Umeme wazidi kumkaanga Ngeleja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeme wazidi kumkaanga Ngeleja

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Nov 5, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,461
  Likes Received: 81,711
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Umeme wazidi kumkaanga Ngeleja
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 05 November 2011 15:14
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Waandishi Wetu
  Mwananchi

  UJUMBE wa Serikali ulioongozwa na Waziri wa Nishati na Madini, Willian Ngeleja jana ulipata wakati mgumu mbele ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wa mpango wa dharura wa kuiondoa nchi gizani.
  Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Dar es Salaam zinasema, wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli (CCM), January Makamba hawakufurahishwa na kile walichokiita "kasi isiyoridhisha" ya utekelezaji wa mpango huo.

  Mpango huo ni ule uliowasilishwa na Ngeleja katika Mkutano wa Nne wa Bunge la 10 Agosti 13, mwaka huu ukibainisha mipango ambayo inatakiwa kuzalishwa kwa megawati 572 ifikapo Desemba 31, mwaka huu.

  Kilichowachefua wabunge ni taarifa iliyowasilishwa na Ngeleja ikionyesha kukwama kwa baadhi ya mipango, ikiwa ni pamoja ahadi ya kupata kiasi cha megawati 150 za umeme kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

  Inaelezwa kuwa licha ya NSSF kuliahidi Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuwa litafua umeme huo, hadi sasa mitambo haijapatikana.Taarifa hiyo ambayo gazeti hili limeiona, inaeleza kuwa NSSF limeenguliwa kutoka katika orodha ya kampuni zinazotarajiwa kuzalisha umeme wa dharura na badala yake Serikali kupitia Tanesco imeanzisha mazungumzo na Kampuni ya Jacobsen ili kuzalisha megawati 100.

  Awali, kampuni ya Jacobsen ilikuwa imeingia mkataba na Tanesco kwa lengo la kuzalisha kiasi cha megawati 250 ifikapo Juni 2012, lakini mkataba wa sasa unawalazimisha kuzalisha megawati 100 ifikapo Desemba na megawati 150 ifikapo Juni, mwakani.

  "Kutokana na kuchelewa kupatikana kwa mitambo hiyo ya kwa wakati, utekelezaji wa mradi huo huenda usikamilike ndani ya kipindi cha mpango wa dharura. Hata hivyo, NSSF inaendelea na mchakato wa kupata mitambo kama walivyoahidi," inaeleza sehemu hiyo ya taarifa ya Ngeleja na kuongeza:

  "Baada ya kuchelewa kupatikana kwa mitambo hiyo ya NSSF, Serikali kwa kushirikiana na Tanesco iliamua kufanya mazungumzo na mkandarasi wa mradi wa Jacobsen kwa nia ya kuharakisha kukamilisha utekelezaji wa mradi ifikapo mwanzoni mwa Desemba 2011 badala ya Juni 2012".

  Kauli ya NSSF
  Hata hivyo, Meneja Uhusinao wa NSSF, Eunice Chiume alisema jana kuwa shirika lake lilikuwa likiendelea na mchakato wa kuwezesha uzalishaji wa umeme kama lilivyoahidi na kwamba halina taarifa za mabadiliko hayo.

  "Sisi tulifungua zabuni tarehe 25 mwezi uliopita (Oktoba), na kampuni tatu zilijitokeza kinachoendelea sasa ni kupitia documents (nyaraka) za zabuni hizo na taratibu zikikamilika mshindi atajulishwa hivyo kuleta mitambo nchini," alisema Chiume na kuongeza:

  "Ilikuwa lazima tujiridhishe na hicho ndicho kilichotokea, kwani awali, tulidhani tungeweza kupata mitambo bila kutangaza zabuni lakini baadaye ilibidi timu iundwe ya wataalamu kumi na moja kutoka ofisi yetu na wadau wote, hili hata Tanesco na Wizara ya Nishati wanalifahamu maana walikuwa sehemu ya timu hii iliyoweza kutufikisha katika hatua tuliyopo."

  Alisema kutokana na mchakato huo kuchelewa kulikuwa ni dhahiri na kwamba heri kuchelewa kulioko kuliingiza taifa katika hasara ya kutapeliwa katika sekta hiyo ya umeme kwa mara nyingine.
  "Sababu za kuchelewa ni genuine (za msingi) kabisa wala hapa hakuna cha kutulaumu, tulikwepa kutapelwa nchini Marekani kutokana na umakini wetu, taratibu za ununuzi pia zinatubana kwa hiyo umeme utapatikana kuchelewa si kwamba tumeshindwa,"alisema.

  Mbele ya Kamati
  Taarifa hiyo ya Serikali iiliyowasilishwa mbele ya kamati hiyo inaonyesha kuwa hadi sasa kiasi cha umeme unaoigizwa kwenye gridi ya Taifa kutokana na mpango huo wa dharura ni megawati 217 tu sawa na asilimia 37.9 ya matarajio ya megawati 572.

  Pia kiasi hicho cha umeme ni sawa na asilimia 46 ya megawati 462 ambazo kwa mujibu wa ratiba ya Serikali iliyotolewa katika Bunge lililopita zilipaswa kuwa zimeanza kuzalishwa tangu mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.

  Umeme huo ni kutoka IPTL megawati 80, Aggreko megawati 100 na Symbion megawati 37.

  Taarifa zilizopatikana zimeeleza kuwa taarifa ya Ngeleja kwa kamati hiyo ilizua mjadala mkali kwa sababu haikuonyesha matumaini ya kutatua tatizo la umeme nchini, kama alivyoahidi bungeni.Wabunge walihoji kwa nini Ngeleja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda walitoa bungeni ahadi ambazo walikuwa wakifahamu fika kwamba pengine zisingeweza kutekelezeka katika muda uliotajwa? Tuliwahoji sababu za kutoa ahadi kubwa hali wakiwa hawana uhakika kwamba wangeweza kutekeleza ahadi hii," alisema mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo ambaye aliomba kutotajwa kwa kuwa si msemaji wa kamati.

  Kwa mujibu wa kalenda ya utekelezaji wa mpango wa dharura iliyotolewa Bungeni na Serikali, NSSF na Symbion ndizo zinazoonekana kuwa nyuma kiutekelezaji kwani hadi sasa walitakiwa kuwa wameingiza kwenye gridi ya taifa kiasi cha megawati 245.
  Kalenda hiyo inaweka bayana kuwa Symbion walitakuwa kuwa wamengiza megawati 145 na NSSF megawati 100, kiasi ambacho kilitarajiwa kuwa kimeingizwa kati ya Septemba na Oktoba, mwaka huu.

  Makamba anenaMwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba alisema jana kwamba: "Ni kweli tumekutana na Serikali kwa ajili ya kupata taarifa za mambo mengi na siyo umeme tu. Tutatoa taarifa wakati mwafaka. Msimamo wa Kamati yangu unafahamika, sisi tulishasema kwamba tunachotaka ni umeme, watu tupate umeme shughuli za uchumi na kijamii ziendelee, kwa hiyo pamoja na kwamba kuna progress (hatua) zimepigwa, tumeendelea kusisitiza hilo kwamba umeme upatikane."

  Mbunge huyo wa Bumbuli (CCM) alisema kamati yake pia inatafakari uwezekano wa kuwa kuwa na Mamlaka ya Udhibiti ya Masuala ya Nishati tofauti na Mamlaka ya sasa ya udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) na Shirila la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

  "TPDC wanakuwa wadhibiti lakini wakati huohuo nao ni washiriki katika sekta hiyo, Ewura wanafanya kazi za sekta ya maji na huko ndiko wameegemea sana, sasa tunadhani kwamba tukiwa na mdhibiti wa nishati tu, itatusaidia mambo mengi na kupunguza malalamiko mengi ambayo yanatokea sasa,"alisema Makamba.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Afukuzwe tu uwaziri...hadithi zimezidi.
   
 3. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  wizara ya nishati ni kama vile haina waziri mwenye dhamana.
   
 4. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Anasubiri nini kuachia ngazi!!
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,461
  Likes Received: 81,711
  Trophy Points: 280
  Analindwa na fisadi Rostam, hivyo msanii hawezi kabisa kumgusa.
   
 6. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nani amfukuze?
  Cha kufanya watanzania ni kumfuta kazi Kikwete!
   
 7. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hizi mamlaka nazo zimezidi! Kama vp nazan tuanzishe na mamlaka ya kudhibiti mafisadi,pccb wao wabaki na rushwa ndogo ndogo kama za mahakimu wakazi mana ndo wanazoziweza! Mafisadi hawawezi
   
 8. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #8
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Ngeleja ni kijana sana na hana experience ya kuendesha Wizara kama ile. Huku umeme balaa na kule madini ndiyo balaa zaidi.

  Angekabidhiwa Waziri ambaye kidogo ana uzoefu wa kufanya maamuzi magumu na kutekeleza sera zinazoeleweka.
   
 9. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2011
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Umeonaeee
   
 10. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #10
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Sijui serikali nzima ndivyo wanavyofanya kazi hivi maana inasikitisha sana na Rais hasemi kitu. Hii inaonyesha Rais anaridhia utendaji kazi wa Ngeleja. Kwani hakuna watu wengine wanaoweza kuchapa kazi ama kuna siri ya ufisadi humo?
   
 11. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #11
  Nov 5, 2011
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hayo ni mawazo mgando. Hii nchi inayumbishwa na hao wazee wanaojilimbikizia vyeo vingi serikalini. Kuna wataalamu wengi tu vijana ambao wakipewa nafasi kama hizo sidhani kama utaona madudu kama haya. Ngeleja yupo kwa ajili ya maslahi ya watu binafsi ambao kwa namna moja ama nyingine lazima atekeleze kile ambacho mabwana wake wanakihitaji na wala si uzoefu.
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hizi kamati nazo ni kama hazina meno!
   
Loading...