Umeshachagua mrithi wa simu yako?

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Hivi unajua kwenye simu zetu unaweza kumchagua mtu awe mrithi wa simu yako ikitokea umekufa ataweza ku access baadhi ya taarifa zilizopo kwenye simu ? Najua wengi hawajui hii.

Kwenye simu zetu Kuna mambo mengi chukulia Kuna picha muhimu umepiga na familia, videos Je ndo zipote baada ya wewe kufa?

Hapana Google & apple wametengeza mfumo wa kuweza kupata baadhi ya taarifa kuhusu marehemu kupitia simu yako.

Ikiwa unahitaji ndugu, jamaa, rafiki , aweze kutumia Akaunti au data zilizopo ndani ya simu yako basi inabidi uweke hii feature On au hutaki ku enable tunajua simu yako unatumia kwenye vitu vya anasa tu acha bhana.

Wapwa si unajua Teknolojia ni Yetu sote basi makala hii ni yako

Kwenye iphone Kuna kitu kinaitwa legacy contact, ni feature ambayo itakusaidia kuweza kuchagua mrithi wa kutumia baadhi ya taarifa zako zilizopo mtandaoni Yani inampa ruhusa ya kuweza kutumia simu yako baada ya wewe kufa.

Kwa watumiaji wa iphone fanya hivi ingia setting >>chagua sehemu name, apple id >> password & security >> legacycontact >>chagua add legacy contact Kisha fuata maelezo utakayopewa.

Watakupa miaka mitatu kuweza kutumia Akaunti ya marehemu baada ya apo itafutwa wanaamini utakua tayari umeshaweza kuhamisha baadhi ya picha, videos ambazo ni kumbukumbu muhimu.

Kwa watumiaji wa Android unahitaji ku enable hii feature inaitwa inactive Google account >> ingia kwenye Google Akaunti yako Kisha >>data & privacy>> shuka chini utaona neno more options>> chagua make plan for digital legacy ingia hapo

Utaweza kufuata maelekezo watakayokupa hatua kwa hatua.

Vipi umechagua watu muhimu wa kutumia Akaunti yako baada ya kufa au kikubwa Kila mtu apambane na Hali yake ?View attachment 2656798View attachment 2656797
Android-Legacy.jpg
legacy.jpg
 
Ahsante sana kwa somo hili mkuu, sikuwa nafahamu. Ngoja niingie kwa google account nifanye activation. Ila sasa hataweza kuitumia simu mapema hivi kabla sijafa? Yaani hataweza kuwa anaona data zangu latest?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom