Umemsikia Davey ? Je wasemaje wewe ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umemsikia Davey ? Je wasemaje wewe ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Oct 26, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Date::10/26/2009'Huu si wakati wa kubeza Kilimo Kwanza'[​IMG]Na Mwandishi Wetu

  MWENYEKITI wa Mtandao wa Wadau wa Kilimo wa Asasi za Kiraia (Ansaf), James Davey amesema huu si wakati muafaka wa kuanza kukosoa dhana ya "Kilimo Kwanza" na badala yake utumike katika kufanikisha mapinduzi ya sekta hiyo muhimu nchini.

  Davey, ambaye pia ni mkurugenzi mkazi wa shirika la Concern, aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam akisema: "Tunafurahi kuona dhamira njema ya serikali katika kuendeleza kilimo... naona kuna fursa nzuri hata kama kuna kasoro kadhaa, lakini huu ni msingi na mahali pazuri pa kuanzia."

  Davey, ambaye alikuwa akieleza yaliyojiri katika mkutano wa tatu wa mwaka wa mtandao huo uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni, alisema kwamba mkutano huo umeainisha mapendekezo manne yatakayowezesha mafanikio ya dira ya Kilimo Kwanza.

  Akieleza mapandekezo hayo Mjumbe wa Ansaf, Salum Shamte alisema kwamba lengo la kwanza ni uratibu wa tasnia ya kilimo katika ngazi ya wilaya ambako jukumu la msingi ni kuwaunganisha wakulima na asasi za kiraia sawia na rasilimali watu na taaluma.

  Alisema nyingine ni kuwezesha uendelezaji wa mlolongo wa kuongeza thamani akisema kwamba umefika wakati kwa sekta ya kilimo kulenga zaidi masomo badala ya kuishia katika uzalishaji pekee.

  Azimio jingine la mkutano huo lilikuwa ni kuboresha ubia baina ya taasisi binafsi na za serikali akitoa mfano wa Mipango ya Kuendeleza Kilimo Ngazi za Wilaya (Dadp) inavyotoa fursa ya kushirikishwa kwa sekta binafsi, lakini ikikabiliwa na tatizo kubwa la maofisa wa ugani ambao wapo katika sekta binafsi.

  Alisema jambo jingine muhimu ni kuwa na mipango ya kimkakati ya muda mfupi, wa kati na mrefu ya kuendeleza kilimo hasa katika ngazi za wilaya. "Katika hili ndipo utekelezaji mzima wa dhana ya Kilimo Kwanza unapokuja. Kubadili dhana ya kuendeleza kilimo kutoka kile cha kawaida cha kujikimu na kuwa cha kibiashara kwa kukiongezea thamani," alisema Shamte ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Katani Ltd.
  Tuma maoni kwa Mhariri
  Facebook
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Huyu ni mshika dau hivyo hawezi kuwa objective.

  Ni sawa na kumuuliza mwenyekiti wa CCM kuhusu ufanisi wa CCM, unategemea jibu lakini objectivity is another matter.

  Muhimu kumsikia anasemaje, lakini process kila kitu with the above in mind.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Asante kwa kunifumbua macho kumbe CCM wamejipanga zaidi heee. Duh hawa jamaa bwana .Sasa yeye Kilimo atakifanyia Dar ama kwenye nyumba ya mikutano Dar ?
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  HII NDIO CONCERN WORDWIDE Our programmesOur work focuses on education, emergencies and health, livelihoods, HIV and AIDS.EducationWith 113 million children of primary school age not enrolled in school, Concern is focused on providing basic education to those who need it most.EmergenciesConcern aims to respond to emergencies as they arise. We also work to reduce the frequency of disasters.HealthConcern recognises the importance of nutrition and a safe environment in the promotion of good health.Livelihoods“Livelihoods” means a person’s ability to earn a living. Our livelihoods work is fundamental to what we do.HIV and AIDSOver 40 million people around the world are now living with HIV. Among these, more than 95% live in developing countriesWanaganga njaa tu hawa sioni wanakujaje kwenye kilimo kufikia kusema hayo majambo, HAKI ARDHI wako wapi mbona kimya kwenye hii issue????????
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Msamiati sahihi mkuu ni "mdau" - siyo "mshika dau." which was literal translation of "stakeholder"..( things have changed since....)
   
Loading...