Umejiandaaje pale Familia yako itakapokutenga?

Umejiandaaje pale Familia yako itakapokutenga?

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,046
Reaction score
92,823
UTAFANYAJE PALE FAMILIA YAKO ITAKAPO KUTENGA?

Anaandika, Robert Heriel

Pengine hujawahi fikiri, na wengi hatufikirii Jambo hili, hata likitokea tunaona Kama ndoto Fulani hivi.
"Watoto wangu wanitenge? Haiwezekani!"
" Mke au mume wangu anitenge? Haiwezekaniki!"
Wengi hufikiri hivyo, tena wengine huzijali familia ZAO Kwa upendo mwingi mwingine upendo uliopitiliza.

Lakini kama kuna Jambo ambalo kizazi cha sasa kinapaswa kulitarajia basi ni SUALA LA KUTENGWA NA FAMILIA YAKO.
Ninaposema Familia yako ninamaanisha Wewe, mwenza wako na watoto wako. Sio familia ya wazazi wako,

Dunia ya leo imekaa kimtego mtego, akili zaidi ni muhimu kuliko Imani na hisia.
Kuitenga akili yako ni kuiharibu future yako.

Taikon Kwa jicho pevu linaniambia kuwa miaka ijayo wengi wetu tutatengwa Kama sio kutelekezwa na wanafamilia zetu wenyewe, watoto wetu tuliowazaa Sisi wenyewe, na wenza wetu tuliowapenda Kwa mioyo yeti na kuwatumikia Kwa miaka mingi.

Swali: je Tumejiandaaje?

Pengine usinielewe vizuri, pengine wengine wakaniona Taikon nimechanganyikiwa na kuvurugwa na mambo kichwani. Ila siku zote Taikon ni mtu ninayeyazungumza mambo Kwa uwazi pasipo kumpendelea yeyote.

Siku moja hautaamini, watoto uliowasomesha na kuvuja jasho na damu ili wafanikiwe wakikutenga na kukuona kero, wala sio mbali ni kesho kutwa tuu.

Swali; umejipangaje?

Niliwahi kusema; maisha kila siku yanatufundisha kujitegemea wenyewe na kumtegemea Mungu pekee yake ili tuwe na furaha ya kweli. Kwa maana furaha ya kweli ipo katika kujitegemea na kumtegemea Mungu.

Hujanielewa?

Jipange, jiandae, jidhatii na Linda hatma yako.
Hatma yako usiiache Kwa yeyote Yule hasa Kwa dunia ya sasa. Hutak kuniamini? Shauri yako!

Ni siku hiyo ukisikia Huyu mtoto sio wakwako ndipo utakapomkumbuka Taikon baada ya yeye kufanikiwa.

Ni siku hiyo mtoto wako WA kumzaa atakapo kuambia Baba/mama; familia yake nayo inamhitaji, inamajukumu mengi hivyo anashindwa kukuhudumia. Ndipo utakaponikumbuka Taikon wa Fasihi.

Ni siku hiyo ukimsikia Mkeo akikuambia tuachane tugawane Mali. Ndipo utakaposema ewaa! Taikon

Ni siku hiyo Mumeo atakapo kufurusha uondoke nyumbani kwenu anataka kuoa mke mwingine, utasema kuna mtu aliitwa Taikon aliwahi sema haya.
Binadamu hawakumbukagi Mema siku zote wanakumbuka mabaya Kwa sababu ya ubinafsi na ubaya walionao

Nataka kukuambia, hakuna anayependa kuombwa ombwa hasa akiwa anashida zake pia. Hata Mungu aliyekuumba hapendi uombeombe kwake.

Kila mtu atabeba msalaba wake, hiyo ni SHERIA muhimu kila mtu mwenye akili lazima aiweke kichwani.

Baba au Mama kumuomba omba mwanao kutamfanya akutenge, kutamfanya asikusalimie mara Kwa mara kwani anajua kila akikusalimia kazi yako kulia shida. UTATENGWA! Utake usitake.

Taikon huwaga nasemaga ukweli wote hata kama unauma, najua wanadamu wengi wanapenda kujionyesha kuwa ni wema na hiyo huwafanya kuwa wanafiki.

Ili usitengwe kuna mambo lazima uwe nayo!

Lazima uhangaike kuyapata, ukifanikiwa kuyapata basi huenda utakuwa umejiweka katika nafasi nzuri ya kutokutengwa.

Ni lazima tujipange vijana, usije ukawa Kama Mpumbavu ukasema siku hizi hatuzeeki hivyo unaponda maisha bila kujiandaa na Pambano lako la mwisho la uzeeni. Unasema utakufa kabla ya uzee, haya vipi usipokufa, miaka sabini ikakukuta upo Duniani na huna hili wala lile.

Mjini pamekushinda kununua viwanja basi nenda vijijini Huko kanunue mashamba walau ya laki 3. Jenga kibanda hata cha matope ukijiandaa na Pambano la mwisho.

Andaa mazingira, tafuta Maeneo potential Kwa ajili ya kujihami.

Sio ununue Maeneo yasiyoeleweka, tabia ya nchi mbovu, hakuna rutuba na wala hakuna mifumo ya maji Kama mito au mabwawa.

Eneo kubwa mi muhimu kwani litakusaidia kuendeshea shughuli zako, kama kufuga kuku, Mbuzi, ng'ombe, kupanda Miti ya matunda na kulima wakati mwingine.

Angalau uwe na heka tano mahali kabla ya miaka 45 Kwa ajili ya kujiandaa wewe Kama wewe endapo utatelekezwa au kususwa.

Usijeiga Wahindi maana kuna Vijana wajinga Sana. Unaiga wahindi kwani wewe mhindi?
Unaiga Wazungu kwani wewe Mzungu?

Kila jamii inamifumo yake ndugu zanguni.

Mbali na Ardhi Kama utapata nafasi JIPANGE kuwa na miradi mingine midogo midogo ambayo utakusaidia pindi ukitelekezwa.

Vijana wa siku hizi usiwategemee hata kidogo, watakutelekeza hapo licha ya kuwa wewe ndiye Mama au Baba Yao.

Ninayo mifano ya kutosha juu ya hili. Ikiwa mifano hii inatokea miaka hii, hujiuliza miaka ishirini au thelasini ijayo wakati wewe ukiwa Mzee itakuwaje?

Kumbuka binadamu ni mnyama aliyeji-brand, Kama unavyoona Wanyama wanavyoishi ndivyo Sisi tutakavyoishi huko mbeleni.

Usizae Kwa lengo la kuja kusaidiwa na watoto.

JIPANGE.

Mumeo au Mkeo huyo IPO siku anaweza kukushangaza. Je umejipangaje?

Sisemi ili uishi Kwa hofu, bali najaribu kuelezea uhalisia ambao wengi hawaupendi.

Tena Bora zamani, mitoto ya kike siku hizi imejawa na ubinafsi,

Likitaka kuolewa na wewe litajiangalia lenyewe litapata nini, utaweza kulitunza, utaweza kutunza watoto wake na kuwasomesha, utaweza kuisaidia familia yake!

Kamwe hayafikirii kuwa litakusaidia vipi wewe ili ufanikiwe, yanachowaza ni maslahi Yao.
Mkizaa watoto, linasubiri wajiweze kidogo wakishafikia umri wa utafutaji sio ajabu Hilo limwanamke likakuacha na sio ajabu watoto wasiwe wakwako.

Siku zote Taikon huwaga nasema, kabla hujaoa au kuolewa ni lazima uwe umeshaijua hatma yako.

Niishie hapa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
"Me siwezi kuhangaika kutafuta ada ya mtoto wangu wakati huohuo nitafute na pesa za matibabu yako, uwezo huo sina"
Maneno hayo aliambiwa bibi yangu na mwanae wa kwanza wa kiume( me namuita anko). Bibi akajibu kiunyonge... sawa we endelea kutafuta ada ya mwanao.

Bibi tumemzika mwaka huu mwezi wa kwanza, r.i.p bibi najua uliumia sana.

Vijana tuishi kwa tahadhari sana, tusione sifa kusomesha watoto shule za mamilioni halafu tukajisahau kujitengenezea maisha yetu ya baadae. Watoto wa siku hz hawaaminiki hata kidogo

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
"Me siwezi kuhangaika kutafuta ada ya mtoto wangu wakati huohuo nitafute na pesa za matibabu yako, uwezo huo sina"
Maneno hayo aliambiwa bibi yangu na mwanae wa kwanza wa kiume( me namuita anko). Bibi akajibu kiunyonge... sawa we endelea kutafuta ada ya mwanao.

Bibi tumemzika mwaka huu mwezi wa kwanza, r.i.p bibi najua uliumia sana.

Vijana tuishi kwa tahadhari sana, tusione sifa kusomesha watoto shule za mamilioni halafu tukajisahau kujitengenezea maisha yetu ya baadae. Watoto wa siku hz hawaaminiki hata kidogo

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app


Subiri uone malipo ya huyo Kijana.

Bibi anamakosa yake, (simhukumu)
Kijana naye anamakosa yake (simhukumu)
 
Taikoni la fasihi[emoji1488]MAANDISHI YENYE WELEDI WA KIWANGO CHA LAMI
 
Hapa issue ni moja tu ,kuwa na pesa uzeeni ....watoto ndio watakuwa wanakupigia simu wanakuja kwako kukutembelea ....! Mimi mwenyewe nimeanza kukwepa simu za mzee maana kila muda ni kuhitaji pesa pesa pesa tu ....hata nikitaka kumpigia hata kama ninasalio huwa nafikilia sanaa....!


Kusema kweli uzeeni kama haitakuwa na vyanzo vyako vya pesa utaonekana kero ...
 
Hapa issue ni moja tu ,kuwa na pesa uzeeni ....watoto ndio watakuwa wanakupigia simu wanakuja kwako kukutembelea ....! Mimi mwenyewe nimeanza kukwepa simu za mzee maana kila muda ni kuhitaji pesa pesa pesa tu ....hata nikitaka kumpigia hata kama ninasalio huwa nafikilia sanaa....!


Kusema kweli uzeeni kama haitakuwa na vyanzo vyako vya pesa utaonekana kero ...


🤣🤣🤣

"Mimi mwenyewe nimeanza kukwepa simu za mzee maana kila muda ni kuhitaji pesa pesa pesa tu ....hata nikitaka kumpigia hata kama ninasalio huwa nafikilia sanaa....!"
 
Back
Top Bottom