UMEME WAONGEZEKA KWA 135% wananchi wataabika

UMEME WAONGEZEKA KWA 135% wananchi wataabika

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2010
Posts
7,263
Reaction score
685
WanaJf habari za asubuhi

Leo nimeona nilete dukuduku langu baada ya kuumia kwa miezi mitatu hivi
Zamani mimi ambaye naishi na mwenzangu tulikuwa tunatumia umeme wa 10,000
kwa mwezi na unabaki(vifaa vya nyumbani ni Fridji,Pasi, Television, Taa za ndani 6, brenda, laptop mbili)

Lakini kwa muda wa miezi mitatu mfululizo kumekuwa na ongezeko la umeme kutoka Tshs 10,000 mpaka Tshs 35,000 kwa mwezi.

Hili ni ongezeko la 130% kwangu mimi, ili ongezeko ni kumbwa sana kwa matumizi ya mtanzania.

Leo katika kuperuzi gazeti la mwananchi (16/12/12) ndio nikakutana na Tangazo la Tanesco lenye kichwa MATUMIZI SAHIHI YA UMEME

Hili tangazo linesema wananchi wameenda Tanesco kulalamika mtumizi ya umeme kuwa makubwa kwa kipindi kifupi kilichopita pamoja na kuwa na vifaa vile vile. Sasa hapa ndio nakajua kumbe sio mimi peke yangu ninayeumia kwa ili wapo wengi.


Swali kwa wanaJF
1. Je na wewe umepatwa na tatizo ilo?
2. Je kwanini Tanesco wamepandisha umeme kimya kimya?
3. Je nifanyeje ili niweze kukabiliana na hawa tanesco maana Jumatatu naenda kwenye office zao kupeleka haya matatizo.
 
jibu la swali lako ni kuipumzisha ccm 2015...na mikakati hiyo ianza na kumshawishi mwenzako akubari mabadiliko.....kataa ccm kwa maendeleo na uhuru wa kweli......haya unayoyaona yanafanyika Tanzania pekee duniani kote ambapo viongozi ni madictator wasioona umuhimu wa mwananchi katika mabadiliko......tuliwatoa wakoloni kwa sababu walitunyonya,walitutesa na walizalilisha utu wa mtanzania.....sasa pana tofauti gani na ccm
 
Chakachua mita, vinginevo utaendelea kuumia hawa tanesco hawaambiliki, mi nakula umeme free, kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake, km vp niPM nikupe namba ya kishoka
 
Nani alikuambia uichague ccm mwaka 2005-2010-2015.. Ndo maisha bora hayo au huyaoni
 
aisee..!

wasn't aware kabisa...!mi nikajua kuna mpangaj mwenzangu ameamua kununua hita ili atukomoe....

kumbe !..
 
aisee..!

wasn't aware kabisa...!mi nikajua kuna mpangaj mwenzangu ameamua kununua hita ili atukomoe....

kumbe !..

Mimi nilikuwa nafikri niko peke yangu baada ya kuona tangazo la tanesco leo wakitoa ufafanuzi kwanini umeme umeongezeka
gharama huku matumizi ya vyombo ni yaleyale
 
Nani alikuambia uichague ccm mwaka 2005-2010-2015.. Ndo maisha bora hayo au huyaoni

Kwanini tanesco wanaongeza umeme kinyemela?

Ungezeko liko hivi umezoea kununua umeme wa 20000 labda unatumia siku 25 kwa kipindi cha miezi iliyopita
sasa hivi umeme waa 20000 unatumia kama siku 15
 
Mimi juzi nilienda kununua umeme wa elfu tano wakanipa unit 9.38 kwa maana waliniuzia umeme wa Tsh. 2049, najiuliza hiki kiasi kingine cha 2951 kimeenda wapi wakati pesa yao ya service charge ya mwezi huu wamekwisha chukua au VAT imepanda? Wanajifanya wamepeleka EWURA maombi ya kupandisha umeme, kumbe wamekwishapandisha kinyemela?
 
hivi hakuna njia ya kuweza kuwashitaki, EWURA au mahakamani? tuwapeleke huko washike adabu
 
Wenzio tumechezea Luku tunalipa buku 10 tu kwa mwezi na Tanesco wakitaka kuja tunapigiwa simu anakuja anarekebisha unampa buku 5 safi maisha tambarare! We wachangie tu magamba hao wanunue VX

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Loh! kumbe! nimeshangaa jana wameniletea bill 25000/= ya mwezi wa 11 wakati kwa kawaida on avarage huwa nalipa 13000/= kwa mwezi! Lipo wapi baraza la kutetea walaji Tanzania? Mbona baraza kama hilo hapo uganda jana wamewapeleka Star tmies mahakamani kwa udanganiyfu?

By the way tokea nianze kupata akili na kupiga kura sijawahi pigia magamba! siku utawala wangu ukifika ntaenjoy maisha kwa sasa wacha tufe wote na mat-shirt, kapelo na kanga viva viva magamba na wapenzi wenu!
 
toka lile zoezi lao la kuingiza namba kwenye luku lipite umeme unakwenda sana... Na hili si kwangu tu kila kuna wenzangu 3 nao wamenoti hilo jambo.....
 
Vumilia tu usilalamike lazima uchangie pesa inayoibiwa na mafisadi.

Ila una nafasi ya kuyaondoa mafisadi madarakani mwaka 2015.

Siyo umeme tu unaoibiwa, unaibiwa kila sehemu na wizi mkubwa zaidi ni wa rasilimali zako.
 
Ila JEyKey ivi kwa huomuititir wa vitu unataka ulipe wekundu mara mwisho mimi kulipa umeme wa wekundu ni ziadi ya miaka minne imepita tena kwa vifaa kama ulivotaja
sasa wananipiga 70-80000 kwa mwezi
Ebu ngoja ili bomba la gesi likamilike labda kutakuwa na ahueni
 
Mimi juzi nilienda kununua umeme wa elfu tano wakanipa unit 9.38 kwa maana waliniuzia umeme wa Tsh. 2049, najiuliza hiki kiasi kingine cha 2951 kimeenda wapi wakati pesa yao ya service charge ya mwezi huu wamekwisha chukua au VAT imepanda? Wanajifanya wamepeleka EWURA maombi ya kupandisha umeme, kumbe wamekwishapandisha kinyemela?
Wewe unaweza kutusaidia kama tukipeleka hili dukuduku mbele, maana umeweka namba za kwenye risiti. Wengine tunaongea yani kienyeji enjeji tu sijui nina friji mbili sasa zinatumia siku mbili sijui nilikuwa nina mashine ya kukaangia dagaa siku hizi umeme unakata sishibi ...please!

Kila transaction ya LUKU inakuja na risiti inayoonyesha units ulizonunua na hela zilizotumika, statistics za vyombo vyako vya ndani na matumizi yako ya ndani sisi hatujui, compare numbers from the receipt! Mfumo wa elimu ufumuliwe:Edward Lowassa!
 
Watu wengi tuna malalamiko hayo hayo. Mimi nipo Songea hali ni hiyo hiyo. Nadhani kitu cha kufanya ni [kwa kila sehemu k.m. Mtaani] kujiorodhesha na kuonyesha bill za nyuma 2 au 3 na bill za sasa, kila kila mtu anaweka saini yake. Kisha katika mfumo wa barua inaandikwa Kwa Mkurugenzi Mkuu, ipelekwe ofisi ya TANESCO iliyo karibu. Tukifanya hivyo nchi nzima watajua tumewasitukia. Mfano kama huu hapo chini;

[TABLE="width: 50, align: left"]
[TR]
[TD]Jina
[/TD]
[TD]A/c Nr.
[/TD]
[TD]Bill
za
nyuma
[/TD]
[TD]Bill
za
sasa
[/TD]
[TD]Saini
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
WanaJf habari za asubuhi

Leo nimeona nilete dukuduku langu baada ya kuumia kwa miezi mitatu hivi
Zamani mimi ambaye naishi na mwenzangu tulikuwa tunatumia umeme wa 10,000
kwa mwezi na unabaki(vifaa vya nyumbani ni Fridji,Pasi, Television, Taa za ndani 6, brenda, laptop mbili)


Lakini kwa muda wa miezi mitatu mfululizo kumekuwa na ongezeko la umeme kutoka Tshs 10,000 mpaka Tshs 35,000 kwa mwezi.

Hili ni ongezeko la 130% kwangu mimi, ili ongezeko ni kumbwa sana kwa matumizi ya mtanzania.

Leo katika kuperuzi gazeti la mwananchi (16/12/12) ndio nikakutana na Tangazo la Tanesco lenye kichwa MATUMIZI SAHIHI YA UMEME

Hili tangazo linesema wananchi wameenda Tanesco kulalamika mtumizi ya umeme kuwa makubwa kwa kipindi kifupi kilichopita pamoja na kuwa na vifaa vile vile. Sasa hapa ndio nakajua kumbe sio mimi peke yangu ninayeumia kwa ili wapo wengi.


Swali kwa wanaJF
1. Je na wewe umepatwa na tatizo ilo?
2. Je kwanini Tanesco wamepandisha umeme kimya kimya?
3. Je nifanyeje ili niweze kukabiliana na hawa tanesco maana Jumatatu naenda kwenye office zao kupeleka haya matatizo.

Haiwezekani kwa mwezi wewe na wenzako matumizi yenu yawe 10,000 kwa vifaa hivi ulivyotaja hapa! Endelea kuchakua mita pia endelela kulalamika.
 
Haiwezekani kwa mwezi wewe na wenzako matumizi yenu yawe 10,000 kwa vifaa hivi ulivyotaja hapa! Endelea kuchakua mita pia endelela kulalamika.

Mkuu ndio nakwambia sasa

Na mimi nakuwa kazini lakini matumizi yake ni jion sasa kwanini matumizi yaongezeke ghafla?
 
Tunalipa deni la Richmond/Dawans/Symbion kiaina, chezea magamba wewe!!!!!!!!!!!!
 
Nunua Solar PV system uachane na magumashi haya!! Serikali ipo madarakani kupiga dili mpaka mtapostuka mifuko itakuwa imeshatoboka zamani.
 
Back
Top Bottom