"Oa! Ili usije ukawa unawatazama tazama hawa wanafunzi wetu wa kike" akaendelea na kusema "Haya chukua fedha hizi milioni 3 mkabidhi Mwalimu wako, halafu mwambie asije akazitumia kutolea mahari" alisikika Mh. Rais Magufuli akimwambia Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Namanyere.