Hongera mkuu kwa kujikwamua na kutengeneza nafasi za ajira kwa waTz wenzako pia. Kama
ZeMarcopolo alivyosema jitahidini sana kuzitambua bidhaa halisi na zile feki ili katika kazi zenu muwe makini na muwe na msimamo wa dhati kuwa hamtatumia bidhaa feki kwa kazi yeyote. Vilevile uadilifu na uaminifu ni vitu cha muhimu sana. Mnapochukua kazi ya mteja fanyeni kama ni kazi yenu wenyewe bila kuchakachua kwa namna yoyote ile. Hii itawajengea jina zuri kwa jamii hivyo kuwavutia watu wengi. Trust me, mtaanza kidogo kidogo na hatimaye mtakuwa na kampuni kubwa ambalo mnaweza kuwa na link ya moja kwa moja na makampuni yanayotengeza bidhaa za ubora kutoka katika nchi zinazoaminika kwa viwango kama vile Ujerumani, Uingereza, Sweden, Marekani etc. Nawatakia kila la heri.