Umejipanga kufanya nini ukifika umri huo?

Umejipanga kufanya nini ukifika umri huo?

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
19,147
Reaction score
43,079
Kuna umri utafika utakua peke yako au na houseboy wako au housegirl wako.
Muombe Mungu umri huo ukukute na mke au mume.

Umri ambao utakua unapokea simu za kuambiwa mzee fulani kafariki,umri wa kuambiwa uliesoma nae amepigwa stroke mwili mzima. Umri wa kuambiwa rafiki yenu kafariki ghafla tu,umri wa kupata taarifa za ndoa kuvunjika na kuambiwa wale watoto siyo damu ya ndugu yenu ni alipachikiwa tu.

Umri ambao utatakiwa kuanza kula kwa muongozo wa daktari na kufanya kazi kwa maelekezo ya mtaalamu wa afya au wa saikolojia.

Umri ambao marafiki zako hawapokei simu zako kwa wakati,siyo kwa makusudi bali wanapambania namna ya kuishi katika utaratibu mpya maana utaratibu wa ujana umeshaisha.

Umri ambao nyumba yako itakua kubwa na tupu kama hakuna wanaoishi, watoto wapo mbali kikazi wana maisha yao au wapo masomoni mbali. Vyumba ulivyojenga kwa ajili yao havina kazi tena vinajaa vumbi tu na buibui.

Umri ambao utakua unatoka mwenyewe kwenda baa kunywa au kwenda hoteli kula na utarudi mwenyewe. Rafiki zako watakua wahudumu watakua wanaakufurahia kwasababu ya stori zako za ujanani.

Umri huo kila mtu ana muda wa kuuanza. Wengine miaka 40 wengine 50 na wengine 60.
 
Mkuu tukiambiwa fainali uzeen ndio huo cha muhimu ni kutafuta pesa mkuu ukiwa na pesa uwezi ukawa mpweke watu na ndugu na wajukuu watakuja wenyewe huwezi ukawa mpweke wanajua tukienda kwa babu tutakula.vizuri tutapata.msaada wa hapa na pale sasa kama huna pesa na hukutafuta ukiwa kijana ndio hawa mambo unayosema yatakuwepo
 
Uzeeni hakuna fainali fainali inachezwa ujanani huko uzeeni unapewa kombe lako la ushindi km ulicheza fyongo ukashika mkia kwenye msimamo wa ligi ndio imekula kwako
Ok msg sent kwa hio cha muhimu ni kuwa pesa
 
Kwanza kabisa kutunza afya, hata ukiwa na kipato cha kawaida utaishi vizuri na kwa furaha.

Haina maana una pesa halafu kila siku kuugua, kwenye simu una namba 10 za madaktari.
 
Maisha ya upweke mbona nimeanza kuishi tokea huu ujana.. so hata km nikifikia huko sitakuwa na stress sana, labda tu ugonjwa unikute ambazo hii ni uncertainty tu
 
What goes around comes around.

Kama uliishi vizuri ujanani, ukatengeneza familia bora, ukatimiza majukumu yako na ukawapa upendo wote wanao na mama yao. Basi uzeeni ni kula bata tu.
 
Nini kilitokea hadi mtoto wa miaka minne aishi kwa upweke?
 
Back
Top Bottom