JosephElly
JF-Expert Member
- Jun 5, 2012
- 2,432
- 1,035
Ndio mkuu, ndo hali halisiMiaka 8 ni usingizi tu
Dah... hapo ukitoa umri wako unaweza jikuta hujala chumvi hata kijiko... ulikuwa umelala all the time... teh teh tehYani kupiga hesabu hapo mpaka naona uvivu kwa sisi vilaza wa hesabu ila nahisi mimi ntakuwa nimeshalala miaka kama 9 hivi.
Nitatumia hesabu rahisi sana kueleweka kuelezea hili.
Tuchukulie wastani unalala masaa 7 kwa siku,
7(hrs) x 365 days = 2555 hrs/days
2555 hrs/days / 24hours = 106.46 days
Hii inamaana kwa mwaka endapo ukiwa na wastani wa kulala masaa 7 kwa siku basi jumla ya siku 106.46 katika mwaka utakuwa umezipoteza ukiwa usingini.
So tukichukulia wastani huo huo kwa umri wa mtu wa miaka 30.
30 years x 106.46 days = 3,193.75years/days
3,193.75years/days / 365 days = 8.75 years.
So kwa mtu mwenye miaka 30 ambaye wastani hulala kwa masaa 7 kwa siku basi anakuwa ametumia miaka 8.75 akiwa usingizini tu.
Piga hesabu kulingana na wastani wako wa muda wa ulalaji na umri wako
Kimahesabu haya mahesabu yako yako sawa, ila kuna few exceptions kwa makundi ya watu...
Kwa sisi ambao tunakesha kama cnn muda wakulala ni mchache sana ukilinganisha na akina Nyasiro ambao ikifika saa nne washategeshea torrent ni kulala tu
Mi sijafanya hesabu hiyo
.
Lakini nadhani nimelala for 5 years
.
Natumaini hapo miaka kama mitatu imeongezeka coz Sikuwa na modem
.
Ila now nalala sana..... Kuna vitu naviweka sawa
Hakuna unachopoteza hapo,kulala ni hitaji la msingi la kimaumbile,lazma ulale na huwez kusema mda uliolala umeupoteza,kwamba umeenda bila faida,kama unataka hvyo usipoteze acha kulala ili usipoteze mda,hlo ni jambo moja umesemea,mbona hujaongelea msosi ambao kwa wastan mtu hula tani mia za msosi kwa maisha yake,je unaweza kusema amepoteza tan mia,kama unataka usipoteze acha kula,watu wengne wanaleta hoja za kutengeneza faida kwenye mambo ambayo sio ya msingi.
Nilivyo anza kusoma point yako nilikubali kuwa kweli hupotezi muda kwa kulala, ila katika hoja yangu neno poteza lipo sehemu moja tu.
Lakini nilivyoendelea kusoma comment yako nikaanza gundua ujinga wako umeanza kujitokeza,
Kwanini nisiseme mtua amepoteza tani ngapi za chakula? Kwani nilazima nilete fact zote za kuhusu binaadamu? Ok ningeleta na huo uzi, ungeuliza mtu hutembea wastani wa kilomita ngapi maishani?
"watu wengne wanaleta hoja za kutengeneza faida kwenye mambo ambayo sio ya msingi."
Unaweza kueleza ni faida gani ninayoipata kwa kuandika juu ya mada hii?
Hakuna mtu aliye sahihi kwa asilimia 100%, unaweza kukosoa na mtu akakuelewa sio kuanza kulete maneno yasiyo na msingi.
yameisha bwana mkubwa!haina haja ya maneno mengi mkurugenzi.
aisee mimi mbona imekja miaka 15 au nakosea wapi..