Umeme kukatika katika, subira tafadhali, mambo kumbe iko Kidatu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Mabibi na mabwana hii clip inajieleza wazi:

Kumbe mambo yote ya hii kadhia yenye sura ya mgawo yako kidatu?

Kumeagizwa bearings hivi zinatengenezwa. Matengenezo yake tokea kwake beberu yanachukua muda kama clip inavyojieleza.

Tuwe na subira kidogo mwali wetu anakua.

Hata kama walisema ng'ombe wa maskini hazai, wetu watake wasitake lazima azae na azae jike!

Ninawasilisha.
 
Hawa kina Mrema na mwenzake Mkama tokea kule pande za kisarawe, hawa tunawaita ni "Mbagusiro" tu. Kwa kiswahili "Mbuzi wa kafara."

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Ndiyo Maana mtanzania kuajiriwa na makampuni ya kigeni ni Kwa sababu tu Sheria zimelazimisha, lakini ki ukweli kabisa, Watanzania wengi ni wazembe na wanapenda zaidi starehe kuliko kazi

Watu wenyewe wawapo kazini, mmoja akijituma utawasikia wakimponda kusema, unateseeka,Kwani Kampuni ni ya babako??
 
Tatizo la huyu mtanzania linasonga na kuishia wapi basi mkuu?

Wewe ukimsikia hata anahoji ya chanjo leo, anaaminika kweri huyu?
 
Bado sana....
2.5237386834090598E18.jpg
 
Mabibi na mabwana hii clip inajieleza wazi:

View attachment 1720216

Kumbe mambo yote ya hii kadhia yenye sura ya mgawo yako kidatu?

Kumeagizwa bearings hivi zinatengenezwa. Matengenezo yake tokea kwake beberu yanachukua muda kama clip inavyojieleza.

Tuwe na subira kidogo mwali wetu anakua.

Hata kama walisema ng'ombe wa maskini hazai, wetu watake wasitake lazima azae na azae jike!

Ninawasilisha.
Hao watumishi wa Tanesco wanaowajibishwa wanaonewa tu. Taratibu za manunuzi za nchi yetu kwa mfumo wa PPRA zinajulikana. Inaweza kuchukua hata miezi 10 kuagiza bidhaa kupitia mfumo huo na taratibu zake. Ukifuatilia kwa undani lazima utakuta watumishi wametimiza majukumu yao.
 
Tatizo la huyu mtanzania linasonga na kuishia wapi basi mkuu?

Wewe ukimsikia hata anahoji ya chanjo leo, anaaminika kweri huyu?

..wakati wa kampeni za 2015 Magufuli alidai kuwa mgao ni suala la kutengeneza.

..alikwenda mbali na kudai eti kuna watu Tanesco wanafungulia maji toka kwenye dams za kuzalisha umeme ili kusababisha mgao.

..kampeni zilipokwisha sikuona mtu yeyote toka Tanesco akishtakiwa. pia sijamsikia tena Magufuli akirudia madai hayo.
 
Usanii si usanii labda kama ni ushamba!
 
Mabibi na mabwana hii clip inajieleza wazi:

View attachment 1720216

Kumbe mambo yote ya hii kadhia yenye sura ya mgawo yako kidatu?

Kumeagizwa bearings hivi zinatengenezwa. Matengenezo yake tokea kwake beberu yanachukua muda kama clip inavyojieleza.

Tuwe na subira kidogo mwali wetu anakua.

Hata kama walisema ng'ombe wa maskini hazai, wetu watake wasitake lazima azae na azae jike!

Ninawasilisha.
Waliua kiwanda cha Mang'ula kilichokuwa na uwezo mkubwa sana kwenye uchongaji wa vyuma sasa tunasubiri huruma ya mabeberu
 
Ndiyo Maana mtanzania kuajiriwa na makampuni ya kigeni ni Kwa sababu tu Sheria zimelazimisha, lakini ki ukweli kabisa, Watanzania wengi ni wazembe na wanapenda zaidi starehe kuliko kazi

Watu wenyewe wawapo kazini, mmoja akijituma utawasikia wakimponda kusema, unateseeka,Kwani Kampuni ni ya babako??
[emoji23][emoji23][emoji23]kampuni ya babaako
 
Waliua kiwanda cha Mang'ula kilichokuwa na uwezo mkubwa sana kwenye uchongaji wa vyuma sasa tunasubiri huruma ya mabeberu

Bila kuwapo jitihada za makusudi za kuwatolea uvivu watu hawa:

IMG_20210218_174254_207.jpg

Tungali na safari ndefu sana.

Hawa jamaa ni mzigo. Hawalisaidii taifa hili na hawana mchango wowote.

Matatizo hukabiliwa si kwa kuyakimbia au kuyatafutia majina mapya.
 
Mabibi na mabwana hii clip inajieleza wazi:

View attachment 1720216

Kumbe mambo yote ya hii kadhia yenye sura ya mgawo yako kidatu?

Kumeagizwa bearings hivi zinatengenezwa. Matengenezo yake tokea kwake beberu yanachukua muda kama clip inavyojieleza.

Tuwe na subira kidogo mwali wetu anakua.

Hata kama walisema ng'ombe wa maskini hazai, wetu watake wasitake lazima azae na azae jike!

Ninawasilisha.
Nimemsikia Waziri anamlinda MD

Ina maana MD hakuwa anajua kama bearing hazijanunuliwa?
Je hakuona umuhimu wa kufuatilia hilo?
Je fedha ya manunuzizi alikuwa nayo nani?
Au watu wa manunuzi walipewa fedha za kwenda kununua vifaa wakakaa nazo?

Lakini MD huyohuyo alikuweko huko siku chache akiutangazia umma kuwa maji yapo ya kutosha na hakutakuwa na wasiwasi juu ya kuwepo kwa umeme wa kutosha.
 
..wakati wa kampeni za 2015 Magufuli alidai kuwa mgao ni suala la kutengeneza.

..alikwenda mbali na kudai eti kuna watu Tanesco wanafungulia maji toka kwenye dams za kuzalisha umeme ili kusababisha mgao.

..kampeni zilipokwisha sikuona mtu yeyote toka Tanesco akishtakiwa. pia sijamsikia tena Magufuli akirudia madai hayo.
Kipindi hicho alipita pale daraja la Mtera akakuta bwawa halina maji kabisaaaaa!!!
Viboko walikuwa wanagaagaa kwenye tope la madimbwi machache ya maji hali ilikuwa tete
 
Nimemsikia Waziri anamlinda MD

Ina maana MD hakuwa anajua kama bearing hazijanunuliwa?
Je hakuona umuhimu wa kufuatilia hilo?
Je fedha ya manunuzizi alikuwa nayo nani?
Au watu wa manunuzi walipewa fedha za kwenda kununua vifaa wakakaa nazo?

Lakini MD huyohuyo alikuweko huko siku chache akiutangazia umma kuwa maji yapo ya kutosha na hakutakuwa na wasiwasi juu ya kuwepo kwa umeme wa kutosha.

Waziri mwenyewe hicho kikombe kumpitia pembeni si kwa sababu ya ugetegete wa huko kwetu tu?

Kujidhania tu nchi tajiri ni kujilisha upepo kweri kweri.

Itamchukua miezi minne beberu kututengenezea bearings labda hizo ambazo labda hata ni mbili tu au hata moja. Hatuna namna inabidi kusubiria.

Bearings ni vitu obvious na hatuwezi kutengeneza. Sembuse chanjo?

Bado tunajishasha kuwa na uwezo wa kukagua ubora wa chanjo zake?

Wajameni, pole pole basi!
 
Back
Top Bottom