Umeishia wapi mradi wa Commuter Trains Dar?

Umeishia wapi mradi wa Commuter Trains Dar?

Maneno Meier

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2013
Posts
2,466
Reaction score
1,700
​


Naam! Naipongeza serikali ya ndugu zetu wakenya kwa kutambua umuhimu wa kuondoa kero za wananchi wao wanazopata kila siku ya Mungu kwenye misongamano ya magari barabarani kwa ku-introduce Commuter Rail Network mjini Nairobi.

Uamuzi huu ni kitendo ambacho kinatakiwa kuigwa na kila serikali ya nchi ambayo iko katika harakati ya kukuza uchumi wa nchi yake kama Tanzania. Ama kwa uhakika wakenya nao wakiamua mambo yao basi huyatekeleza kwa kishindo.

Ni kitu cha kushangaza sana kuona serikali yetu ya nchi tajiri kama Tanzania yenye
wasomi wengi wa fani za mechanical na civil engineering ikawaacha wasomi hao kuzurura barabarani na vyeti vyao kwenye mabahasha ya kaki na briefcases wakitafuta kazi, wakati serikali yetu na ya nchi yenye rasilimali nyingi inashindwa kuwatumia wasomi hao kwenye mradi kama huu ambao utawawezesha vijana wetu kupata ajira na vile vike kupanua maarifa yao.

Rais Magufuli kama wataalam wa kutengeneza Rail Network kutoka Tanga mpaka Arusha tunao, kuna ugumu gani wa ku-introduce Commuter Rail Network yetu wenyewe kwenye jiji letu kama wakenya wanavyo fanya? Kwani kuna teknolojia gani ya ajabu ambayo watanzania watashindwa kuitekeleza?

Kama watanzani wenyewe wameweza kui-revive railway yetu ya kutoka Tanga mpaka Arusha kupitia Korogwe, Same na Moshi na inafanya kazi vizuri, kwanini sasa tushindwe kuwatumia wataalam haohao kuweka mfumo huo wa usafiri kwenye jiji letu la biashara?

Niiombe serikali yetu, isiwe inapoteza mda na pesa nyingi za umma kwa kutafuta makandarasi wa kufanya usanifu wa kina au yakinifu wakati watu wetu wenyewe vigezo hivyo ambavyo hao makadarasi wanavyo, tunao? Nina uhakika wataalam wetu walio jenga reli ya Tanga na Arusha wangeweza tekeleta hiyo kazi kwa urahisi mkubwa, endapo serikali ingewapa huo mradi kuutekeleza.

Kwa kutumia makampuni ya nje kwenye kika mradi haitusaidii sisi kitu, kwani matokeo tunayo yapata ni miradi kucheleweshwa na pia kuzinufaisha nchi nyingine kifedha ambazo zingeweza kutuletea faida sisi wenyewe kwa kuwa na mzungungiko wa fedha ndani.

Kwa kuanza mradi huu hatuhitaji treni za umeme kama za SGR, kuna treni nzuri zinazo tumia diesel au betri au Oxygen na Haydrogen gases ambazo ziko very very efficient. Wajerumani wanazo treni za aina hii na wanazitumia kwenye baadhi ya majimbo yao, kwa mfano kwenye kipande cha miji kati ya Bautzen na Goerlitz na Krefeld na Klewe.

Treni za namna hii mimi naona zingerahisisha sana usafiri wa Dar na vitongoji vyake jirania badala ya mabasi ya mwendo kasi. Mbali na hiyo karakana na treni zenyewe zingetoa ajira kibao na pia wasomi wetu kupanua maarifa.

Rais Magufuli nakuomba chonde chonde usirudishe mfumo wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es salaam ambao umefeli. Rais Nyerere alijitahidi sana kuleta mfumo wa mabasi ya UDA, lakini uliuwawa na watanzania wenyewe. Huu mfumo wa mabasi ya mwendo kasi utadumu tu katika kipindi chako. Ukiondoka madarakani watanzania watauua tena. Hivi sasa naona mabasi mengi yamesha anza kuharibika na hayafanyiwi Service ya kutosha.

Angalia kwa mfano ule mfumo wa mashine za kukatia Tickets vituoni, wenyewe nao kwenye baadhi ya vituo umeshaanza kufa. Sijui hao watendaji wako wamesha kupa hiyo taarifa? Nenda mwenyewe ukakague kwenye hivyo vituo utajionea mambo ya ajabu yanayofanywa na watu ambao wamepeqa majukumu ya kuuendesha mradi huu.

Tanzania hakuna mtu anajihisi kuwa yeye ni responsible kwa mali za umma, kila mmoja anataka mali za umma zimnufaishe yeye tu.
Kwa hali hii nahisi kuwa sisi wengi wetu bado ni masokwe. Hatuna ule uwezo wa kutambua kuwa vitu vizuri vipya vinahitaji kutunzwa.

Hizo mashine za kukatia ticket automatic wanaziua kwa makusudi ili waweze kupata nafasi ya kuiba fedha. Ndiyo lengo lao.

Najiuliza kila mara kama wakati walivyo zifunga hizo mashine hakukuwepo na watu walio kuwa trained utaalam wa kurekebisha au kuzifanyia service hizo mashine, punde zinapo haribika au kuwa na defect?

Watanzania tunataka short cut ya kupata pesa bila kufanya kazi. Ndiyo maana naamini Commuter system itasaidia sana kuondoa ubadlifu huu, kwa sababu vifaa vingi vya treni hawawezi vitumia kwenye shughuli nyingine.

Tanzania tunahitaji Generation nyingine na sio hii tuliyo nayo ya kuanzia Mwalim Nyerere mpaka Rais Kikwete. Tanzania tunahitaji Generation ya Magufuli!
Screenshot_20201103-225633_Google.jpg
 
Utapoteza muda wako kusikiliza ahadi Hewa.

1. Dodoma alituahidi ujenzi wa uwanja wa Michezo kabla ya 2020 kashindwa.

2. Alituahidi ujenzi wa kiwanja cha ndege Msalato kabla ya 2020 kashindwa.

3 Dodoma alituahidi ujenzi wa Barabara ya Mduara kashindwa.

4. Ujenzi wa Hospitali ya UHURU kabla ya 2020 kashindwa.

NI MTU WA AHADI HEWA.
 
Hivi UDA limepatwa na nini mbona silioni?

Tujue kwanza kuvisimamia vidogo halafu ndio tuje kwenye makubwa yanayofanana na hayo.
 
​
Naam! Naipongeza serikali ya ndugu zetu wakenya kwa kutambua umuhimu wa kuondoa kero za wananchi wao wanazopata kila siku ya Mungu kwenye misongamano ya magari barabarani kwa ku-introduce Commuter Rail Network mjini Nairobi...
Asipokujibu, muulize mhutu mwenziye, Rais wa Burundi.
 
Back
Top Bottom