umeshindwa kumwacha, nyamaza

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,271
2,401
karibuni nilikutana na mdogo wangu wa kike kwenye daladala. Alikuwa na rafiki yake wa kike wakitokea chuo (sikitaji). Baada ya muda yule shost alishuka nikabaki na mdogo wangu. Tuliposhuka nikamuuliza vipi kuhusu rafiki yako? Nikutanishe nae. Nimevutiwa nae. Akaniambia tayari ana mchumba wake. Nakasema basi.

Baada ya muda akaniambia kuwa lakini shost yake huyo hana raha katika mahusiano yake. Jamaa anambana sana hadi kumnyima uhuru. Inafika wakati anatamani kuachana nae. Moyoni nikasema YES! Nikamwambia mshawishi waachane. Akasema atalifanyia kazi.

Baada ya siku chache nikampigia mdogo wangu kumuulizia ishu imefikia wapi. Akasema alijaribu kumshawishi lakini binti alikataa kushawishika. Akasema anaogopa akiachana na jamaa, atamuua. Nikashangaa sana moyoni.

Hizi ndizo fikra za wanawake na wanaume? Haya ndo mapenzi? Hapo ni uchumba. Wakioana itakuwaje? Moyoni nikasikitika binti mzuri anakosa amani kiasi hicho. Yani hadi leo wanawake hawajitambui? Anaogopa atauawa...!
 
Mkuu ukijiangalia vizuri utagundua kinachokufanya useme hvyo ni vile umependa. Ila sikuzote mambo ndo yapo hvyo. Good girls love bad boys!

hapo nakukatalia. Huyo jamaa ni ant social. Jamaa anatumia zaidi vitisho kuliko adventure. Labda hiyo tafsiri ya bad boy umeigeuza. Kuna bad boys kwa maana ya adventure katika mapenzi na kuna hawa aina ya huyu jamaa
 
ni kweli akina mama hawajitambui,jamaa alimfuma mke wake anaongea na hawara wake,jamaa akmbana mkewe amweleze ni nani lkn mama akamdanganya mumewe,kisa jamaa alimtishia akimtaja atamua unaona kazi hiyo
 
teh teh sasa kinachokufurahisha hapo au kukuudhunisha hapo ninini? kama sio umbea tuu...inaonyesha unataka kutumia udhaifu wa mvulana mwenzako kumpata mrembo wake....! teh teh, kama unabusara nafikiri ni vema ukawaalika yeye na boyfriend wake kupitia mdogo wako dinner one day uwaeleze maana ya mahusiano, ....!
 
karibuni nilikutana na mdogo wangu wa kike kwenye daladala. Alikuwa na rafiki yake wa kike wakitokea chuo (sikitaji). Baada ya muda yule shost alishuka nikabaki na mdogo wangu. Tuliposhuka nikamuuliza vipi kuhusu rafiki yako? Nikutanishe nae. Nimevutiwa nae. Akaniambia tayari ana mchumba wake. Nakasema basi.

Baada ya muda akaniambia kuwa lakini shost yake huyo hana raha katika mahusiano yake. Jamaa anambana sana hadi kumnyima uhuru. Inafika wakati anatamani kuachana nae. Moyoni nikasema YES! Nikamwambia mshawishi waachane. Akasema atalifanyia kazi.

Baada ya siku chache nikampigia mdogo wangu kumuulizia ishu imefikia wapi. Akasema alijaribu kumshawishi lakini binti alikataa kushawishika. Akasema anaogopa akiachana na jamaa, atamuua. Nikashangaa sana moyoni.

Hizi ndizo fikra za wanawake na wanaume? Haya ndo mapenzi? Hapo ni uchumba. Wakioana itakuwaje? Moyoni nikasikitika binti mzuri anakosa amani kiasi hicho. Yani hadi leo wanawake hawajitambui? Anaogopa atauawa...!

...usukule huo....

kujikubalisha kudhani kwamba bila yeye hakuna tena maisha...
mtu anakujengea imani kwamba ati either yeye afe (ajiue) au wewe
ufe au mfe wote sababu ya penzi...

ujinga mtupu!

sikatai kwamba watu wanauana au kufa sababu ya mapenzi, alkini hiyo ni
dalili tosha ya mtu aliyeshindwa kujitambua thamani yake kiasi kwamba
anaona maisha yake yameshikiliwa na mwingine.

mwanaume huyo anayetishia kumuua huyo binti, usikose naye tayari keshamjaza
maneno huyo binti kwamba atajiua akiachwa....hahhhh!? mapenzi si upofu, ni kuchagua kutoona!
 
bora wewe mkuu umeliona hili. Na wanaosema nashindwa kujitafutia hawajui kuwa mahusiano yana njia nyingi tu za wawili kukutana. Haijalishi ni mdogo mtu kaunganisha. Mbona kuna wazazi wanawaunganisha wanao na wana wanaishi vyema tu? Sembuse mi na mdogo wangu, tena si wa kuzaliwa.
lengo la mimi kuleta hichi kisa ni kuona jinsi gani wanawake wasivyo na maamuzi ya ziada kwenye mahusiano. Hilo tu
 
Usikute huyo shoga kamwambia dada yako hayo ili akuondoe njiani tu. Hivi mtu umkute kwenye daladala tu ndo umvunjishe mapenzi yake na jamaa!
 
Good girl (or very good) kakaaje?
A good girl ni yule ambae hafanyi kitu chochote kinyume na tabia generaly accepted as "good values" of the society she lives in, na hafanyi kitu she would be ashamed to confirm if confronted... a very good girl does that and anawashawishi wengine around her to do the same... and it applies to good boys and very good boys too.
 
Kwa hiyo good girl ni subjective na mazingira mtu aliyopo. Pia litaingia na suala la generally accepted by who? Society yoyote haina good values ambazo zinakubaliwa na wote.

Ukiweka hizo points mbili, good girls ni takriban wote
 
part niliyoipenda ni hiyo ya wewe kumuomba dada yako akukuwadie...unasubiri uletewe jibu la ndio? man up and face the lady kama kweli wampenda....
 
I am a good girl (very good in fact) and I hate bad boys. inatokea mkuu. Na kama mtoa mada anampenda kweli huyo dada basi awe hero wake kwa kumset free from that man.

watu kama hao ni wa kuacha kama walivyo hadi wafunguke macho wenyewe
 
karibuni nilikutana na mdogo wangu wa kike kwenye daladala. Alikuwa na rafiki yake wa kike wakitokea chuo (sikitaji). Baada ya muda yule shost alishuka nikabaki na mdogo wangu. Tuliposhuka nikamuuliza vipi kuhusu rafiki yako? Nikutanishe nae. Nimevutiwa nae. Akaniambia tayari ana mchumba wake. Nakasema basi.

Baada ya muda akaniambia kuwa lakini shost yake huyo hana raha katika mahusiano yake. Jamaa anambana sana hadi kumnyima uhuru. Inafika wakati anatamani kuachana nae. Moyoni nikasema YES! Nikamwambia mshawishi waachane. Akasema atalifanyia kazi.

Baada ya siku chache nikampigia mdogo wangu kumuulizia ishu imefikia wapi. Akasema alijaribu kumshawishi lakini binti alikataa kushawishika. Akasema anaogopa akiachana na jamaa, atamuua. Nikashangaa sana moyoni.

Hizi ndizo fikra za wanawake na wanaume? Haya ndo mapenzi? Hapo ni uchumba. Wakioana itakuwaje? Moyoni nikasikitika binti mzuri anakosa amani kiasi hicho. Yani hadi leo wanawake hawajitambui? Anaogopa atauawa...!

Wewe na Mdogo wako lenu moja tu, Demu anaonekana anamsimamo na mtu wake ndio maana mipango yako haifanikiwi. Halafu hili lakupeana lift na mdogo wako naona kama vile ni ukosefu wa maadili maana mzee mzima unakosa privacy na huyo unayeomba lift kwake, hili kwa mwanamke mwenye akiri hakubali kabisa. Haya Mambo yakidhungu bwana inawezekana hata rafiki yako akimtaka mdogo wako utampigia pande vile vile au mdogo wako akiwa na tabia mbaya sijui ujasiri wakumkea utaupata wapi?
 
Usikute huyo shoga kamwambia dada yako hayo ili akuondoe njiani tu. Hivi mtu umkute kwenye daladala tu ndo umvunjishe mapenzi yake na jamaa!

we unaishi dunia gani? Kwanza umesoma mada vizuri?
 
Wewe na Mdogo wako lenu moja tu, Demu anaonekana anamsimamo na mtu wake ndio maana mipango yako haifanikiwi. Halafu hili lakupeana lift na mdogo wako naona kama vile ni ukosefu wa maadili maana mzee mzima unakosa privacy na huyo unayeomba lift kwake, hili kwa mwanamke mwenye akiri hakubali kabisa. Haya Mambo yakidhungu bwana inawezekana hata rafiki yako akimtaka mdogo wako utampigia pande vile vile au mdogo wako akiwa na tabia mbaya sijui ujasiri wakumkea utaupata wapi?

soma tena mada kwa utulivu
 
Back
Top Bottom