema uhamisho kwa watumishi wanaoomba kuhama kutoka halmashauri za majiji kwenda wilayani au maeneo mengine ya vijijini, agizo hilo haliwahusu bali wao wanaweza kuhamishwa.

Waziri Ummy amemuagiza Katibu Mkuu Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe kuwa “Kuanzia leo ni marufuku na sitaki kusikia kuhusu uhamisho wa mtu kutoka vijijini kwenda mjini hasa katika majiji na manispaa, ila kama wanatoka huko kwenda halmashauri za vijiji waharakashiwe uhamisho wao ili waende.

Waziri Ummy ametaja jambo la pili linalomchukiza kuwa ni madeni ya wazabuni ambayo huzalishwa bila mpangilio.

“Utakuta halmashauri inatoa tenda ya kujenga kitu fulani na wakati huo huo inashindwa kumlipa mzabuni na kufanya deni liendelee kukua, hivi mkurugenzi na baraza la madiwani hamlioni hilo, yani inanikera hasa,” amesema Ummy.

Amebainisha kuwa mambo hayo yanamkera na kumnyima usingizi ndani ya Tamisemi lakini anaendelea kupambana nayo siku hadi siku akiamini wenzake watamuelewa.

Katka taarifa yake Waziri amezungumzia changamoto ya ucheleweshaji wa taarifa za Tamisemi kwamba kunatokana na mfumo lakini kwa baadhi ya maeneo inachangiwa na uzembe wa baadhi ya watumishi.

Ametoa agizo kwa vikao vya mabaraza ya madiwani kutoketi badala yake watakuwa wanangoja taarifa ya Tamisemi ndipo watakutana kwa ajili ya kujadili pamoja na mambo mengine taarifa za Wizara na kujilinganisha na wenzao wengine.

Mwananchi
 
Kumbe ata yeye kuna mda hanakuwa mvivu wakufikiri kiasi hiki!?

Kwann watumishi wanahama kutoka vijijini kuja kwenye majiji?

Kama wasipo hama jua wapo watakao acha kazi. Mazingira ya vijijini sio rafiki kwa watumishi wengi hasa wa kike ili jambo liangaliwe lasi hvyo wataangaika kumtafta mchawi wakati wanamfunga wenyewe
 
Naona analewa madaraka huyu mama, inamaana watu wasifuate familia zao? Yani watu waendelee kuchepuka kisa mke yuko mbali? Huu ni ulevi wa madaraka.

Ummy Mwalimu anapwaya kama waziri sio wa TAMISEMI tu bali hata alipokuwa Wizara ya Afya!! Jiwe kabla hajafa alisha muwashia taa nyekundu; kwani asingetwaliwa saa hizi huo uwaziri angeusikia kwenye TBC

Alikuwa na Samia Tanga pale mwendazake alipotwaliwa hivyo wakawa karibu sana wakati wa purukushani ya ile transition, hivyo Samia alipoapishwa ilimbidi amlipe fadhila kwa kumpa uWaziri wa TAMISEMI

Hiyo ni Wizara strategic inahitaji mtu mathubuti na sio mtu wa longolongo , hivyo kuna umuhimu kwa kufikiria upya nani atamsaidia Rais kwenye Wizara hii. Time is the essence ,muda sio rafiki.
 
Kosa la Waziri ni nini?
 
Inafikirisha sana, hao watumishi wanaojaa mijini ni aidha watoto wa wakubwa, wake zao, wana familia na pia wale wanaotoa miili yao (wakike) kwa wakubwa. Wasiokuwa na connection ndio hupangiwa vijijini.
Ajitokeze mtu hapa ambaye amekwisha muona mtoto wa mkubwa yeyote ambaye Ni mtumishi wa serikali wa kada yoyote aliyewahi kupangiwa kijijini.
Ummy mwenyewe ataje mtu wa familia yake anayefanya kazi kijijini.
Watoto wa masikini wanaendelea kuonewa tu.
 
Ummy bila shaka upo humu, maafisa utumishi wamegoma kupandisha watumishi madaraja pamoja na Mama Samia kuwataka wafanye hivyo! Yaani nikae kijijini na mshahara kiduchu pamoja na maisha magumu? Bora njie mjini nifungue hata grocery, au nipige part time kwenye shule binafsi!
Nchi ngumu sana hii!
 
Huko vijijini pangeni zaidi walimu wa kiume, wanawake siyo wastahimilivu kwenye mazingira magumu........kuhusu madeni ya wazabuni hakuna namna ni kulipa tu maana wameshasambaza huduma hiyo.
 
mm ni mhasibu wa hamlashauri naenda kumfuata mke kijijini halafu huko nitafanya kazi gani.au mm ni daktari bingwa naenda kijijini ati kumfuata mke wange je huko kuna huduma za kibingwa?
Kwa hiyo watu wa kijijini hawahitaji kuhudumiwa na daktari bingwa?
 
Ummy bila shaka upo humu, maafisa utumishi wamegoma kupandisha watumishi madaraja pamoja na Mama Samia kuwataka wafanye hivyo! Yaani nikae kijijini na mshahara kiduchu pamoja na maisha magumu? Bora njie mjini nifungue hata grocery, au nipige part time kwenye shule binafsi!
Nchi ngumu sana hii!
Acha kazi
 
mwalimu tena ndio imepigwa pini kabisa.na dokezo lako atupitish
 
Yeye kama anaona ni rahisi na raha kuishi kijijini, ajiuzulu hiyo nafasi yake ya uwaziri na ikiwezekana na huo ubunge wake wa kupewa! Halafu aje kufanya kazi huku Magamba Lushoto.

Au ndiyo kusema kwenye hii nchi kuna binadamu wengine wana haki ya kuishi Mjini, na wengine vijijini?
 
Back
Top Bottom