2004 nikiwa kisiwani Lukuba nikiwa mvuvi mashuhuri kijana,nikapendwa kimapenzi na binti wa darasa la 7. Sasa ninachokifahamu mimi nikutokumkatalia mwanamke ombi la mapenzi waziwazi.
Basi,kila akitoka shule ile saa kumi alasiri ananiombe nimsindikize kuelekea kwao.
Sasa siku moja akaniomba nimfikishe nyumbani kwao,hapo sijawahi kumkubalia wala kumkatalia ombi lake.
Ile tunafika nyumbani kwao,akatokea ndugu yake ndani,alikuwa mwenye elamavu wa miguu.
Alikuwa wa kike nadhani alikuwa mkubwa kwa huyu mwanafunzi na alikuwa akitembea kwa kujivuta chini kwa kutumia makalio.
Hili lilichagiza moyo wangu kumsogeza huyu binti mita 5 mbali nami tena na ilinichukua miezi 6 sijamjibu ukiachilia mbali kuzurula naye kitaani mpaka nilipobadili kazi ila alikuwa akinilaumu kuwa kutokueleweka kwangu kuna mtesa sana.