Umeshawaandaa watoto wako kuja kutawaliwa na Watoto wa watawala wa sasa?

ANAUPIGA MWINGI

JF-Expert Member
Apr 14, 2022
389
753
Haina ubishi kwamba watoto wa watawala wa sasa ndo watakao kuja kutawala watoto wetu, hii iko wazi, watawala upigaji wanao fanya ni kwa faida ya watoto wao ili waje kutawala baadae.

Hawa watawala kwa sasa watoto wao wanasoma shule za kiwango cha juu, utawakuta International school, utawakuta Kenedy House kule Arusha, na huko wanaenda kuvuna Exposure za kutosha na network ambazo watazitumia kuja kutawala watoto wetu.

Angali watoto wa Viongozi wengi walio pita ndo hao kwa sasa wanatutawala, na hawa waliandaliwa kwa kila kitu.

Bahati mbaya sisi watawaliwa tunajidanganya eti watoto wetu wanasa Englisha Medium wanaongea Kingereza, hakuna kitu pale wewe waandae kusaikolojia tu waje kutawaliwa na watoto wa watawala wa sasa.

Ufisadi unao fanyika kwa sasa ni watoto wao wanawekewa Benki, hizi zitakuja kuwasaidia kwenye harakati za kutaka kutawala watoto wetu, Sisi tuendelee kushangilia ufisadi tu ila watoto wetu watakuja kutulaumu sana kushindwa kuchukua hatua.

Pesa zinazo pigwa sio za kujemga majumba hapana hizi ni pesa nyingi sana na watoto wannawekewa benki hasa huko nje na zitakuja kuwasaidia sana,
 
Back
Top Bottom