Umeme wa gesi hatima yake ni nini?

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,903
Taifa Sasa lipo katika mjadala wa umeme wa hydroelectric power ambao n mradi ulioachwa na aliekuwa Raisi wa JMT.

Lakin kabla ya huu mradi, kulikua na project ya umeme wa gesi ambao ulikua katika utekelezwaji na uligharimu taifa kwa habar ya fedha, watu kuvunjiwa nyumba zao nk.

Baada tu ya awamu ya nne kumaliza muda wake na awamu ya tano kujimwambafai Kwa kushka hatamu, ndoto za project hyo ikafia hapo na ndoto za HEP zikachkua nafasi na mpaka Sasa pamoja Kuna mijadala ya hapa na pale inaendelea.

Maswal yangu ni haya:
1). Ni nini hatima ya mradi wa umeme wa gas ambao tayari ulikua umeligharim taifa mabillion ya fedha za watoa jasho?

2). Serikali inashauliwa na nani ambaye kimsingi anapaswa kulaumiwa kwa sababu inaonekana kama hakuna utafiti wa kina juu ya projects za serikal kiasi kwamba kunakua na ukurupukaji unaoligharimu taifa?

3) ile miundo mbinu ( mfano Mabomba) iliyokua imewekwa tayar hatima yake nini?

Mimi yangu ni hayo tu, naomba kuwakilisha!
 
Back
Top Bottom