Hakuna Tariff ya REA mkuu. Tariff zote ni za Tanesco.
Tofauti inakuja kuwa kwenye matumizi ya umeme. Iko hivi
REA ni wakala wa umeme maeneno ya vijijini. Hivyo kazi ya REA ni kusambaza (kuvuta line, kuweka transformer na kufungia umeme) maeneo ya vijijini.
Baada ya REA kufunga umeme mteja husajiliwa Tanesco na hapo mradi hukabidhiwa Tanesco na REA hapo ndio bye bye hawapo tena. Sasa kutokana na matumizi ya umeme kuna Tariff ambazo za majumbani ni T1 ambayo ni matumizi ya kawaida na Tariff 4 ambayo ni watumiaji wa hali ya chini. Wasiozidisha unit 75 kwa mwezi (ambao wengi tuna assume wapo vijijini). Hapa ndio inaibuka hiyo notion yako ya kusema "Tariff ya REA" kitu ambacho sio kweli.
Ikitokea mtu uliwekwa kwenye Tariff 4 ukazidisha manunuzi ndani ya mwezi automatically meter yako inatoka kwenye hiyo Tariff na ukinunua umeme utauziwa kwa bei ya Tariff 1..
Bei ya umeme kwa T4 unit moja ni tshs 100 wakati T1 ni tshs 292