UMEME WAONGEZEKA KWA 135% wananchi wataabika

UMEME WAONGEZEKA KWA 135% wananchi wataabika

Niwapeni husahuri, kama mtu unajiweza basi nunua heater ya maji ya moto ya solar, ac ya solar na umeme inapunguza 30-60% ya umeme na ki windvane cha 600w hapo umeme wa elfu 10 utakutosha kabisa full kiyoyozi na maji ya moto mda wote.

Vinginevyo basi ni swala la modification ya mita tu hakuna zaidi.

Pesa yenyewe inakwenda kwa walioshiba. Heri tukawane sisi wanyonge tu.

Sent from my GT-I9300
 
Wewe unaweza kutusaidia kama tukipeleka hili dukuduku mbele, maana umeweka namba za kwenye risiti. Wengine tunaongea yani kienyeji enjeji tu sijui nina friji mbili sasa zinatumia siku mbili sijui nilikuwa nina mashine ya kukaangia dagaa siku hizi umeme unakata sishibi ...please!

Kila transaction ya LUKU inakuja na risiti inayoonyesha units ulizonunua na hela zilizotumika, statistics za vyombo vyako vya ndani na matumizi yako ya ndani sisi hatujui, compare numbers from the receipt! Mfumo wa elimu ufumuliwe:Edward Lowassa!

Unaweza kuwa msemaji mzuri wa tanesco zaidi ya yule dada yako.
 
imebid niangalie earth wire leo, na kuwabana wapangaj wenza maana ime shoot ghafla kutoka 80000 to 180,000pm
 
Hiyo ndio nchi ambayo mpaka ikulu yataka profit katika kuwapa wanachi huduma . i.e kampuni ikulu. Tuna deni la Al Adaiwi (Dowans) then Tumeingia mkataba ya milele na IPTL na wengine ambao price ya umeme wanayouza kwa tanesco ni twice ya price tunayolipia wananchi. So you have to reap eat until your third generation 2150. Sorry Tanzania sina pa kwenda tu ila one day mtalipa tu haya mateso kwa tamaa zenu. Only way to do is to dilute the the depende from those cone company then produce our own and keep the demand from them constant or to have many comapnies to produce electricty and have the autonomy region wise or let us pay huge sum and have inc consequnce and vunja contarc with IPTL dowans and etl. You leaders i hate u.
 
Mimi nafikiri kuwe na uwazi watoe kwenye jarida maalum na vyombo vya habari orodha ya unit na pesa inayotakiwa kulipwa. Orodha hizi pia zibandikwe kwenye vituo vya mauzo. Sasa hv Tanesco wanafanya kila kitu kinyemela na kwa usanii wa kutisha kwa maelekezo ya uongozi mpya wa wizara ambao hauna jipya bali ulaghai. Mgao kinyemela, bei juu kinyemela, kuzima mitambo ya luku kinyemela, nk Nafuu kabisa Ngeleja na kina Mhando walikuwa wawazi. mimi nilikuwa nanunua uniy 678 kwa laki moja kwa matumizi ya nyumbani kwa wk 3 sasa hv napata unit 353 kwa pesa hiyohiyo na umeme unakaa siku 9 au kumi pekee na hapa ndio sielewi unit moja ni shs 300 kwa umeme wa nyumbani? sisi ndio tunalipia wenye viwanda na mabiashara makubwa? manake wao unit moja ni kitu kama shs 80 na kama wamepandishiwa kinyemela itakuwa kwenye mitaa ya shs 100 na si juu sana ya hapo,
 
Mimi nafikiri kuwe na uwazi watoe kwenye jarida maalum na vyombo vya habari orodha ya unit na pesa inayotakiwa kulipwa. Orodha hizi pia zibandikwe kwenye vituo vya mauzo. Sasa hv Tanesco wanafanya kila kitu kinyemela na kwa usanii wa kutisha kwa maelekezo ya uongozi mpya wa wizara ambao hauna jipya bali ulaghai. Mgao kinyemela, bei juu kinyemela, kuzima mitambo ya luku kinyemela, nk Nafuu kabisa Ngeleja na kina Mhando walikuwa wawazi. mimi nilikuwa nanunua uniy 678 kwa laki moja kwa matumizi ya nyumbani kwa wk 3 sasa hv napata unit 353 kwa pesa hiyohiyo na umeme unakaa siku 9 au kumi pekee na hapa ndio sielewi unit moja ni shs 300 kwa umeme wa nyumbani? sisi ndio tunalipia wenye viwanda na mabiashara makubwa? manake wao unit moja ni kitu kama shs 80 na kama wamepandishiwa kinyemela itakuwa kwenye mitaa ya shs 100 na si juu sana ya hapo,
 
Serikali ya mafisadi inawafanya Watanzania wasiwe na namna ya kukabiliana na gharama kubwa za maisha zinazopanda kwa kasi ya kutisha bali kutafuta namna hata kama ni ya kuvunja sheria ili kuweza kumudu gharama hizo. Mwezi mmoja tu gharama zako za umeme zimeongezeka na kwa almost 100%!!!!! duh!!!!

Loh! kumbe! nimeshangaa jana wameniletea bill 25000/= ya mwezi wa 11 wakati kwa kawaida on avarage huwa nalipa 13000/= kwa mwezi! Lipo wapi baraza la kutetea walaji Tanzania? Mbona baraza kama hilo hapo uganda jana wamewapeleka Star tmies mahakamani kwa udanganiyfu?

By the way tokea nianze kupata akili na kupiga kura sijawahi pigia magamba! siku utawala wangu ukifika ntaenjoy maisha kwa sasa wacha tufe wote na mat-shirt, kapelo na kanga viva viva magamba na wapenzi wenu!
 
Nadhani Fastjet imetufumbua macho hebu jiulize nauli ya Dar to Mza hapo awali ilikuwa sh ngapi? Na baada ya kuja fastjet imekuwa sh ngapi? Kwani fastjet yeye hatumii mafuta anatumia maji?.
 
WanaJf habari za asubuhi

Leo nimeona nilete dukuduku langu baada ya kuumia kwa miezi mitatu hivi
Zamani mimi ambaye naishi na mwenzangu tulikuwa tunatumia umeme wa 10,000
kwa mwezi na unabaki(vifaa vya nyumbani ni Fridji,Pasi, Television, Taa za ndani 6, brenda, laptop mbili)

Lakini kwa muda wa miezi mitatu mfululizo kumekuwa na ongezeko la umeme kutoka Tshs 10,000 mpaka Tshs 35,000 kwa mwezi.

Hili ni ongezeko la 130% kwangu mimi, ili ongezeko ni kumbwa sana kwa matumizi ya mtanzania.

Leo katika kuperuzi gazeti la mwananchi (16/12/12) ndio nikakutana na Tangazo la Tanesco lenye kichwa MATUMIZI SAHIHI YA UMEME

Hili tangazo linesema wananchi wameenda Tanesco kulalamika mtumizi ya umeme kuwa makubwa kwa kipindi kifupi kilichopita pamoja na kuwa na vifaa vile vile. Sasa hapa ndio nakajua kumbe sio mimi peke yangu ninayeumia kwa ili wapo wengi.


Swali kwa wanaJF
1. Je na wewe umepatwa na tatizo ilo?
2. Je kwanini Tanesco wamepandisha umeme kimya kimya?
3. Je nifanyeje ili niweze kukabiliana na hawa tanesco maana Jumatatu naenda kwenye office zao kupeleka haya matatizo.

Hilo tangazo linasemaje mkuu maana ninakabiliwa na tatizo kama lako lakini sijapata fursa ya kujua tatizo ni nini
 
Kumbe! Nilikua nikishangaa kwanin zitumike 3units per day!? Wakat matumiz ni taa 5, tv, na frij mwisho saa 4 uck havikeshi on!
 
Nazichanga mdogomdogo ili niweke Umeme jua wa uwezo mkubwa baasi na sasa nafikiria kuchimba kisima cha maji na kuvuna maji ya mvua zijazo ili nao sijui Nuwa sijui Dawsco/Dawasa (kazi kubadili majina utafikiri ndio wanaongeza tija kwa kubadili hayo majina) iwe mwanzo na mwisho kubisha hodi kwenye geti langu
 
Back
Top Bottom