Umenipata Msiba!!

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Nimezamishwa kinani, kwenye lindi la huzuni,
pakushika sipaoni, mwenzenu ni simanzini,
Nina uchungu moyoni,limenikuta jamani,
Umenipata msiba.

Mwana kukuza nyumbani, na vyuoni masomoni,
Nikamfunza kanuni, za kuishi maishani,
Za kuheshimu jirani, na wakubwa majiani,
Ametoweka.

Kama mvuke wa chai, mwanangu amenihini,
umemtoka uhai, sijui nifanye nini,
Leo mfu siyo hai, amelala kitandani,
Kifo kimemzingira.

Nyumba yote ni vilio, waja hawasikizani,
Alikuwa kimbilio, la kwangu na majirani,
Kweli mola atakalo, hutokea dunia,
Mwanangu nakulilia.

Najipangusa machozi, ni mkiwa wa wakiwa,
Lilikuwa pandikizi, mwenye tabia muruwa,
Leo hii hajiwezi, hakuna analotambuwa
Umenipata msiba!!
 
nilistuka niliposoma title kumbe mpoto yuko kazini, kazi nzuri hata hivyo!
 
Ciello na nitonye nimefiwa kweli na mtoto mwenye miaka 30. sisi wengine kila kitu cha hisia kinaelezeka vizuri kwa ushairi!! Kwani na sisi washairi hatufiwi kama wanamuziki ambao wao hutumia muziki kuelezea hisia zao?
 
Last edited by a moderator:
mkuu Kigarama pole sana ndiyo njia hiyo!samahani pia nilidhan ni shairi haikuwa lengo langu kukudhihaki.Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu.
 
Last edited by a moderator:
mkuu Kigarama pole sana ndiyo njia hiyo!samahani pia nilidhan ni shairi haikuwa lengo langu kukudhihaki.Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Ameen!! ndiyo njia yetu sisi sote yeye katangulia sisi tuko nyuma yake!!
 
Pole sana Kigarama! Ila kwa wale watani watafikiri ni shairi.

Pole sana kwenye kipindi hiki kigumu na MUNGU ampe mwenetu Mwanga wa MILELE!
 
Ciello na nitonye nimefiwa kweli na mtoto mwenye miaka 30. sisi wengine kila kitu cha hisia kinaelezeka vizuri kwa ushairi!! Kwani na sisi washairi hatufiwi kama wanamuziki ambao wao hutumia muziki kuelezea hisia zao?

Mkuu pole sana Mungu akupe nguvu kwenye kipindi hiki kigumu
 
Last edited by a moderator:
Kiongozi Kigarama,Pole sana mwanajamvi mwenzetu.
Mtoto wa miaka 30 hakika ulimlea kwa upendo na kujitoa kwingi.
Mungu akufariji na akupe nguvu ya kustahimili.
 
Last edited by a moderator:
Mtoto wa miaka 30? Si mchezo.

Shkamoo Kigarama na pole sana kwa pigo hili kubwa. Mungu akutie nguvu na akupe moyo wa subira.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa..... Jina lake na lihimidiwe.

RIP kijana wetu.
 
Na mimi niamkie.
Me Kingwangwa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom