Umewahi Kukutana Na Huyu ??

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
219
Kuna wakati mwingine tunapokuwa katika shuguli mbali mbali za kimaisha kuna mambo watu wanakutana nayo haswa ambayo mengi wanayaweka kapuni kwasababu unakuta ameshamalizana nao kwahiyo anaendelea tu na maisha yake , hajui kama akiamua kuelezea mkasa wake sio tu anakuwa amejiondolea msongo wa mawazo na kuwa huru zaidi bali atakuwa ametoa mwanya kwa wengine wasiojua kujua zaidi na kuweza kujipanga zaidi .

Rafiki yangu mmoja alipigiwa simu na mtu mmoja huyu mtu alikuwa anahitaji laptop akataja specifications zake na mengine aliyokuwa anayataka yeye kwahiyo huyu rafiki yangu akamtafutia laptop hiyo akaenda kuinunua kwa mtu mwingine ili aje kumuuzia huyu mwingine aliyekuwa anataka .

Alipofika pale katika kukabidhiana jamaa akasema hana pesa kwa pale kwahiyo waende katika ATM watoe pesa wampe , katika kufanya hivyo wakaingia katika gari , yule jamaa akafunga vioo vyote na loki za gari kuanzia hapo akamwambia yule rafiki yangu kwamba kuanzia sasa yuko chini ya ulinzi

Rafiki yangu akapelekwa mpaka kituo cha polisi aliposhuka katika gari akawekwa pingu , moja kwa moja mpaka kituoni kwa mahojiano kule katika mahojiano akaambiwa aseme kwa nani tena ameuza tena laptop akataja kesho yake asubuhi wakaenda kuchukuliwa wale watu ambao amewauzia hizo laptop .

Kumbuka rafiki yangu hakuambiwa atoe maelezo mpaka asubuhi ilipofika yeye alilazwa ndani tu aliambiwa akiulizwa chochote aseme amefungwa kule kwa kesi simu ya mkononi akisema ni suala la laptop pale kuna kesi nyingi za laptop kwahiyo kesi zote za ndani mule atapewa yeye rafiki yangu akaogopa sana .

Asubuhi ilipofika ukaanza msako kuwatafuta wale ambao anawauziaga hizo laptop zile laptop zikaenda kuchukuliwa tu bila maelezo yoyote wakishampata mwenye laptop hiyo ni halali yao , kumbuka mpaka hapo askari yule hajamuuliza yule kijana vielelezo vyovyote kuhusu laptop ile kama risiti na maelezo mengine yote haya askari hajauliza .

Haya wakachukuwa laptop zingine , rafiki yangu hajaenda kazini wanamtafuta mpaka nyumbani ,askari hajatoa nafasi kwa kijana yule kuongea na jamaa zake wengine kumtafuta kujua yuko wapi na anafanya nini watu wanawasi wasi na mpendwa wao
Ikaingia siku ya 3 yule kijana bado yuko na askari yule kutafuta hizo laptop zingine ambazo yule kijana aliwauzia watu alikuwa anaambiwa asiende kwa watu wazima aende kwa vijana wenzake kwanza huyu askari alikuwa anauliza hao anauliza ni wa size gani kama ni wazima basi haendi kwa sababu alikuwa anajua atakachokutana nacho .

Basi siku ya 4 ndio akapewa muda wa kuongea na jamaa zake wengine kuwajulisha kwamba yuko wapi , na alipewa masharti kwamba aweke loud speaker ili askari naye asikie anasema nini mimi nilipewa taarifa hizo pia nikaenda katika sehemu husika .

Ikabidi niende kazini kwake pia , kule kazini kwake wakasema huyo mtu alichukuwa laptop moja ya kwenda kuuza kwa mteja wake hajarudi tena wakafikiri amepotea na laptop hawakuwa na mawasiliano naye tena lakini ndio hivyo alikuwa ameshikiliwa na huyo polisi .

Niliporudi tena kule polisi askari akawa anataka shilingi laki 2 ili aweze kumwachia yule kijana au kama hiyo haiwezekana basi laptop iachwe pale atafutwe mteja mwingine aje kununua hiyo laptop wagawane hizo pesa nusu kwa nusu ndio kijana yule awe huru sasa .

Nikamwomba polisi maelezo ya mshitakiwa bado askari hana maelezo anatoa maelezo mengine ya watu ambao walienda kulalamika kituo hicho cha polisi na akasema kama tukiendelea kubishana zile kesi zote anamtupia yule kijana , sasa hapo kesi ilikuwa ameshabadilishwa

Muajiri wa huyu kijana alivyoenda hapo polisi akaambiwa kijana wako amekamatwa na kifaa cha wizi ambacho sio ile laptop iliyokuwa pale muajiri akaambiwa atoe laki 2 kama dhamana ya kijana huyu muajiri hakuwa na lingine la kufanya nae akashindwa kuelewa .

Hiyo laptop haikuwa polisi ilikuwa gest house ambayo iko karibu na kituo cha polisi na vingine vyote ambayo alikuwa navyo huyu kijana , polisi kaamuwa kuweka vitu vya watu katika nyumba ya wageni na mtuhumiwa kuwekwa katika selo

Yule muajiri alipewa ile laptop yake akaondoka nayo lakini kijana akabaki pale kituoni bado kwa sababu ambazo hazieleweki basi mimi nikaenda kumsaidia huyu rafiki yangu na mambo yake hizo hela tukazitoa kwa mara ya pili .

Halafu nikaanza kuongea na huyu askari kumjua vizuri kujua nani alimpa namba ya yule kijana akamtaja na sasa nikamuuliza huyo aliyekupa namba yake na kuja kulalamika yuko wapi adhibitishe kwamba kweli ndio huyu na mali yake ndio hiyo nikaambiwa huyo mtu amesafiri hawezi kuja mahali hapo .

Nikakubaliana nae tukutane nae baada ya wiki moja tuongee mambo mengine kuhusu ICT na mambo mengine kwa sababu alikuwa yuke interested akaniambia analaptop yake anapenda kuitumia .

Baada ya wiki tukakutana na yule askari tena kwenda kuongea na kuona hiyo laptop anayoisemea , nikaiwasha na kuangalia ndani yake hiyo laptop haikuwa mali ya huyu askari ilikuwa ni mali ya mtu mwingine wa dodoma kwa sababu usajili wake unaonyesha pale , nyaraka zake ziko ndani ya laptop ile sikupenda kumuuliza ameitoa wapi au kama yeye jina lake ndio lile lilioandikwa mule katika hiyo laptop .

Nikamwonyesha baadhi ya mambo tu , kisha ndio tukaenda katika hiyo nyumba ya wageni kwenda kuona vitu vingine zaidi maajabu huyu askari ana mali nyingi sana za watu haswa laptop zaidi ya 10 zilizokuwa na nyaraka za watu mule katika nyumba ya wageni ambayo iko karibu na kituo hicho cha polisi .

……………………………………………………………………………….

Baada ya muda kidogo huyu askari akanipigia mimi simu kuna mtu alipotelewa na laptop yake akaenda kushitaki pale computa yake alikuwa ni aina ya MAC soma maongezi yetu

Polisi – kuna mtu yuko hapa ametoka kidogo lakini nitakupigia na namba nyingine naomba umwambie unaweza kumtafutia hiyo laptop lakini atoe chochote .

Mimi – je kama hicho kitu kisipopatikana na hela umeshachukuwa

Polisi – nimemwambia wewe ndio gwiji mwenyewe usijali

Mimi – kwanini umempatia no yangu bila ridhaa yangu ?

Polisi – dogo unataka tufufue ile kesi yenu ? jibu kama nilivyokutuma hili ni dili .

Muda kidogo nikapigiwa simu na mtu huyo akanieleza ikabidi nikate simu yangu na kuizima kwa muda .

………………………………………………………………………………..

Ikabidi sasa nianze kutembea kati kati ya mji kuonana na jamaa wengi kuanza kuulizia experience zao namambo yale wakasema askari huyo ndio zake hiyo tabia anayo kwa muda mrefu sasa watu wanapotezewa muda wao sana na mengine .

Nilipojaribu kudadisi zaidi kuna watu anashirikiana nao hawa watu wenyewe huwa wanajifanya wameibiwa laptop au vifaa sasa mtu anapomwandikia kwamba jaribu hichi na kile basi ndio huyo mtu anatafutwa anaambiwa yeye apelike kitu Fulani na ndio mzozo unapoanza hapo .

Haya ndio mambo ya ASKARI WETU sasa hali inatisha watu ambao tunategemea wawe ndio walinzi wa mali na vitu vyetu ndio wanageuka wanakuwa hivi .

Kama ndio hivi wanafundishwa huko katika vyuo vya upolisi au kama katika viapo vyao wanaapa kuendesha vitendo hivi kwa udi na uvumba basi iko kazi mitaala yao inabidi ibadilishwe .

Maisha mema ndugu mabibi na mabwana .
 
Shy, una taarifa muhimu sana ambayo itasaidia kukomesha tabia kama hizi na kutenda haki kwa watu wasio na hatia. Unaonaje kama ukimpigia simu Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam ili umueleze haya mambo, nina amini atakupa nafasi mkutane naye umpe A to Z.

Does this make sense to you?
 
hii kali, umtajie na jina la huyo polisi hayawani! hatuna haja ya kuficha madudu ya namna hii. hili dili likiisha anaweza kuhamia kwenye dili la kuchukua silaha kituoni na kushirikiana na majambazi kuvunja nyumba za watu na kuua. chonde chonde shy usimwache
 
Ni vizuri utoe majina kamili (Manina yake mawili au matatu), jina moja halitoshi, maana wapo James wengi.
 
Unaweza pia toa namba yake kama unaifahamu maana hiyo ni moja tu na ni rahisi kuwa traced.
 
Back
Top Bottom