Umepoteza thamani ya utu wako

Umepoteza thamani ya utu wako

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,144
Reaction score
166,078
KAMA UNA WALAU ROBO YA HIZI SIFA BASI UMEPOTEZA THAMANI YA UTU WAKO

1. Unaisoma hii status ukaipenda. Ukaenda kuibandika kwako bila kutaja mahali ulipoiiba.

2. Unaye mwanamke mzuri, aidha ni mkeo ama mchumba ama mpenzi hata siku moja hujawahi kumtumia meseji ya kumsifia alivyo mzuri, lakini kila siku hukosi kuwamwagia sifa wanawake wengine jinsi walivyo wazuri. Vivyo hivyo, una mumeo ama mchumba ama tu mpenzi, hata siku moja hujawahi kumsifia juu ya utanashati wake. Lakini kutwa kucha huishi kuwasifia mabrazameni wengine.

3. Kila siku unashinda facebook na kucomment kwenye status za wengine lakini mpenzi wako akiweka status hata like tu huweki.

4. Kila siku huchoki kutembelea vituo vya watoto yatima ama wagonjwa hospitali wakati una ndugu zako ambao ni yatima hata shati tu hujawahi kuwanunulia. Una rafiki yako umesikia anaumwa hata hujawahi kwenda kumjulia hali.

5. Ukisikia jamaa fulani ana kipaji hukosi kwenda kumsapoti wakati una ndugu zako kibao wenye vipaji lakini huna time nao.

6. Umepata digrii yako sijui ni ya ngapi na ni siri yako moyoni kuwa ulichojoa mara kibao kwa mhadhiri ili uipate lakini bado unajitamba kuwa wewe ni msomi.

7. Kutwa nzima unalalamika kuwa nchi hii ina mafisadi ndiyo maana ni masikini wakati wewe hata ukitumwa ukanunue kitu cha elfu kumi tu lazima kuna buku utapiga panga.

8. Bingwa wa kuwapeleka washikaji outing lakini una mpenzi wako hata siku moja hujawahi kwenda naye japo tu Coco beach akale mihogo naye akipulizwa na upepo wa bahari ya Hindi.

9. Una miaka kadhaa hujawahi kwenda kwenu kuwajulia hali ndugu zako lakini kila mara unatupia mapicha facebook ya mahali ulipopanga na kuandika ‘home sweet home’.

10. Una gari maridadi kabisa linang’ara ajabu ndani full maunyunyu huku mwenyewe umepiga pamba za kufa mtu lakini nyumbani kwako ni kuchafu ile mbaya una vyombo vichafu umevirundika hadi vimetengeneza utando. Ama ni binti maridadi una make-ups kali utadhani una ubia na viwanda vya maurembo lakini nyumbani kwako ni mchafu ajabu.

11. Wewe ni mwanaharakati wa usawa wa kijinsia, kila siku tunakuona kwenye majukwaa na vyombo vya habari ukitetea usawa wa kijinsia kwa nguvu zote lakini nyumbani kwako una msichana wa kazi ambaye unamkandamiza ile mbaya na hakumbuki hata mshahara wake wa mwisho ulimlipa lini.

12. Kila siku unasema wewe ni mdau wa mpira huishi kushabikia timu za mamtoni na haya maSimba na maYanga lakini mtaani kwenu kuna majanki wana vipaji ile mbaya wanachezea chandimu umeshindwa hata tu kuwanunulia mpira japo wa Kichina.

13. Wewe ni binti upo shule unakubali kuhongwa Galaxy S4 ama Blackberry Bold na sijui nini na nini halafu kula yako shule ni ya shida kweli ila unaona ufahari kuwa na simu kali.

14. Wewe ni baba mtu mzima kabisa lakini unatembea na vibinti vidogo vidogo tu halafu kila siku ukiwa kwenye mawarsha na makongamano unashika bango kuwa adhabu iongezwe kwa wabakaji wote. Unasahau kuwa huna tofauti nao.

15. Wewe ni msanii aidha wa movie ama muziki. Ukipita mahali full madharau kwa watu halafu kila siku unalalamika Wabongo hawanunui kazi zenu. Watanunuaje wakati hela zao ndizo zinawafanya wadharauliwe?

16. Wewe ni mwanablogu lakini unaiendesha blogu yako kwa kuweka picha za utupu ama kuandika udaku usio na akili juu ya maisha ya watu. Yaani unajisikia raha kupata vijisenti kwa kuvuruga maisha ya watu wengine.

17. Rafiki yako anakuamini anakusimulia siri zake halafu wewe unakwenda kumsimulia mtu mwingine. Ama mtu anakusimulia matatizo yake wewe unayageuza bango.

18. Kingereza chako ni cha magumashi lakini unaona fahari kuzungumza mbele za watu nawe uonekane wamo wakati Kiswahili kipo tu stand by kwa ajili yako.

19. Ni binti na unaishi kwako lakini kila siku unakula magengeni kwa sababu eti unaona uvivu kupika wakati huo huo unasema unataka upate mume bora. Huyo mumeo utamlisha vyakula vya magengeni? Yaani chipsi mishkaki halafu waweke kila kitu?

20. Hata siku moja hujawahi kupiga kura halafu kila siku unawalalamikia viongozi wabovu. Ulitaka viongozi wazuri waletwe kwa uweza wa Roho Mtakatifu?



©Fadhy Mtanga
 
22. Kama umeo na kuolewa halafu bado unapiga mzigo beki tatu au mchepuko, basi wewe ni
popoma uliyekubuhu, inabidi utubu.
 
23.unalilia mabadiliko kipindi wewe mwenyewe hujaanza kubadilika...badilika kwanza nawewe ni sehemu ya taifa
 
18. Kingereza chako ni cha magumashi lakini unaona fahari kuzungumza mbele za watu nawe uonekane wamo wakati Kiswahili kipo tu stand by kwa ajili

mwanzo wa kutojua ndiyo mwanzo wa kujifunza....onyesha ujinga wako kwani ujinga ili usaidiwe...bora kujaribu kuliko kutojaribu
 
unalalamika juu ya ugumu wa maisha na bado kutwa unashinda nyumbani umelala
 
Back
Top Bottom