Umeme wa megawati 80 kuanza mwakani

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1583427561257.png

BODI ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) inatarajia kupokea umeme wa mradi wa maporomoko ya Mto Kagera ya Rusumo, unaojengwa katika Kata Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera ifikapo mwaka 2021.

Mradi huo utakapoanza kutekelezwa, utasaidia kutatua changamoto za umeme nchini. Mradi huo unaendeshwa na nchi tatu za Tanzania, Rwanda, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambazo zimeingia makubaliano ya uhitaji wa nishati hiyo kutoka bwawa la mto Kagera.

Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk. Alexander Kyaruzi, alisema mradi huo utanufaisha wananchi kwa kuwa na umeme wa uhakika kutoka kwenye bwawa hilo. Dk. Kyaruzi alisema, mradi huo wa megawati 80, na utagawanywa kwa nchi hizo tatu na kila nchi kupata megawati 27.

Aidha, alisema kwa Tanzania, kituo kikuu cha kuingiza na kusambaza umeme kinaendelea kujengwa katika Kata ya Nyakanazi wilayani Biharamulo, ambacho kitagawa maeneo yote ya ndani na nje. hatua ya kwanza na ya pili kwa uwekaji wa miundombinu ya nchini ya miamba. "Hatua hizo mbili tulizonazo isingekuwa changamoto ya fedha kutoka na matetemeko ya ardhi kwenye makazi ya watu, tungekuwa hatua za ukamilishaji hivi sasa,"alisema George.

Aliongeza kuwa baada ya kukamilika hatua hizo, zitajengwa ofisi za usimamizi wa mradi huo zitakazokuwa zinaangalia ugawaji wa umeme kwa kila eneo la mpaka wa nchi hizo tatu. Mradi huo ulianza mwaka 2017 na ulitarajia kukamilika Februari mwaka huu, lakini kutokana na changamoto za kifedha na matetemeko ya miamba kwenye makazi ya watu, ulisimama. Ujenzi huo unasimamiwa na kampuni za CGCOC na JVJWHC za China.
 
Correction, nchi tatu ni TZ, Burundi na Rwanda. There is no DRC participation in this project.
View attachment 1378047

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom