Umilikishaji Silaha ki holela serikali inajichimbia kaburi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umilikishaji Silaha ki holela serikali inajichimbia kaburi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rungwe, Nov 3, 2011.

 1. rungwe

  rungwe Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h]

  [​IMG]
  Jeshi la polisi la jiji la New York (NYPD) liko katika wakati mgumu sana wa kupambana na makundi ya wahalifu (organized crime) hususan waporaji wa mabenki, wafanya biashara ya madawa ya kulevya na wahuni wengine (thugs) ambao wanamiliki silaha nyingi za kivita.

  Baadhi ya silaha hizo kama bunduki aina ya AK 47, Israel Uzi gun na bastola za kariba mbalimbali si kwamba ziliingizwa Marekani kwa magendo au kinyume cha sheria, bali zilinunuliwa ki halali katika maduka kedekede ya silaha yaliyo zagaa katika Marekani yote.

  [​IMG]Ni jambo la kushangaza kidogo kwamba katika majimbo mengi ya Marekani, ni rahisi zaidi kununua silaha (bunduki, bastola, au risasi) kuliko kununua paketi ya sigara. Hii inatokana na ukweli kwamba kumiliki silaha ni haki ya kila mwananchi ki katiba. Marekebisho ya pili ya katiba ya Marekani (second ammendment) yanampa kila raia (asiye na rekodi ya uhalifu) haki ya kumiliki na kubeba silaha (rights to bare arms). Aidha Wamarekani wanaamini kwamba magonjwa yanayotokana na uvutaji silaha kama saratani ya koho (Bronchitis) na magonjwa ya moyo (Heart desease) yanaua watu wengi zaidi kuliko wale wanao uawa kwa bunduki.


  Hata hivyo, katika siku za karibuni majimbo (states) mengi yameanza kuangalia upya utaratibu wa utoaji leseni za kumiliki silaha (kwa kuwachuja zaidi waombaji) baada ya kubaini ongezeko kubwa la wahalifu wanaojijengea himaya ambazo inawawia vigumu hata polisi kuzivunja. Ni sababu hiyo iliyo wafanya polisi wa New York (NYPD) wakishirikiana na kikosi maalumu cha Alcohol Tobaco and Firearms (ATF) kulivalia njuga suala la silaha zilizoko mitaani.


  
  [TABLE="class: tr-caption-container"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Afisa wa Polisi akikagua silaha iliyokamatwa[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  
  Katika nchi yetu jeshi la polisi hususan idara yake ya upelelezi wa makosa ya jinai (CID) ndio yenye jukumu la kutoa vibali vya kumiliki silaha. Hata hivyo idara hiyo haikamilishi taratibu zote peke yake bali huhusisha kamati tendaji za ulinzi na usalama za mitaa, wilaya, na mikoa katika kuwachuja waombaji wa leseni za kumiliki silaha, kuwaondoa wale wasiofaa na kuidhinisha wale wanaonekana kutimiza sifa za umiliki.


  Hata hivyo katika siku za karibuni vijana wengi wasio na sifa zinazo stahili kumiliki silaha wamekuwa wakionekana katika mabenki, arusi, viwanja vya mipira na hata vilabu vya usiku wakiwa wamebeba bastola. Wengi wa vijana hawa huzitumia silaha hizo kuwatishia watu wanao gombana nao, na au kuwafanya raia wengine wawaogope kwa kuwadhania kuwa nao ni ma askari.


  Hatuna hakika ni wangapi kati ya vijana hawa ambao huzitumia silaha hizo kwa uporaji, au kuwakodisha majambazi. Tatizo ni kwamba wengi wa vijana hawawanazo leseni halali za kumiliki silaha ambazo wamezipata baada ya kumwaga mapesa kwa wahusika na hivyo wanapo kutwa na polisi wakiwa wamebeba silaha hizo huwa hawana tatizo.


  [​IMG]Ndipo tunapohoji utaratibu mzima wa utoaji wa leseni za silaha. Utaratibu ambao unaonekana kuwa mzuri ki nadharia lakini umegubikwa na rushwa na hivyo kutozingatia uwezo na ulazima wa muombaji kupewa silaha. Aidha, ongezeko kubwa la vijana wanaobeba silaha mtaani linatupa picha kuwa serikali haishituki wala haioni hatali ya kuwapa raia silaha nyingi wakati haina uwezo wa kuwadhibiti. Wale waliopitia JKT watakumbuka kuwa wakati ule askari mmoja akipoteza risasi moja, kombaniya nzima ililazimika kuitafuta hadi kuipata kwani makamanda wanaamini kuwa bunduki moja na risasi moja inaweza kuteka kikosi kizima na hata kuangusha serikali.


  [TABLE="class: tr-caption-container"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]40 Smith & Wesson[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Upo uwezekano mkubwa kwamba kutokana na hali ngumu ya maisha inayo endelea kukua siku baada ya siku baadhi ya silaha zilizo tolewa ki halali zikatumika kufanya uhalifu kama inavyotokea Marekani. Aidha siku wananchi watakapo amua kufanya maandamano ya kweli kupinga serikali kama inavyo endelea kutokea katika nchi nyingine nyingi duniani, silaha hizi zinaweza kutumika kupambana na ma askari na
  hivyo kuifanya serikali kuingiza vifaru mitaani kama ilivyo tokea Libya na inavyoendelea kutokea Syria.


  Wakati wenzetu (NYPD) wenye nyenzo za hali ya juu na uwezo mkubwa wa kifedha wanahangaika kupunguza silaha mitaani, ni aibu kwetu sie tunao jitahidi kuongeza silaha mitaani. Ni vema viongozi wetu wakajifunza kwamba dawa ya kupunguza uhalifu ni kuimarisha jeshi la polisi na kuboresha hali ya maisha ya wananchi ili wasishawishike kufanya uhalifu.


  Tunaiasa serikali, kwamba endapo haitachukua hatua madhubuti kudhibiti utoaji holela wa leseni za silaha, itakuwa inaongeza mzigo mkubwa kwa jeshi la polisi, na vifo kwa raia wasio kuwa na hatia. Kuwapa silaha raia wenye njaa ni kujinyonga...
  [​IMG]
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Colt 45

  Tembelea:

  mwana dikala
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...