Kisambo
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 845
- 514
Kibao hicho ambacho kitakuwa Hewan Leo kweny vitu vya Radio na Mitandao ya Kijamii!
Haya hapa ni baadhi ya Mashahiri yanayosomeka kweny kibao hich akionekana ku wa Diss watu weng sana!
=======
THE TRUE BOY IS IN THE BUILDING!
Wimbo mpya wa Mipasho (Diss track) kutoka kwa msanii 'mtata', Ney wa Mitego umesikika Live kwa mara ya kwanza kupitia kipindi cha XXL.
Katika wimbo huo uitwao 'Shika Adabu Yako', Ney amewaumbua kwa kuwataja majina wasanii na watu maarufu nchini akianika ubovu wa matendo yao na kuwataka wabadilike.
Kuonyesha anajua anachokifanya, msanii huyu anayejiamini kupitiliza, ametamka wazi ndani ya wimbo huo kuwa hatishwi na chochote na kuwataka wenye ubavu waende kushitaki kokote kwani yeye hana cha kuhofia.
Itakumbukwa kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Ney aliandika baadhi ya mashairi ya wimbo huo na kusema kuwa huu wimbo ni wa kusikiliza getto kwani akiutoa patachimbika!
Hata hivyo, pengine kutokana na athari za mikwara ya hapa na pale kutoka kwa wasanii haswa wa Bongo Movie waliosoma mashairi hayo kutaka kumpeleka mahakamani kwa madai ya kudhalilishwa, Ney ameamua kuupeleka hewani na kutoa picha huenda ameona kama Mbwai iwe Mbwai tu!
Miongoni mwa vijembe vinavyopatikana kwenye wimbo huo ni;
Msanii Ray kujifanya Mkongo kwa kununulia mkorogo fedha zinazotokana na mauzo ya movie zake na kuishi kwao hadi sasa, Bongo Movie imekufa kufikia hatua wasanii wa kike wa filamu kutaka kuimba km snura na shilole, Niva kuishi kwa mademu na huku akimiliki gari ya M10 wakati hana getto, wanafunzi wa chuo kuishi maisha ya anasa na kupoteza dhana ya usomi. Wadada wengi wa mjini na kutovaa chup**, biashara?
Hakuishia hapo, alihamia kwa BASATA, kwa kuwashangaa wanavyoshindwa kufanya kazi yao kwa weledi na kuishia kuwafungia wasanii nyimbo bila kujua ugumu wanaopitia..
Pia, akaendelea na wadananda kwa kumtaja Shetta kuwa anaringishia gari ya kifahari aliyohongwa na Chief Kiumbe kwa kujitapa 'My new ride', Ommy Dimpoz kuhusishwa na Ushoga kitaani, DJ Choka kuwa bize na bata bila kujali familia huku hana hata godoro la kulalia.
Mimba ya Wema Sepetu ni ya kweli au kiki za msimu? Na anamshauri aangalie umri unaenda asiendekeze kiki kwani mwishowe ataitafuta Kiki hadi kwa FID Q.
Serikali ya Magufuli nayo haikuachwa...
Usikilize hapa