Umeme kupanda kwa 155% January 2012-Ushauri

Mkombozi

JF-Expert Member
Feb 19, 2008
806
426
Wakuu kama mnavyofahamu Tanesco inakusudia kupandisha bei ya umeme January 2012 kwa kipindi cha dharura cha miezi 6.Nashauri watu wote wenye hela zao wanunue umeme wa kutosha miezi 6 December hii kabla haujapanda bei.Unachotakiwa kufanya baada ya kununua ni kwenda kununua umeme kidogo sana ili ulipe service fee ya kila mwezi ambayo sijui ni kwa nini inatozwa..Ni ushauri wa bure
 
THANKS Mkuu kwa ushauri. Ninunue kwa Bulk say 500,000/ ama ninunue wa 100,000/=(??)
 
Hata kama utanunua kwa wingi namna gani itakuwa suluhisho sahihi la tatizo la umeme.

Tatizo la umeme Tanzania liko kwenye uongozi. Viongozi wa Tanzania wamekuwa wakiendesha mambo ya umeme kisiasa sana. Mzingo mkubwa wa gharama za umeme wanabeba wananchi umetoka na sera na mikakati mibovu; na rushwa kwenye kubwa kwenye sekta ya umeme.
 
Bilioni 64 za (1) kujisherehesha, zilizokopwa kumlipa (2) Rastam Aziz kimya kimya, (3) kujiwekea kwa ajili ya kugombea uchaguzi wa wa urais 2015 (kwa huyo mgombea mgongoni ambaye ameonekana vijisenti havijatosha bado) na pia (4) kuwahonga wabunge kupitisha sheria za kunufaisha PROJECT-MEMBE kamwe zisitafutwe kwa njia hii kwenye umeme.

Mpango huu ukitekelezwa ajira zote zitakauka, milango ya viwanda vingi kufungwa na gharama ya maisha kuruka angani, ngojeni mje myaone hata kabla bei ya mafuta na haijawa vingine huko mwakani.
 
Wakuu kama mnavyofahamu Tanesco inakusudia kupandisha bei ya umeme January 2012 kwa kipindi cha dharura cha miezi 6.Nashauri watu wote wenye hela zao wanunue umeme wa kutosha miezi 6 December hii kabla haujapanda bei.Unachotakiwa kufanya baada ya kununua ni kwenda kununua umeme kidogo sana ili ulipe service fee ya kila mwezi ambayo sijui ni kwa nini inatozwa..Ni ushauri wa bure
nani kasema kuwa beiya umeme inaongezeka kwa kiasi hicho? Wao waliomba, Ewura ikafanya tashtit na hawajatoa majibu.
Lakini hata kama wakiongeza, sidhani kama hilo litakwua suluhisho la matatizo yanayowakabili tanesco. Suluhisho la kampuni hii is far beyond electricity tarrifs
 
Poleni sana; mimi nilishafunga solar system; kwa mwanga, tv, computer nk sipati ugonjwa wa moyo ila kwa bei ya mahitaji ya viwandani hakika inatisha, na kwa ongezeko hilo itakuwa balaa.
Kama mchangiaji hapo juu alivyosema, tatizo ni uongozi. Pipa linavuja sana hivyo kila tutakachoingiza kitavuja tu, haliwezi kujaa. Dawa ni kuliziba kwanza na kwa kuwa haiwezekani kuliziba, then tutafute jipya!
 
Hivi mtoa mada una ufahamu wowote ule kuhusu kitu kinachoitwa school fees? kama ungekuwa upo kwenye hilo daraja huwezi kuja na ushauri huu. December ni mwezi wa mateso makubwa kwa sisi wazazi.
 
Hivi mtoa mada una ufahamu wowote ule kuhusu kitu kinachoitwa school fees? kama ungekuwa upo kwenye hilo daraja huwezi kuja na ushauri huu. December ni mwezi wa mateso makubwa kwa sisi wazazi.

Naunga mkono. Yaani kichwa kinaniuma sana nikifikiria SCHOOL FEES!!!!.
 
kwani ni lazima nitumie umeme wao. najipanga kutumia njia mbadala siwezi acha lipa ada na kufanya maendeleo ya maisha kisa ninunue umeme mwingi kuikomesha tanesco.sishindani na wajinga
 
Kazi ya m k w e r e hiyo tutakoma ubishi.

Best wangu yani safari hii mpk afute miaka aliyoibakiza Mi naona atakuwa amejitwinisha sana kodi ya Watanzania lakini yeye aendelee tu kwn kuna siku maombi ya Watanzania itajibiwa na nafikiri haina muda. WAO WANA PESA SISI TUNA MUNGU MWENYE UWEZO WA YOTE!
 
Back
Top Bottom