Umeshawahi kupata mpenzi tapeli?

Umeshawahi kupata mpenzi tapeli?

Faith HJ

Senior Member
Joined
Aug 16, 2017
Posts
177
Reaction score
215
Habari zenuuuu

Swali ndio kama hilo, Nakumbuka ilikua mwaka 2012 nilikutana na kijana mtanashati sana, handsome, Yaani ukimwangalia anavutia kwakweli. kukutana kwetu ilikua katika mazingira ya kazi tu tukajikuta tukibadilishana namba,sikua na kuaanza kuwasiliana mara chache chache sikua nikimtafuta mara kwa mara si kwamba sikutaka hapana nilijizuia nilitaka asione namhitaji sana lakini kiukweli nilimpenda. Siku moja akaniambia naenda harusini tarehe Fulani na nimelipa kadi ya double je unaweza kwenda na mimi sikua na hiana na wakati huo tulikua tukichat tu Hakuonyesha kama ana any feelings for me so I trusted him.

Tarehe ya kwenda harusini ilifika akanitafuta asbh kuniambia kama sikua na nguo ya kuendea kwenye sherehe nimwambie, mimi nimwambia ninayo lakini sio nguo mpya kati ya nguo zangu za kutokea nilichagua mmoja ambayo niliona ingenifaa. Ilipofika mida ya kwenda aliniambia nimsubiri sehemu atanipitia na kweli niliwahi akaja akanichukua tukaenda huko Harusini.

Mambo ya huko yaliendelea kama mjuavyo harusini kulivyo, tulipomaliza ilikua kama saa 7 usiku akaniambia tuondoke,tukaodoka hapo sasa akiwa ananirudisha kwangu na hakuwa anapafahamu,kabla ya kufika home kwangu, Akapaki njiani nikaogopa nikamwuuliza mbona unapaki akanijibu nataka kuongea na wewe nikwa nimetulia nikamwambia ok.....Akaniambia Faith NAKUPENDA tangu nilipokuona nilitamanikukuambia ila sikuona mda sahihi wa kukuambia kutoka na kuwa busy mda mwingi but nadhani leo ndio siku sahihi kwangu nivuta pumzi kwanza ile ya hofu akagundua nimepata hofu akaniambia usihofu.

ki ukweli sikumjibu ndio wala hapana, akanirudisha mpaka kwangu tukaagana akarudi zake kwake. sikulala vizuri mawazo mengi yalinisumbua yaliyochanganyika na furaha coz hata mimi nilimpenda ila sikutaka kujionyesha. asbh alikua wa kwanza kunitafuta na kuniomba niende kumsalimia kwake hata sikubisha nikasema sawa.

Mda ulipowadia nilienda baada ya kunielekeza nikamkuta anapika, nikamsaidia tukamaliza tukala then tukaanza kuangalia movie nilipostuka ilikua saa 2 usiku nikamwomba nirudi akanirudisha lakini kabla ya kunishusha alirudia maneno yake ya kuniambia ananipenda nami sikumjibu. Tuliendelea na mawasiliano hapa sasa hata mimi nikawa namtafuta. kuna siku aliniambia anaenda kikazi Mwanza kama nitaweza kuomba ruhusa kazini kwangu twende wote nikamwambia mpaka niombe ruhusa kwanza nikikubaliwa ndio nitamjibu kweli nilienda ofisini nikaomba ruhusa nikapewa nikamwambia nimekubaliwa akafurahi mnoo. Tukasafiri zetu tulipofika Mwanza akaniambia niwe huru kama sipo tayari kulala nae chumba kimoja nilale peke yangu nikamwambia nilale mwenyewe akalipa 2 rooms siku hiyo kila mtu akalala kwake.

Asbh alikuja kunisalimia kisha akaniga kwenda huko kwenye kazi iliyompeleka, jioni aliporudi alinikuta Hotelini naangalia Movie akaniambia tukateembee, Nilikubali nami Mwanza ilikua Mara yangu ya kwanza kufika Tulizunguka zunguka then tukarejea hotelini tukala tukaingia vyumbani mi nikaoga nikaa kitandani nikaanza kuchati na baadhi ya marafiki ilipofika kama saa nne usiku nikasikia mtu akigonga nikafungua nilimkuta J mlangoni hakuongea Chochote alichofanya ni kunivutia kufuani kwake na ma kiss kama yooote kikafanyika kilichotarajiwa.

From there we started serious relationship, next day Tulirudisha room moja tukawa tunalala wote, baada ya 4 days mimi nilirudi kazini na yeye alirudia after 14 days. Tuliendelea na mahusiano yetu. He was a good guy sijui tu alikujaga kupatwa na nini, Mwaka uliisha nikiwa katikati ya mahaba. shida ilianzia hapa niliomba Mkopo wa Mshahara kwa muda wa miaka 5 nikamwambia mpenzi wangu akafurahi nikidhani kafurahia ambacho nimepanga kufanya nitakapopata Mkopo kumbe mwenzangu Hatukua pamoja.

Nikapata mkopo nikamwambia tayari, tulikaa kama wk mmoja akaja na stori kuwa kuna mahali nyumba inauzwa haifaisha I mean (pagale) badala ya kufanya ninachotaka kufanya bora ninunue hiyo sehemu ni Asset nzuri nikakubali na yeye ndio ananiunganisha na huyo mtu, Wapendwa nilienda kutoa hela zangu zote nikampa yule mwanaume akaja kuniambia tayari nisubiri hati inaandaliwa tulikaa kama wiki 2 hivi akawa Gafla akawa haeleweki mwisho hakupatikana.

sikumpata tena hakuatikana kwake kwa mda mrefu kitu kama 2 years Gafla siku moja najizungukia zangu mjini nikakutana nae dukani. akaniita Faith mi nikamjibu kwa kumwambia presentable man like you lakini ni TAPELI aliniangaliaa nikaona Chozi linamtoka na mimi hapo nilishapata hasira so sikutaka kuendelea kuongea nae nikaondoka maana nilihisi ningeleta shida Dukani kwa watu bure. mpaka leo nimeshamaliza mkopo ila huwa nawaza huyu Mwanaume alipatwaga na Shetani gani jamani ni hicho kihela kidogo tu hivyo ndio kilikutoa roho J wangu? nibora ungesema tu ulipata shida au Mbona ulinijali tu jamani na kuonyesha ulinipenda? Labda nikupe nafasi uniambie ulipatwaga na nini maana bado huwa siamini kama kweli ni tapeli, Hivi wadada wenzangu kuna yeyote alieyepitia haya kama mimi?
 
Pole sana faith. Hayo mambo hutokea tu. I guess mshkajini yule type ya watu ambao wakipatwa na shida hawasemi. Wanaugulia kimya kimya..
Hiko ni kitu kibaya sana hasa kwa mpenz wako.

Anyway. Faith.. sijui nn kiliendelea mpaka hapo. Ila uwe makin. Jarib kumchunguza mtu kabla ya kuwa nae serious.
 
Somo la bure hili..

You may not start conversation with the following recipient;Tairus
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom