Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,188
- 3,360
Binafsi ni moja wa watu niliowahi kuexperience kufungiwa selo, Niliwekwa lock up Police central pale Arusha, Nlivyofika niliingia chumba kidogo cha kutoa maelezo ya kesi na kuhifadhi vitu nlivyonavyo na kuamrishwa nichuchumae (ukiwa mbishi unakula makofi ya kutosha)nakumbuka nilikuwa na simu na elf 22, nlkakabidhi vitu vyangu nikapewa kijikaratasi cha vitu nlivyoweka.
Nlivyotoka hapo kilichofata nliamrishwa(sio kuombwa) kuvua mkanda na viatu nikasachiwa fasta fasta kama kuna vitu nimeficha then nikaingizwa ndani selo(hapo ilikuwa kipindi cha baridi kungekuwa na joto ningeingia na boksa peke yake), Aisee ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia mule nliwahi kuskia masela wa mule ukiingia wanakupiga lakini wala sikuguswa na tulisalimiana vizuri na story ziliendelea, Jion kuna roll call unaitwa jina la kwanza sasa ole wako useme "Nipo" utakiona, inabidi useme jina lako la ukoo unahamia uoande wa watu waliohesabiwa, Ikifika usiku utaratibu ni huo huo, Mule ndani sio mahala pazuri mpasikiage tu, Ikifika usiku mnalala chini kwenye sakafu hakuna cha mkeka wala nini na mnalalia ubavu ili wote mlale mana mnakuwa wengi sana huwezi kulala kama upo kitanda cha 6x6, Nashukuri mungu kesho yake nlipewa dhamana nikarudishiwa vitu vyangu na nikaondoka na kilichofata ilibidi niripoti polisi wiki nzima asubuhi saa mbili na nilifanya hivyo.
Kosa langu lilikuwa ni dogo sana na ushauri naowapa mtii sheria mana hata ukimwaga taka sehem isiyotakiwa, kukojoa sehemu zisizotakiwa kunaweza kukupeleka mule ndani.