UMEYA MOROGORO: CCM wapigana ngwala................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UMEYA MOROGORO: CCM wapigana ngwala...................

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Dec 15, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  CCM Morogoro yachafua hewa


  na Mwandishi wetu, Morogoro


  [​IMG] CHAMA cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Morogoro mjini, kimelalamikiwa kwa kuwahujumu baadhi ya wagombea wa nafasi ya umeya na Unaibu Meya kwa kile kinachodaiwa kuwafanyia kampeni za waziwazi wagombea wawili wanaowataka wao. Wakizungumza na Tanzania Daima kwa sharti la kutotajwa majina yao kwa nyakati tofauti, baadhi ya madiwani hao wamedai kuwa wamekuwa wakiitwa na vigogo wa wilaya na kupewa misimamo ya mtu gani anayefaa kuwa Meya wa mji huo.
  Viongozi hao ambao wanadaiwa kuwapigia debe watu wao ni pamoja na vigogo wawili wa wilaya hiyo ambao majina yao kwa sasa, yamehifadhiwa.
  Wanaodaiwa kupigiwa debe katika kinyang’anyiri hicho ni pamoja na diwani wa kata mbili za mjini hapa ambao majina yao pia yanahifadhiwa.
  “Hawa watu wanaharibu sana chama mwanzoni walikuja na njia ya kuleta ukabila kwa kushirikiana na kikundi cha kabila la Waruguru cha Manispaa ya Morogoro kijulikanacho kama Twimanye…..
  “CCM mkoa nao umekuwa ukifumbia macho mambo hayo, sio kama hawayaoni wanayaona sana, na baadhi ya viongozi wa mkoa wamekuwa wakishiriki kuhakikisha jambo wanalolitaka viongozi hao wa wilaya linafanikiwa,” alisema mmoja wao.
  Walisema hali hiyo inawatia mashaka na kuwaondolea imani na viongozi hao na kumwomba Rais Jakaya Kikwete kuwachukulia hatua viongozi hao wenye lengo la kuiharibu CCM.
  Madiwani hao waliiambia Tanzania Daima Jumatano kuwa viongozi hao walikuwa wakifanya hayo, huku wakitumia jina la Rais Kikwete kwamba ametoa baraka kwa madiwani hao kushinda.
  Uteuzi wa umeya na unaibu meya ndani ya CCM, unatarajiwa kufanyika leo ambapo majina wagombea wa nafasi hizo, baada ya kupatikana yatapelekwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Morogoro kwa ajili ya kupigiwa kura na Baraza la Madiwani.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  Tatizo la CCM ni mageuzi ya shingo upande.....................hivi yale mageuzi ya kuwashirikisha wanachama katika kuwapigia kura ya maoni wagombea ubunge kwa nini hawakuyasogeza hadi hapa?
   
 3. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Inategemea ni lengo gani linawaongoza kwa wakati huo. Ule ulikuwa mkakati maalum wa Makamba ambao kwa upande wa madiwani hana maslahi nao sana. Ndivyo mambo yalivyo
   
Loading...