Umeya Arusha utata mtupu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,073
1,250
UTATA wa uchaguzi wa umeya jijini Arusha umechukua sura mpya mara baada ya naibu meya aliyechaguliwa juzi ambaye pia ni diwani wa TLP katika kata ya Sokoni jijini Arusha, Michael Kivuyo kuibuka na kutoa matamko mawili tofauti moja likiwa ni kutoutambua uchaguzi uliofanyika kwasababu ulikuwa ni batili jingine ni kukubali uteuzi wa nafasi yake katika uchaguzi huo.

Hatahivyo nao uongozi wa Manispaa ya Arusha chini ya msimamizi wake,Estomi Chang’a pamoja na ofisi za meya wa nayo kwa pamoja jana waliibuka na kutoa ufafanuzi juu ya utata uliojitokeza katika uchaguzi huo
Tamko hilo la naibu meya huo lilionekana kuzua kizazaa jijini hapa ambapo alilitoa katika hoteli ya Equitor iliyopo mkabala na ofisi za manispaa wakati akihojiwa na waandishi wa habari waliotaka kujua msimamo wake kwa sasa baada ya uteuzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari majira ya saa 7;30 mchana, naibu meya huyo aliasema uchaguzi uliofanyika ni batili kwa sababu idadi ya theluthi mbili za wajumbe waliopaswa kupiga kura haikutimia na hivyo kuuita kuwa ni batili.
Mbali na sababu hiyo, Kivuyo alipigilia msumari akisisitiza kitendo cha mbunge wa viti maalumu mkoani Tanga, Mary Chatanda kupewa ruhusa ya kupiga kura kilikuwa na uwalakini kutokana na yeye kutokuwa mwakilishi wa Mkoa wa Arusha.

“Msimamo wangu uko wazi kabisa uchaguzi ulikuwa batili kwani column (idadi) ya wajumbe haikutimia, lakini kitendo cha kumruhusu mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Tanga kupiga kura nacho hakifai na nilishasema kabisa hata ITV”alisema Kivuyo.

Wakati huo huo katika mkutano ulioitishwa jana na meya wa Manispaa ya Arusha, Gaudence Lyimo, naibu meya huyo alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya madai ya yeye kutoutambua uchaguzi huo ihali ndio uliomuingiza madarakani, Kivuyo alishikwa na kigugumizi na kudai mbali na kutoutambua, lakini anakubali uteuzi wa nafasi yake.
“Lakini mimi nakubali kuwa ni naibu meya”alisema Kivuyo kabla ya kuomba ridhaa ya kuondoka katika kikao na wanahabari.

Katika mkutano wa ufafanuzi juu ya utata uliofanyika ndani ya ofisi za meya mkurugenzi wa manispaa hiyo, Chang’a alifafanua utata wa suala la Chatanda na kwamba mwakilishi huyo aliruhusiwa kupiga kura kutokana na maagizo kupitia kwa ofisi ya Bunge la Jamhuri la Tanzania.
Chang’a alisema mara Chadema walipoibua hoja ya Chatanda ilibidi awasiliane na Ofisi ya bunge na kupatiwa maagizo ya barua iliyotumwa kwa nukushi yenye KUMB,NA CEB.77/77/155/01/79 ya desemba 17 iliyosaniwa na Naibu Katibu wa Bunge, Eliakimu Mrema ambapo barua hiyo ilimtambua Chatanda kama mjumbe halali wa Manispaa ya Arusha.
“Mara baada ya hoja ya Chatanda kuibuliwa na Chadema ilibidi nipate ufafanuzi kupitia ofisi ya bunge ambapo walituma barua kwa fax kuwa Chatanda ni mjumbe halali wa manispaa ya Arusha”alisema Chang’a

Kuhusiana na suala la idadi ya wajumbe kutotimia ili kuweza kumchagua meya na naibu wake, mkurugenzi huyo alifafanua kwamba suala hilo sio kweli kwani nusu ya wajumbe ambao ilikuwa ni madiwani 17 walitosha kupiga kura katika uchaguzi huo kwa taratibu za kisheria.

“Hili suala la Chadema kudai kuwa idadi ya theluthi mbili ndio wanapaswa kufanya uchaguzi halipo mimi nilipoona wajumbe 17 wanatosha kufanya uchaguzi nikaamua kuitisha sasa utata uko wapi”alifafanua Chang’a
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom