Umeshawahi kununua kitu cha wizi?

Umeshawahi kununua kitu cha wizi?

Desierto

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
847
Reaction score
2,954
Huu msala omba tu usikukute aisee unaweza kuondoka na Mali zako zingine ambazo hata hazihusiani kabisa na wizi.

Mimi kwa mara ya kwanza nimekutana na huu msala nimenunua tv nch43 nimenunua ikiwa mbovu kioo ili nivune spea almanusura inipeleke ndani.

Japo muhusika au mwenye Mali kasema ilikuwa imevunjika kioo hivo hivo.

Pia nilicho shukuru mwizi ni WA ndani ya familia.

Je, Uliwahi kutana na huo msala na uliishaje?

Na pia kunaweza kukwepeka? Au ni ajali tu inamkuta mtu yoyote.
 
Lazima receipt, historia, kabla ya kununua kitu, na kama nataka ku take risky, sitakuwa na connection yeyote na Muuzaji baada ya kununua, ila vitu kama:

- Simu

Lazima receipt, na Bora sana ikiwa dukani, ila kununua simu used mtaani kwa mtu usiyemjua na hawa Police ambao uchunguzi na upelelezi ni kipigo, utafia mahereza.
 
Usijaribu tena man.. ni risk sana...tena hivi vitu vya kununua mikononi mwa watu tena bei rahisi ni risk sana...
 
Huu msala omba tu usikukute aisee unaweza kuondoka na Mali zako zingine ambazo hata hazihusiani kabisa na wizi.

Mimi kwa mara ya kwanza nimekutana na huu msala nimenunua tv nch43 nimenunua ikiwa mbovu kioo ili nivune spea almanusura inipeleke ndani.

Japo muhusika au mwenye Mali kasema ilikuwa imevunjika kioo hivo hivo.

Pia nilicho shukuru mwizi ni WA ndani ya familia.

Je, Uliwahi kutana na huo msala na uliishaje?

Na pia kunaweza kukwepeka? Au ni ajali tu inamkuta mtu yoyote.
Tanzania hii, hasa mijini, ni rahisi kununua vitu vya wizi bila wewe kujua kuwa ni vya wizi.
Unaweza kununua bidhaa dukani kihalali kabisa, lakini kumbe ziliibwa kutoka mahali kwingine.

Unaweza ukanunua mahindi au mihogo ya kuchoma, au nazi, kumbe huko vilikotoka, vimeibwa kutoka mashamba ya jirani. Si kila kilichopo sokoni kimefika pale kihalali asimilia 100.
 
Back
Top Bottom